mlinzi mlalafofofo
JF-Expert Member
- Apr 20, 2008
- 277
- 548
Inafahamika kuwa ndoa ni kitovu cha malezi na makuzi bora katika jamii yoyote duniani. Nje ya ndoa mtu wa aina yoyote anaweza kuzalishwa, mzuri au mbaya, japo mara nyingi uwezekano mkubwa ni kuzaliwa kwa machokoraa, wala ngada n.k.
Imesikika mara nyingi kuwa moja ya sababu kubwa ya watu kushindwa kuoana ni hali ngumu ya kiuchumi.
Kwaiyo basi mimi mlinzi mlalafofofo kama mlipa kodi halali naishauri serikali yangu kugharamia harusi ya kwanza ya mja awaye yoyote ndani ya jamhuri ili kama taifa tuwawezeshe wale wote wenye nia ya kuishi katika muungano wa ndoa.
Kwa wale wote wanaoendelea kuishi kama mke na mume wakipika na kupakua miaka na miaka bila kuwa na mpango wowote wa kuingia makubaliano ya ndoa, watu wa aina hii wamulikwe na sheria na ikiwezekana wakamatwe na kuhojiwa sababu ya wao kufanya hivyo.
Au nasema urongo wajameni?