Hatimaye Hamad Rashid, Shoka Hamis na wenzao wawili wafukuzwa CUF!

Kuna wakili mmoja kanieleza kwamba kumetokea amri kadha za mahakama kuu ya Bara kuhusu mashauri yaliyoibuka huko Zenj. Akiniletea details za mashauri haya nitayamwaga hapa JF.
 
Jamaini, hakuna lawyers ndani ya JF mwenye uelewa wa majukumu (jurisdiction) ya mahakama kuu ya Tz ili aondoe kabisa hali hii iliyojitokeza?
 
Hata mie nimeshangaa kusoma kuwa Malaria Sugu ni mwandishi wa habari! Duh! Kama ni kweli iko kazi. Natamani kufahamu ni chombo gani cha habari anakiwakilisha.
Huyu jamaa anako ka blog kake ambako kanatembelewa na yeye peke yake. Huko ndiko anakofanyia kazi ya uandishi!
 
Hakika chadema pekee ndio chama kinachomfaa mtu mwenye uchungu wa kweli wa kutetea wananchi,Tumuache maalim seif aendelee na siasa zake za kibaguzi Cuf,najua tatizo kuu ndani ya chama hicho wanataka mtu mwenye rangi kama Ismail Jusa ndio aw katibu mkuu na aende ikulu.Achana nao hao karibu kambini tuwasambaratishe ukija huku 80% uhakika kurudisha jimbo mikononi mwako
Hamad aelekee CCK tu!!!
 
Kwa hilo barubaru yuko sawa na hicho ndicho kilichowapa jeuri CUF kwa kutokusikiliza amri ya mahakama na HR yeye yupo kwenye siasa miaka mingi sana lakini ameshindwa kulitambua hilo.Na kitu chengine cha kusikitisha hao wanaojiita Great thinker hata hawaijui nchi yao, ya kuwa kwa upande wa mahkama tumeungana katika mahkama ya rufaa na hiyo pia baada ya sheria mpya kupitisha hivi karibuni tu itainyima haki mahakama ya rufaa kusikiliza kesi za rufaa kutoka ZNZ.kwa hiyo huyo jaji aliyetoa uamuzi huyo ni kihiyo kwa ameshindwa kuelewa juridiction yake haiwezi kuvuka bahari na kama kikao kingefanya mainland basi CUF ingekuwa na makosa.Jamini someni katiba ya nchi yenu na wacheni kubwabwaja.
 
Ahsantum kwa taarifa.

Hakika alipewa kamba ya kutosha sana ili ajimalize mwenyewe. Na sasa amejimaliza.

Kumbuka kuwa kuna wengi walitimuliwa kuanzia Mapalala, Naila Jidawi na akina Msabaha. Na wote sasa mnawaona wakoje na wanaishi vipi na hishma yao kwa jamii hususan ya kizanzibari ikoje?


Namsikitikia sana Mh Hamad rashid na kumpa pole, choyo na kiu ya madaraka imemponza.




sio kwamba ameona chama kinakosa dira?!
 
kama ni kweli hii inaashiria machafuko mapya zanzibar kati ya watakaokuwa wafuasi wa Hamad na wale wa cuf
 
nnn-564x272.jpg


Historia ya Zanzibar ni ndefu sana katika dunia. Tunaweza kusema pia tarikh ya Zanzibar imechukua muda mrefu kuenea katika ulimwengu. Wanahistoria mbalimbali na hata wa wagunduzi wa kimataifa wameandika mambo mengi na vitabu vingi tofauti tokea mwaka 1980 lakini vyote ukivitizama, ukivusoma na ukiunganisha maudhui yake vinakupa ishara ya kuviona visiwa vya Zanzibar ni katka visiwa vichache vilivyo duniani vilivyo na umaarufu, usataarabu na uwelewa wa mambo kwa watu wake.

