Hatimaye Lowassa abomoa hadhi ya CHADEMA

Hatimaye Lowassa abomoa hadhi ya CHADEMA

Watanzania tuwe makini katika kuchagua tuchague viongozi waadilifu,wachapakazi,na pia wenye uzalendo wa kweli na wapenda maendeleo
 
LOWASA ABOMOA HADHI YA CHADEMA:

Mgombea wa nafasi ya uraisi ndio kiini cha kampeni katika chama husika,kwa mara ya kwanza,taifa la tanzania linashuhudia maajabu ya mgombea wa nafasi ya urais kupitia umoja wa UKAWA Ndg: E. Lowassa akipigiwa debe kwa asilimia 97% na wapambe wake badala ya kujinadi mwenyewe.

Katika wagombea nafasi ya urais waliojitokeza mwaka huu 2015,Bw. Lowassa ni ni mgombea pekee ambae ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kushindwa hata kujibu shutuma dhidi yake,kueleza sera za chama kwa ufasaha,amekuwa mgombea ambae kwa kiasi kikubwa anatetewa kwa kila jambo na wapambe wake badala ya kujitetea mwenyewe.

Tathimini inayoonekana ni kwamba Chama cha CHADEMA kwa sasa kimepoteza misimamo yake juu ya hoja za upingaji masuala ya ufisadi na rushwa.Agenda hizi zilikuwa zikiibeba kwa kiasi kikubwa chama hicho kiasi hata cha kuweza kupata wabunge wa kutosha bungeni na kuunda kambi ya upinzani kipindi cha bunge la 2010/15.

Kupitia ajenda hizo ndipo wakina Mnyika, Lisu, Msigwa, Lema waliweza kujulikana kwa uhodari wao wa kuongea.Tujiulize wako wapi sasa makamanda hao na kauli zao?Kwa sasa CHADEMA wamekuwa kama wakiwa baada ya kuukumbatia ufisadi,chama kimekuwa bubu kiasi cha kinashindwa hata kuzungumza uzaifu wa mgombea wao na juu ya hali yake kiafya ilhali hata kwa macho anaonekana.

Watanzania tujiulize?Kipi kilichojificha juu ya suala hilo?Ni kweli Lowassa alitoa fedha kwa mbowe kununua chama ili agombee urais?Nini anakiitaji huko ikulu?Kama wapiga debe wake ndio wenye mamlaka kiasi cha kuzungumza mambo juu yake,akiwa rais nani atakaeongoza nchi?Kwa dalili hizi Lowassa anafaa kweli kupewa nchi?

Tafakari mpiga kura.

Naona umekuja kasi! Hata wenzako walikuja na speed kama yako lakini sasahivi wengi tu wako ukawa! Utatuelewa tu mpaka ikifika 25 oct kura yako tunayo!
 
Ninyi ndio mliowekwa hapo millenium towers kijitonyama kufanya ujinga huu!! Hizo pesa na ziwe laana kwenu na uzao wenu.
 
Ukweli mnaupata lakini sema vichwa vinakuwa vigumu kuelewa mnahitaji elimu ya ziada kwa ajili ya kujitambua.

Niongezee vijana wa IT tuongeze nguvu kwenye mitandao. Tujitahidi wadau hali yetu ni mbaya huko field
 
Kamua ukawa, kamua ukawa
 

Attachments

  • 1442606538988.jpg
    1442606538988.jpg
    44.3 KB · Views: 175
Kukumbatia maji kama jiwe ni ujinga wajomba, acha uchu wao wa madaraka uwaadhibu
 
Ukkosa la kuongea kuhusu mafunguo, unaamua tu kumkaba lowassa....
Mbn kikwete analonga sana lkn kashindw kuongoz nchi?????
 
Mafisadi papa kama Lowasa sisi wanainchi hatutaki hata kusikia sauti zao,walizokula zinawatosha.
 
unataka fisadi aingie ikulu ili iweje hatutaki huo ufisadi kafanyeni na mafisadi wenzenu.

CCM kiboko mpaka makarani mafisadi wana mijengo hataree. ...mara elfu kumi fisadi mmoja kuliko ccm mafisadi laki tano
 
Kupigana vita inataka Afya bora na. Kumbu kumbi ii ujue umeweka wapi silaha yako kwani huwezi tena kukumbushwa 👏
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom