Hatimaye pikipiki yangu niliyonunua wiki mbili zilizopita imenikanda.

Hatimaye pikipiki yangu niliyonunua wiki mbili zilizopita imenikanda.

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
5,102
Reaction score
14,024
Asante Mungu kwa nafasi nyingine madhara yangeweza kuwa makubwa kama kupoteza uhai ama kiungo chochote lakini umeamua kunipa majereha ambayo nimeweza kuyahimili na lesson kadhaa juu ya kuendesha pikipiki pia kujiandaa kwa majanga yasiyotabirika.

I don't blame anyone kwani kabla ya kununua pikipiki na kuifanya kuwa means ya transport kwenye harakati zangu nilishashuhudia ndugu, jamaa na marafiki wakipoteza uhai ama kupata majereha ya kudumu kutokana na pikipiki but I decide to take that risk nikijua even me naweza kupoteza maisha kutokana na pikipiki.

Jana kama kawaida nimemaliza harakati zangu mitaa ya uhasibu mishale ya saa tano kasoro usiku nikawasha chombo yangu nakuanza safari ya kuitafuta mbezi all is well mpaka kufika mitaa ya matumbi kinaanza kimvua fulani kidogo kidogo mjuba sina habari nakomaa nacho mpaka nafika kibo mvua inazidi naamua kusimama na kujificha kwenye kituo cha mwendokasi pikipiki kibao ila wote tunajikinga na mvua.

Mvua imepungua mhuni nawasha chombo kuanza kuitafuta mbezi naimaliza kimara mwisho naingia njia ya mwendokasi mvua inarudi sasa kwa kutokuwa na experience naamua kukimbiza pikipiki ili niwahi kufika mvua isinichakaze kumbe ndio naenda kujichimbia kaburi tatizo linakuwa giza plus mvua so sioni mbali kuhamaki road blocks hizi hapa nikanyage breki nishushe gia pikipiki ikateleza nipo chini nimelaliwa na pikipiki upande wa kulia wote chapu nikaamuka mwili hauna ushirikiano kabisa nimesimama najaribu kunyanyua pikipiki niendelee na safari nashindwa

sababu ni night kali na nilipoanguka ni mbali na kituo cha daladala no one anakuja kunipa support nimesimama kama dk mbili namuona mtu anapita namuomba msaada wa kuninyanyulia pikipiki anafanya hivyo namuomba aniendeshe mpaka geto mbezi anadai hajui pikipiki vizuri naona sio kesi nakaa kwenye pikipiki nawasha naanza kuondoka mpaka kituo kinachofuata mkono wa kulia unakataa nikaona hapa nitakuja kupigwa na semi ikabidi nipaki pembeni ni make call kwa jirani yangu aje anichukue kweli anakuja ananiendesha mpaka home huku nikimpa info ya kilichotokea.

Nafika home ananisaidia kuingiza pikipiki ndani na kunielekeza nipashe maji nijikande na anasepa ile navua shati naona bega la kulia limeenda upande na mkono kama umelegea stress zinaanza mfukoni nimebakiwa na elfu kumi na tano tu nafanyaje nimpigie bimkubwa nasita sababu alinikataza kuendesha pikipiki mjini najikaza natoka nje natafuta boda ya kunipeleka dispensary mwamba ananiambia nauli afu tatu nampa nimefika nikiwa na hisia napata msaada wananiambia hawana X-ray niende boch ama hospitali ya wilaya ubungo.

Bochi ipo karibu ila ni private nikienda nitakuja kutafutana ugomvi na ndugu kulipa invoice kubwa naamua nijikaze kwenda kimara hospitali ya serikali napanda bajaji buku mfukoni nabakiwa na elfu kumi na moja nimefika naambiwa nitowe buku tatu ya kujisajili na kumuona daktari chapu natoa hela naelekeza chumba cha daktari kufika huko naambiwa inabidi nifanyiwe x ray nikalipe afu kumi na tano mapokezi ili wajue impact ya ajali money is not enough nabembeleza kwa ahadi ya kulipa asubuhi nakubaliwa

Nafanyiwa X ray good news sijavunjika ila nimeteguka bega inabidi waninyooshe mpunga unahitajika ili huduma ziendelee wakuu tutafute hela huwezi kukosa watu wa kukuchangia ila jinsi hela za matibabu zinavyopatikana ndio mtihani kwa sisi tusio na financial stability.

Asante kwa wote waliniosupport katika nyakati hizi ngumu na mnisamehe kwa usumbufu
 
Ulipoandika 'hatimaye' nikafahamu ulishatoa post kuhusu pikipiki yako..
Nadhani ulikuwa unasubiri tuchimbue makaburi...


www.jamiiforums.com_threads_yawezekana-kujifunza-pikipiki-siku-moja-ya-kesho-ili-jumatatu-nian...png
 
Back
Top Bottom