Hatimaye naenda kuoa Moshi mke wa pili raha jipe mwenyewe

Naenda Moshi kwetu kwa ajili ya kufunga ndoa baada ya karibia miezi 3 toka niachane na mke wangu ambaye tumeishi miaka kadhaa na tumebahatika kuwa na watoto pia

Nilileta huu uzi humu jukwaani

Nimejifunza kwenye maisha hakuna kitu kizuri kama kuwa na furaha na amani ya moyo hicho ndo kikubwa tu

Kuna watu wanaishi ndoa za mateso wanavumilia kwamba wanaona wakiachana na wapenzi wao kwamba jamii na watu watawaonaje au watazungumzaje, rafiki yangu tafuta furaha yako na amani ya maisha yako bila kuangalia watu wanasemaje imradi usivunje sheria au kumuudhi mungu

Mimi naenda kufunga ndoa Moshi na mke wangu mpya, Kikubwa furaha tu na amani na ustawi wa maisha tu...

Mipango ya ndoa ilikua toka mwezi mmoja, sasa watu wananiuliza kwanini nimeharakisha kuoa wakati ni miezi tu miwili umetoka kuachana na mkeo wa kwanza,sasa wao wanataka nifanyeje?nikae miaka ndo nioe tena?ili iweje sasa?Na kwanini niishi kibachelor wakati uwezo wa kuoa na kuhudumia mke kila kitu ninao?
Ila kupitia maandiko yako mbalimbali kwenye hili jukwaa, wewe kuishi na mke ni ngumu. Nahisi hata huyo unayekwenda kuoa utaachana naye tu
 
Ww ndio ulikuwa shida mmeachana miezi mitatu sahivi unafunga ndoa kweli acheni kuwalaumu wanawake tatizo kubwa utakuwa ww, nenda kafunge Ila hiyo ndoa huenda haitadumu mwisho wa siku tutasikia unanyemelea kwa bi mkubwa yetu macho kikubwa uzima tu
Kwahiyo unataka nikae hivi hivi nikifanya zinaa?
 
Kwahiyo angekaa miaka miwili ndio yeye asingekuwa tatizo?? Kwa kukaa miaka miwili ndio ataonekana mtalaka wake ndio alikuwa tatizo??

Mbona huu wako ni uwezo mdogo sana wa kufikiri ndugu???

Halafu eti unamtilia nuksi kwa kutomtakia kheri katika ndoa yake. Hakujui humjui, binaadam bhana.

Njooni muwaone wachawi huku jamani
Kabisa hata mm jamaa kanishangaza
 
Wanawake wanalilia Sana ndoa shida uanza wakishapata cheti cha ndoa na kuzaa watoto,uikaribisha ndoa kwa shetani, vurugu mechi,mume anavurugwa anavurugika riziki hazikai kwenye vurugu.
Mume ukimbia akikimbia sababu ya upumbavu wa mwanamke,mwanamke uanza kumtangaza mme mabaya kakimbia katelekeza watoto,uanza kukimbilia kwa waganga na kujazana kwa mwaposa kukanyaga mafuta ya urudisho.
Wanawake wengi wanaolia makanisa asilimia kubwa wao ndio chanzo cha kuzivuruga ndoa zao.
Wanaamini kelele ni suluhisho.
Mwanaume na kelele ni vitu viwili tofauti.
Viumbe visivyopenda kelele duniani ni mwanaume na dolphin.
Wanawake waelewa huwa ni wapotezeaji,wapotezeaji wengi ndo ndoa zao zinadumu na sio hawa wa haki SAwa wa kucopy kwenye tamthilia.
Maana lengo kuu la tamthilia zote ni kubomoa ndoa sio za kiswahili, korea,kihindi,kizungu,nk madirector wanajua nini ajenda au wanatumika bila kujua na darksiders.
Umeandika kweli mkuu
 
Athari za kelele za wanawake kwa mume.

1.Makelele ndio chanzo cha wanaume wengi kushinda bar hadi saa sita usiku wakiamini watamkuta mpiga kelele amelala.
2.Kupungua kwa nguvu za kiume maana mnyama mkali apendi kelele.
3.Wanaume kutembea nje
4.Kupotea au kupungua kwa riziki nyumbani,nyumba yenye kelele roho Mtakatifu anatoka nduki akai, shetani ndo ushika usukani.
5.Magonjwa ya kupalalaizi kupooza, pressure,moyo.
Wanawake wengi kelele zao ndio chanzo cha vifo vingi vya wanaume,wanaume hawana uwezo wa kuhimili kelele au kueleza matatizo yake nje.