Historia hiyo hiyo haikuwacha kuwazungumza wakaaji, wenyeji au wazaliwa wa visiwa hivi kwa mapana na marefu kiasi ambacho imeonyeshwa kwenye maandiko mengi kama wenyeji wa visiwa hivi ni watu walio makini, mahodari, wazalendo na wafuatiliaji na wapambanaji.

Kwa mtiririko huu ndio tunapoona mampambano yameanza mbali tokea hata kabla ya Mreno, kuja kwa Mreno, kung'olewa kwa Mreno, na mapambano mbalimbali hii yote ikionyesha ushujaa wa watu wa visiwa hivi kutetea haki zao. Zama hizo zilipokwisha zama za kisiasa ziliingia kuanzia miaka ya 1957. Siasa ziliingia katika miaka hiyo na zikashamiri katika visiwa vya Unguja na Pemba. Kwa kuwa siasa ilishamiri basin a fitna na khiana nazo zilichukua nafasi yake nazo zikawa sehemu ya harakati hizo za siasa. Matokeo yake yakawa ni mapambano ya ndani yaliyochukua sura ya chuki na kupambana wenyewe kwa wenyewe hadi kupelekea kupotea kwa maisha ya watu wengi na wengi wao wakiwa hawana hatia.

Haya yote yametendeka kwa kuwa tu baadhi ya wahusika walisimamia zaidi ubinafsi wao kuliko maslahi ya wengi. Mduara huu uliozunguka visiwa hivi uliviathiri na kuvipotezea watu wengi maisha yao. Wenine wengi wakahama nchi yao wanayoipenda na kusambaa katika kila pembe ya ulimwengu kwenda kuhuisha uhai wao na hata kufikia kusahau kwao kwenye asili yao, kulikofukiwa vitovu vyao na vya wazee wao. Hawana lawama kwani si makosa yao bali ni makosa ya ubinafsi na khiana za wenye tama.

Nimeanza na utangulizi huu kwa lengo la kukumbusha ili tunapoamua kujadili mambo, matokeo au watu mbali mbali kwa nafasi zao za utumishi wa kinchi au wa kisiasa tunapaswa turudi nyuma kwenye historia yetu ili kwanza kujiangalia na halafu twende mbele kwa kufanya maamuzi yenye busara. Vinginevyo pasi na uangalifu wa kupima kwa mezani iliyo sawa tutakuja kujikuta tunashabikia mambo na kuyamini mambo hayo kinyume na uhalisia wake.

Hali hii ni kama hivi sasa miongoni mwetu tunavyoliona na kulitazama hili sakata la kufukuzwa Hamad Rashid katika chama cha CUF kwa mtazamo ulio mwepesi na kuvutwa na upepo wa hadaa za mwanasiasa aliyejiandaa kutizama ubinafsi wake kuliko dhamira ya kweli ya mapambano iliyotegemewa kuonyeshwa na kusimamiwa na nafsi yake.

Hamad Rashid Mohammed kwa wakati ule, alikuwa ni miongoni mwa vipenzi vya rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius K. Nyerere hata kufikia kwa mwalimu Nyerere kumpa nafasi nyeti ya kuwa naibu waziri wa fedha wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Bila shaka alipata nafasi hii baada ya kukubalika na idara ya usalama wa taifa.

Hata hivyo Hamad Rashid alijiunga na mapambano ya kudai haki za Zanzibar katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa ndani ya CCM pamoja na Maalim Sei.. Jambo hili llipeleea kufukuzwa katika system ya chama cha CCM yeye, Maalim Seif na wenzao wengine wakipewa muda mdogo kujitetea na hapohapo hukumu kufuata.

Alijiunga na vugu vugu la kudai heshima na haki ya Zanzibar ndani ya muungano kabla ya kuundwa kwa vyama vingi vya siasa katika miaka ya 1980. Alishiriki katika kuasisi chama cha CUF mwaka 1992 na vugu vugu lake kubwa lililopelekea watu kuteswa, kufukuzwa makazini, kufungwa na kuuliwa.

