Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 65
So, JF members are not interested in this, are they? Some mining outfit plays police in an otherwise peaceful village in Tanzania, and that does not attract the attention of JF members?
Where are you Mwafrika wa Kike? Its your thread, remember? There was plenty of activity around here when it was rumored that Mzee Mwanakijiji had developed some soft spot towards you. Is this thing of trigger happy guards arresting villagers, for trespassing on the villagers own land, not a whole lot more interesting to you, and even to Mzee Mwanakijiji?
Come on guys, your silence on this is deafening!
Kamati ya Madini ilipewa muda gani naona time is up longtime kama alivyosema bi mdogo hapa. Sasa, tuambiane yameishia wapi..
sasa sijui wataiweka hadharani au hadi Rais aamue kwanza..?
Muda waliopewa wali ulishamalizika, lakini kwa kuwa walikuwa hawajamaliza kazi, wakaomba kuongezewa muda na JK akawapa hadi kati kati ya Aprili. Kwa taarifa nilizonazo, ripoti inakaribia kukamilika na mipango iliyopo ni ikabidhiwe kwa rais kabla ya Aprili 10.
Time is almost up, sijui tutaona usanii mwingine?
Rufiji, naona unanitoa nje ya Dar es Salaam kidogo. Inaelekea Mkapa alikuwa na ulafi sana wa mali, lakini alijenga uchumi zaidi ya waliomtangulia na waliomfuatia. Kuna viongozi corrupt (eg Suharto wa Indonesia) ambao pamoja na mapungufu yao, wanajenga sana uchumi. Mkapa ni wa aina hiyo.
Mkapa alipokea uchumi wenye kasi ya mfumuko wa bei ya 30%. Miaka kumi baadaye alikabidhi uchumi ambao kasi yake ya mfumuko wa bei ilishashuka hadi 4.5% kwa mwaka!
Mkapa alifanikiwa kuondoa deficits kwenye bajeti yetu. Mkapa alileta mapinduzi makuu kwenye civil service, alijenga madaraja na mabarabara, alianzisha mapinduzi makubwa kwenye Elimu, alianza ukarabati wa hospitali zote za serikali, etc. etc.
Lazima niongezee kwamba Mkapa alikuta jeshi (JWTZ) linalovaa viraka akawanunulia nguo na magari. Wote tuliona.
Mkapa hakuwa malaika. Alizalisha sana mali lakini akachota hapo kidogo vile vile. Sina shaka kwamba kama Mkapa angekuwa bado Rais, barabara ya Mtwara hadi Mwanza ingeshamalizika, kasi ya mfumko wa bei kwa sasa ingekuwa kwenye 2.5%, etc. etc.
Baada ya kukurudishia, anomba turudi kwenye mada.
Tunasikilizia ripoti tu..we're still around!Tunataka kuona whats going,what went on and ofcourse what should be done!Jim ,
Nakubalina na wewe kabisa , Augustine Moshi ameonyesha na anazidi kudhihirisha ubias wake inapokuja kwenye ishu ya Mkapa. Aingii akilini kwa mtu kusema ya kuwa Mkapa ameleta maendeleo ya ajabu wakati ukweli ni kuwa Mkapa ametumbukiza nchi yetu kwenye umasikini wa ajabu. Hivi kweli tunaweza kukaa hapa na kusema inflation ilishuka kwa kiasi fulani wakati hata hatujui ni vigezo walivyotumia kupata hiyo figure ?
Vile vile ni lazima tutambue ya kuwa hizo figure zinakuwa cooked na BOT , Jee tutawezaje kutathmini ukweli wa hizo figure ambazo zinatolewa na kina Balali ? Pili huwezi ukasema ya kuwa Nyerere akuhusika na success ya awamu ya kwanza ya Mkapa, ni lazima tutambue ya kuwa kama isingekuwa Nyerere ...mkapa singekuwa rais wa Tanzania . Kwa hiyo JK ndiye aliyemshika mkono na kumpa strategy za jinsi ya kurevamp masuala ya uchumi. Mimi napinga argument ya kusema kwa kuwa simply mtu alifanya makosa fulani hawezi kuyarectify in future.
Mwisho , ni lazima tutambue ya kuwa kama ile mikataba ingeweka manufaa ya mtanzania mbele basi nchi yetu ingeweza kupiga hatua sana . Lakini huyo bwana uchumi unayemsema wewe akujali hilo bali alijali tumbo lake ! Angalia nchi nyingi duniani wanavyotumia rasilimali zao vizuri katika kujenga nchi yao . Moshi angali jinsi Mkapa alichofanya pale bandari Dar es Salaam, pamoja na kwamba wataalamu walimwambia ya kuwa TSCAN kampuni ya Karamagi imetia serikali hasara yeye aliextend muda wa mkataba kwa miaka 10 zaidi....
Kwasababu Mh Rais mwenyewe ameshakubali kuwa mikataba ni mibovu na kinyonyaji..kwanini asisitishe huo uchimbaji/mikataba iliyopita hadi hapo hiyo kamati itakapotoa taarifa na mapendekezo?Ni kwamba kamati ikishatoa taarifa yake kwa Rais, basi Rais ataunda kamati nyingine ya kuaangalia hiyo taarifa na kumwambia inasema nini na afanye nini. Ndio mtindo walio nao hawa "wenzetu".
Wakati haya yote yakiendelea, walafi wanachimba madini kwa kasi kubwa. Kwa nini Rais hawaambii wasitishe uchimbaji kwanza mpaka kieleweke?
Kwa sasa, Kamishina wa Madini anatakiwa atoe tamko la kusitisha uchimbaji mpaka akague usalama wa migodi yote kwanza. Hawapashwi kuendelea kuchimba tu wakati hakuna hata uhakika kwamba wameweka vizuio vya maji ya mvua. Fikiria Watanzania wako kwenye mashimo ardhini wakati hata kitu kidogo cha kuzuia maji ya mvua yanayotiririka yasiingie hakipo!
Nasema wasitishe mpaka kieleweke kwanza!
Kwasababu Mh Rais mwenyewe ameshakubali kuwa mikataba ni mibovu na kinyonyaji..kwanini asisitishe huo uchimbaji/mikataba iliyopita hadi hapo hiyo kamati itakapotoa taarifa na mapendekezo?