Hatimaye Joseph Kabila akubali kung'atuka madarakani

Hatimaye Joseph Kabila akubali kung'atuka madarakani

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,623
Reaction score
8,427
45004482_304.jpg


Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametangaza Jumatano kwamba hatogombea katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ametangaza Jumatano kwamba hatogombea katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu.

Hatua hiyo ya Kabila inatuliza wasiwiwasi uliokuwepo miongoni mwa upinzani na Jumuiya za kimataifa kwamba angejaribu kuwania muhula mwingine na kusalia madarakani.

Msemaji wa serikali amesema waziri wa zamani wa mambo ya ndani Emmanuel Ramazani Shadary ambaye kwa sasa ni katibu mkuu wa chama tawala ndiye atakayepeperusha bendera ya chama chake cha kisiasa, mnamo ambapo Congo ikikabiliwa na uchaguzi wa kwanza wa amani na makabidhiano ya madaraka ya kidemokrasia katika historia ya nchi hiyo.

Tangazo hilo limekuja saa chache kabla ya muda wa mwisho wa wagombea kujisajili kukamilika.

Shadary atakuwa mgombea wa muungano wa vyama ulioundwa hivi karibuni wa Common front for Congo.
Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2001, kisheria hawezi kuwania muhula mwingine baada ya muda wake kumalizika mwishoni mwa 2016. Uchaguzi umeahirishwa tangu wakati huo na kuchochea maandamano.

Chanzo: DW
DkEwAM4W0AEKxCe.jpg
 
Hongera JK hakika umetumia busara sana....

Natamani Mr slim plus museven wangekuiga kwa hili...
 
I congrat him in this.
Pandikizi Bemba kuwa raisi. Congo still wont be safe.
 
Rais Joseph Kabila leo hii amejitofautisha na baadhi ya marais wa Afrika kwa kuamua kuheshimu kipindi chake cha uongozi baada ya kuamua kutogombea kwenye uchaguzi mkuu utakao fanyika mwezi Disemba mwaka huu,pongezi nyingi zimfikie na hiyo ni aibu kwa marais wanaojiongezea vipindi vya kuongoza kama wafalme hasa hapa Afrika.
 
Back
Top Bottom