Wanawake mkiacha kelele mtaponya ndoa zetu maana mume, kelele uwaondoa wanaume majumbani.
Wanawake wasio na kelele ndoa zao huwa zinadumu.
Kelele za nini kupotezea kuna wacost nini?
KILA kitu mwataka mjue,mfatilie, muulize,nk kumtaka mwanaume awe mtakavyo ni SAwa na kuyapandisha maji milimani.
Tutajitahidi kuacha kelele, ila napo kukaa mda mrefu bila kelele na kuongea ongea ni mtihani
 
Tutajitahidi kuacha kelele, ila napo kukaa mda mrefu bila kelele na kuongea ongea ni mtihani
Tunajua mnatoa sumu lakini hizo sumu mnapotoa ndizo zinazowaathiriki waume,we ukitoa unapata nafuu mume anapokea Yale maneno makali,machafu yakiingia kwa mume ni sumu mbaya sana,yenye kuleta madhara hayo.
1.upungufu wa nguvu za kiume
2.mume kuchelewa kurudi home kukwepa kelele
3.Vimada
4.Mume kuwa mlevi
5.magonjwa ya moyo
6 Kupungua kwa kipato, nyumba yenye kelele Malaika mleta pesa akai ukimbia Malaika mleta pesa akai nyumba chafu.
Sababu wanaume tunayabeba moyoni na atuyaongei kuyatapika.
7.Vifo vya mapema vya wanaume
 
Tutajitahidi kuacha kelele, ila napo kukaa mda mrefu bila kelele na kuongea ongea ni mtihani
Ukitaka kuishi vizuri na mmeo mmpotezee KILA afanyalo,take easy utaona ndoa inaenda tu kwa amani,shida je wanawake wanaweza? Wakati siku hizi tamthilia ndio Mwalimu wenu.Mnaiga na kucopy KILA kitu kwenye zile tamthilia,zile ni program za freemason lengo kuu ni kubomoa misingi ya familia, wahusika wa tamthilia wanaweza wakawa wanajua au awajui wanatumika.
 
Huyo mke aliyekuacha alikuwa sahihi 100% maana kichwani kwako una chuki kuhusu Israel na Marekani. Hauna kitu kipya zaidi ya kuwaza vita na vifo tu akaona ipo siku unaweza kumdedisha.
Hata huyu usipojirekebisha lazima akukimbie maana akiingia JF anakutana nyuzi Oh Israel atachakazwa akimchokoza Iran, Iran ametengeneza mabomu kwa ajili ya kuipiga Israel. Marekani karibia watu 20000 wanakufa kila siku. Anaona huyu hamna kitu.
Naenda Moshi kwetu kwa ajili ya kufunga ndoa baada ya karibia miezi 3 toka niachane na mke wangu ambaye tumeishi miaka kadhaa na tumebahatika kuwa na watoto pia

Nilileta huu uzi humu jukwaani

Nimejifunza kwenye maisha hakuna kitu kizuri kama kuwa na furaha na amani ya moyo hicho ndo kikubwa tu

Kuna watu wanaishi ndoa za mateso wanavumilia kwamba wanaona wakiachana na wapenzi wao kwamba jamii na watu watawaonaje au watazungumzaje, rafiki yangu tafuta furaha yako na amani ya maisha yako bila kuangalia watu wanasemaje imradi usivunje sheria au kumuudhi mungu

Mimi naenda kufunga ndoa Moshi na mke wangu mpya, Kikubwa furaha tu na amani na ustawi wa maisha tu...

Mipango ya ndoa ilikua toka mwezi mmoja, sasa watu wananiuliza kwanini nimeharakisha kuoa wakati ni miezi tu miwili umetoka kuachana na mkeo wa kwanza,sasa wao wanataka nifanyeje?nikae miaka ndo nioe tena?ili iweje sasa?Na kwanini niishi kibachelor wakati uwezo wa kuoa na kuhudumia mke kila kitu ninao?
 
Mchepuko amekuroga uachane na mkeo ili umpe second chance na imekuwa, umeshajaa mkononi mwa mchepuko!

Kichwa kimeshakuvurugika!
 
Back
Top Bottom