Mradi wa maji wa miji 28 Kilwa umeanza kunufaisha Wananchi kupitia uwekezaji mkubwa wa Serikali

Mradi wa maji wa miji 28 Kilwa umeanza kunufaisha Wananchi kupitia uwekezaji mkubwa wa Serikali

Wizara ya Maji

Govt Institution
Joined
Oct 2, 2024
Posts
32
Reaction score
19
3.jpeg
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) amekagua mradi huo na kuona utekelezaji wake akielekeza maunganisho mapya ya huduma ya maji kwa wananchi wa Mavuji iwe siku Saba tu.

Mhe. Aweso akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mavuji, Kilwa Masoko , mkoani Lindi baada ya kufungua maji ya bomba ya mradi mwishoni mwa wiki Septemba 26, amesisitiza kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa mazingira Kilwa Masoko (KIMUWASA) na Mamlaka za maji nchini huduma ya maunganisho ya maji majumbani isizidi siku Saba.

"Sasa niwasihi sana watendaji wa Wizara ya Maji mradi umekamilika na umeanza kutoa huduma, sasa maunganisho mapya yasizidi siku saba, sio mwananchi anaomba kuunganishiwa maji unamwambia njoo kesho, njoo kesho ili mradi atoe kidogo dogo, hizo zilipendwa" Waziri Aweso amesema.

Mradi wa maji wa miji 28 Kilwa unathamani ya kiasi cha Shilingi za Tanzania Bilioni 44 na utekelezaji umefika asilimia 94.3 ambapo umeanza kutoa huduma ya maji kwa wakazi wa kijiji cha Mavuji. Mradi huo utanufaisha wakazi zaidi ya 59,983 ambapo lita milioni 5 .5 za maji zitazalishwa kwa siku kutoka mto Mavuji.
2.jpeg

1.jpeg
 

Attachments

  • 1.jpeg
    1.jpeg
    216.2 KB · Views: 3
  • 2.jpeg
    2.jpeg
    140.2 KB · Views: 5
  • 3.jpeg
    3.jpeg
    168.3 KB · Views: 6
Back
Top Bottom