DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,212
- 4,517
Habarini za asubuhi wakuu,
Moja kwa moja kwenye mada tajwa. Ni hivi, mpaka sasa inaonekana viongozi wa mataifa yenye ushawishi pamoja na wataalamu wa afya wameona ukweli kwamba UVIKO-19 ni ugonjwa ambao tunalazimika kuishi nao.
Wametambua kwamba pamoja na kuchanja, ngoma bado inaendelea kuenea, pamoja na kufunga mipaka, mara barakoa, mziki uko palepale. Lakini zaidi ya yote kuna jambo ambalo nahisi limewafungua macho zaidi, kwamba idadi ya maambukizi inakuwa juu sana, wanaopona pia wanakuwa wengi huku kukiwa na idadi ndogo sana ya vifo.
Maana yake ni kwamba huu ni ugonjwa ambao kweli unaoua ila zaidi wale wenye umri mkubwa na wenye matatizo mengine ya kiafya. Kwa watu wasio na matatizo mengine ya kiafya na siyo wazee, idadi ya vifo ni vichache sana.
Mimi wiki iliyopita nimeshuhudia mtu wangu wa karibu ameupata UVIKO-19 ila mimi sikuipata, cha kushangaza mwenzangu hakuwa na maumivu makali wala nini. Haiogopeshi hata kidogo kwa mtazamo wangu.
Kibaya zaidi, huu ugonjwa haujawaua waafrika kama kind Gates walivyotabiria kwamba waafrika wataokotwa mitaani wakifa kama mende. Hili ni jambo la kufurahia sana.
Mataifa mengi ya Ulaya yameanza kulrgeza masharti na kufungua mipaka yao ili kuruhusu maisha ya rudi kama kawaida.
Inawezekana mpaka ifikapo msimu wa joto tutakuwa watu huru duniani kote.