Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
ishara ya vidole viwili inayofanana na herufi V ni ishara inayotumiwa na watu wanaotaka mabadiliko.hapa nchini ishara hii hutumiwa na chama cha chadema ikiwa ni alama rasmi iliyopamba bendera ya chama hiki.
Kwa wale wanaowafahamu wamasai watakubaliana na mimi kwamba ni kabila pekee hapa tanzania au east africa kwa ujumla lisilotaka mabadiliko.
lugha yao,mavazi na mfumo wao wa maisha umepita vikwazo vingi vya mabadiliko.
Leo mgombea ubunge wa arumeru mashariki kupitia chadema ameonekana kukonga nyoyo za morani wa kimasai na kusababisha morani hao kurukaruka, kuinua mikono hewani,kukunja ngumi iliyoacha vidole viwili na hivyo kuunda alama ya mabadiliko.
hatimaye wamasai wamekubali kukombolewa.....!!!
Kwa wachambuzi wa mambo ya saikolojia mtakubaliana na mimi kwamba huu ni ujumbe mkubwa kwa chama tawala huko arumeru.
Naomba mwenye video clip ya taarifa ya habari ya itv leo usiku aiweke ili tujionee uhondo.