Hatimaye nimefanikisha

Hasira ya nini ndugu yangu, ungedanganya watoto wenzako huko mtaani, mtu mwenye uwezo wa ufanya biashara na kuwa na kuwa na savings ya 45m lazima awe na Biashara nzuri na inayoendelea, sasa inaonekana wewe hiyo 45m yote ndo ilikuwa maisha yako, sasa kwa nini usiwe mwongo we mwongo?
Logic (mantiki)
 
na hapo ndio nilikosea
kwa dunia ya sasa ipuka sana kuuza au kununua kitu chochote chenye thamani pasipo ushahidi au mkataba unaotambulika kisheria bila kukosa mashahidi unaowaamini,binafsi kwa dunia ya sasa ilivyo digital biashara kama ya gari above 10mil. Lazima ntachukua na kaclip kaushahidi at the time tunacornfim makabidhiano
 
Nmewahi kudhulumiwa gari na jamaa yangu tena classmates wang nilimuamin Sana nilivopata majanga nkadhan ndo atansaidia kumbe kaenda kunitia ndimu na gari langu kabeba kisa blue card ilikua bado ina jina lake.Wallah sintokuja kumsahau Pole Sana metalkelfin nkihadithia ya kwangu ya kwako yana afadhali ila pole Sana bro
Pole pia mkuu.wengi hudhani ni stori za kufikirika
 
Kuna mambo mengine tunamuhusisha Mungu mpaka anatushangaa.
Hivi dunia ya leo, bank kibao unatembea na cash 45ml mnalipana 10ml kienyeji tu kama majirani wanavyopeana chumvi halafu ooh Mungu. Huu udwanzi.
Hata kununua shamba siku hizi kama inazidi million kwa nini msiandikiane na muuzaji ndo mje wote bank unamlipa kila mtu njia yake kuepusha kubeba pesa??
Tuwe tunajiongeza
Mkuu tunajifunza kwa makosa
 
kwa dunia ya sasa ipuka sana kuuza au kununua kitu chochote chenye thamani pasipo ushahidi au mkataba unaotambulika kisheria bila kukosa mashahidi unaowaamini,binafsi kwa dunia ya sasa ilivyo digital biashara kama ya gari above 10mil. Lazima ntachukua na kaclip kaushahidi at the time tunacornfim makabidhiano
Ni kweli aisee
 
Pole sana najua ilitokea bahati mbaya hukufkiria kama itakua ivyo ilo nifunzo kwn siku yapili hutopigwa kizembe usiwaze piga moyo konde
 
Ndugu hivi karibuni nilikuja na nyuzi za kulalamika kuhusu matatizo yalionikumba.

ISSUE ILIKUA HIVI
Nilikua kwenye gari binafsi natoka arusha kwenda iringa.nilikua na kiasi cha pesa kwenye gari kama 45 million kwa ajili ya shamba na kununua gari mtu anayeniuzia yupo iringa na ndiye aliyenichezea mchezo.

Baada ya kufika Iringa tuliuziana gari nilimpa million 12 nkabakiwa na 33 million. Usiku huo nililala kwa huyo jamaa aliyeniuzia gari nikaamka na kuanza safari nikiwa na gari niliyoinunua kwenda kununua drip pipe za shambani nikiwa njiani kwanza nilikamatwa kwa kosa la gari kuwa na spotlight.

Pili nilikuwa sina leseni(umri wangu mdogo ulichangia mimi kusumbuliwa zaidi).nililipa faini na kuondoka kwa speed kali nikiwa na hasira

Kufika eneo la tanangozi mbele yangu kulikuwa na gari kubwa na kuna njiapanda inapandisha juu mkono wa kulia kuna jamaa alikuwa na noah ghafla baada ya gari kubwa kupita akaingia barabarani kwa kuwa nilikua kasi sana nikamgonga ubavuni gari yake ikarushwa ng'ambo ya barabara, yangu ikachomoka tyre la upande wa kulia na ikaendelea kwenda na mbele kuna basi la New force limesimama.

Gari ilikuwa inavutia barabara nikajtahidi kuitoa ikaenda kupindukia kwenye kabonde kushoto niliumia uti wa mgongo nikachubuka na mkononi kidogo.

Basi maaskari wakaja kupima pale wakakuta mi sina leseni na yule jamaa wa kwenye noah hana leseni mi nikapelekwa hospitali.

Matatizo yalianza kwani niliibiwa pesa zangu zote pale kwenye ajali lakini cha kushangaza yule jamaa aliyeniuzia gari alichukua gari lile na kwenda kulitengeneza huku akiwaambia watu sikumpa hela yote hivyo bado ananidai.

Wiki mwanamke wangu(sijamuoa ni msichana nilikuwa naishi nae tu kishkaji)eti akauza baadhi ya vitu na kurudi kwao Bukoba kwa kweli nilichanganyikiwa pesa niliyoitafta kwa shida leo narudi kuwa fukara.

Baada ya kuandika uzi hapa nikiomba msaada kuna jamaa ni wakili alinisaidia kunihamisha hospital na nilivyoruhusiwa baada ya kutoka alinipa pesa za kuanzia upya maisha kama laki tatu hivi.

Namshukuru Mungu nipo mtaani napambana upya ila Koku bado nakupenda Mumy uje tuishi pamoja.

Raymond gari nilikumalizia hela yote sikutaka tuandikishane sababu nakujua ila nakudai unasema nikupe million saba, ya nini bro? nitakachokufanyia hutonisahau bado napambana na maisha upya ila kaa ukijua nitapambana na wewe hata ukiwa maiti.

Kitu nitakachokufanyia itabaki historia kwa kizazi chako chote sitakuacha salama, nakuahidi ukoo wako wote watanilaumu kwa nitakachokifanya.
Jamaa aliyekuuzia gari alitokea wapi hapo kwenye ajali??...stori yako yakufikirika zaidi........
 
Lakini uliwezaje kununua gari kwa milioni 12 alafu msiandikiane? Hapo shule yako imekusaidiaje? Je ungekamatwa ukaambiwa kuwa hiyo gari imeibiwa kwa mtu ungesemaje?
 
Back
Top Bottom