Hatimaye nafunga ndoa, hakika huyu binti anastahili kuolewa

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Aug 2, 2022
1,465
4,675
Ni safari ya miaka 9 ya kufahamiana nae, ni jirani yangu kutoka huko mkoa wenye Mawe mengi zaidi.

Nilimfahamu kanisani nikiwa likizo ya masomo (nimetoka advance) yeye akiwa o-level form two binti mdogo sana asiyejua chochote kile, hapo ndipo safari yetu ya kufahamiana ilipoanzia.

Kwa akili yangu ya kipindi kile niliona kama napita tu wala sikua na mawazo yoyote kwamba tungefika nae umbali wote huu.

Miaka ikaanza kukatika nikaenda chuo mpaka nikamaliza tuko nae mpaka nikapata kazi bado tupo wote.

Kwa kipindi choote cha miaka 9 (tokea namfahamu mpaka tukaanza mapenzi), tumepitia mambo mengi sana, sio furaha tu pia matatizo.

Nilipokua chuo nilifanya mistake nikawa na mwanamke Mwingine Japo alikuja kujua baadae baada ya Mimi kumaliza chuo, alilalamika na kunung'unika sana Japo hakuniacha alinisihi sana nijitahidi tukamilishe ndoto tuliyoianza miaka iliyopita.

Nimeshamfanyia vingi tu vibaya kwenye safari yetu vingine alijua vingine hakujua, alijua kwamba nimemtongoza rafiki yake akaishia tu kulalamika (miaka mingi iliyopita).

Amekua akiniombea sana kwa Mungu na amekua akionyesha mapenzi ya kweli kwangu, kiukweli kabisa katika miaka yoote hiyo sijawahi kuona akionyesha dharau au mabadiliko yoyote yale, anaweza kua ameshanicheat kwa sababu biblia inasema tuishi nao kwa akili but nikiwa nae sijawahi kuona/kugundua kama ana mahusiano mengine, inaweza kua ni ngumu sana kumpa simu yangu akinishtukiza lakini kwake anytime anaweza kunipa simu yake.

Kwenye safari ya miaka 9 (tokea namfahamu) kiukweli nimekutana na mabinti wengi tu wenye character tofauti na wengine ni smart sana kuliko yeye, wenye juhudi sana kuliko yeye na wapambanaji kuliko yeye but still nasonga nae.

Niko kwenye miaka ya kati sina pressure yoyote ya kuoa lakini nataka nikatoe mahali nifunge ndoa nichukue jiko kabla ya mwezi wa 6, maana kwao nilishaenda kujitambulisha rasmi Japo najulikana kama nilivyosema awali ni jirani yangu.

Wakuu niulize swali moja hapa sidhani kama litakua na maana sana? Je mwanamke anaweza kubadilika baada ya kuingia kwenye ndoa?

Lengo la kuoa mapema sana naona malengo yangu yatafika nikiwa na mke, mfano Mimi ni mtumishi nataka nifungue biashara na amini kwa jinsi tulivyo wadogo na kama akili yake ikiwa ina charge tunaweza fika mbali zaidi, maana yeye ndio atakua muangalizi wa mambo ambayo nitayaanzisha.

Samahani sana wadau natoroka chama naenda kwenye chama kingine.
 
Ana tako kama huyu?
289454114_733343784648913_8471023617399913620_n.jpeg
 
Wanaume wngi hamjui kuvet wnawake ambao ni long term material

'Ooh Bro ananifanyia hivi, bro ananifanyia vile'

'ananipa kila nachotaka, anakuja kila napomuhitaji' i need to marry her ....

Ashawahi kutakwa/ kudate na mtu aliyekuzidi value? Alibehave vipi? Mwanamke yoyote anaweza kuwa loyal ikiwa hana options.
 
Ni kweli kabisa unalolisema mkuu
 
Wanaume wngi hamjui kuvet wnawake ambao ni long term material

'Ooh Bro ananifanyia hivi, bro ananifanyia vile'

'ananipa kila nachotaka, anakuja kila napomuhitaji' i need to marry her ....

Ashawahi kutakwa/ kudate na mtu aliyekuzidi value? Alibehave vipi? Mwanamke yoyote anaweza kuwa loyal ikiwa hana options.
Ni miaka 9 sasa sidhani kama hajawai kukutana na mtu alienizidi maisha, wapo wengi tu na Mara nyingi huwa tunapiga nae story kama rafiki ananiambia vingi tu, labda ni kwa sababu ya sumu ambazo nimeshamuambukiza na commitment yangu kwake.
 
Back
Top Bottom