ElBaradei
Member
- May 4, 2017
- 40
- 14
Wadau habari za mida tena. Baada ya uchunguzi wa kina kabisa jana nimefanikiwa kuthibitisha kuwa WCF tayari watu wapo kazini. Baada ya written ya 18/03/2017 ilipita kama wiki 2 tu na mwezi April mwanzoni wateule walitumiwa meseji za kuhudhuria oral interview na kufikia tarehe 17/04 /2017 walipatiwa offer za kusaini na kurejesha makao makuu. Tarehe 01/05/2017 walireport kazini rasmi. Nimeleta habari hii ili kuwataarifu wale wenzangu na mimi wanaosubiria majibu mpaka leo. Tusahau kuhusu WCF na sasa tuendelee kusaka sehemu zingine na kuachana na ndoto za mchana za kusubiria penye hamna. Vijana wenzangu wa kitanzania tujaribu kutafuta namna za kujiajiri na sio kutegemea ajira za sekta rasmi. Jiulize .... Tanzania kuna graduates wangapi na ulinganishe na idadi ya taasisi, mashirika,kampuni, viwanda na sekta yoyote ile iwe ya imma au binafsi na utambue umri wa kustaafu ni 60+ .... Wale waliokua wanaota ndoto za mchana kwamba kuna list ya oral itatoka basi amkeni sasa.....