Katika uchaguzi wa mwanzo wa vyama vingi 1995 ambao chama cha CUF kilikuwa kikitarajiwa sana kutwaa serikali ya Zanzibar, Hamad Rashid aligombea uwakilishi kwa matarajio ya kuwa waziri wa serikali ya Zanzibar. CUF imekuwa ikinyimwa ushindi wake Zanzibar kwa ubabe unaofanywa na serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kuwa ilifahamika chama cha CUF lengo lake ni kurudishwa kwa dola ya Zanzibar. Baada ya kuuona muelekeo wa siasa za Zanzibar wa kuporwa ushindi kila baada ya uchaguzi kwa nafasi ya urais aliamua kugombea ubunge katika uchaguzi wa pili uliofuatia wa mwaka 2000. Aliendelea kuwa mbunge hadi muda huu anafukuzwa katika CUF.

Mwaka 2009, Maalim Seif na Rais mstaafu Amani Karume walileta maridhiano ya wazanzibari yaliyopelekea kwa mara ya mwanzo kufanyiwa marekebisho ya katiba ya Zanzibar yaliyotamka kuwa Zanzibar ni nchi na kuweka msimamo wa kuyaondoa mafuta katika orodha ya mambo ya muungano. Baada ya kumalizika uchaguzi mkuu wa 2010 serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar iliundwa. Hamad Rashid alitegemea kupata nafasi ya uwaziri katika serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuteuliwa kuwa mwakilishi. Bahati mbaya Hamad Rashid hakuteuliwa kuwa waziri na hivyo suala hili halikumfurahisha.

Serikali ya Jamhuri ya muungano ilimteua Hamad Rashid kuliwakilisha bunge la Tanzania katika bunge linaloziwaklisha nchi za jumuiya ya madola, commonwealth Parliamentary Assembly (CPA) akiwa ni mbunge wa bunge hilo na makamo mwenyekiti wa kamati ya fedha ya bunge hilo. Nafasi hiii alikuwa ameishika kwa muda mrefu mbunge wa CCM, Bwana Mporonyoki. Nafasi hii ni nyeti na kakatifu hapewi mtu isipokuwa anaeaminiwa na CCM. Jambo hili lilimnyima Hamad Rashid muda wa kuwepo bungeni na kulitumikia bunge ipasavyo.

Hivi tujiulize msingi wa mapambano ya Hamad Rashid ndani ya CUF ameutoa wapi ghafla? Kwa nini basi iwe ni ndani ya kindi hichi ambacho chama kinajipanga na mchakato wa katiba mpya ambao ndio msingi mkuu wa kuundwa kwa CUF? Jee hivi kweli agenda yake ya mapambano ni kwamba Maalim Seif anakiuwa chama? Kwamba matawi ya CUF hayafunguliwi? Kwamba Maalim Seif hafanyi ziara Tanzania bara? Kwamba Maalim Seif hakushiriki kampeeni za CUF bara?

Hivi karibuni Hamad Rashid ameuthibitishia umma wa watanzania msimamo wake mpya juu ya mustakbala wa muungano kinyume na msimamo wake ule aliofukuziwa katika CCM na akashiriki kuunda CUF. Msimamo ambao ndio msingi wa mapambano ya wadai haki wa Zanzibar pale alipoulizwa na kutakiwa na mwandishi wa Star TV atoe msimamo wake thabit juu ya muungano tulionao anauonaje, na ana maoni gani juu ya marekebisho ya katiba. Jawabu yake ilikuwa ni kwamba anaamini umoja ni nguvu utengano ni udaifu.

Na yeye mara zote amekua akisimama katika umoja. Wa bara wanaishi Zanzibar na wa Zanzibar wanaishi bara, hivyo ni jambo la kuendelezwa. Kero anayoiona yeye katika muungano ni kwamba mpaka leo hakuna tume ya pamoja ya fedha, jambo ambalo lingeweza kuondoa kero ndogo ndogo zilizopo.

Hivi ni kweli Hamad Rashid alifukuzwa katika CCM kwa kuwa kulikosekana tume ya pamoja ya fedha? Hivi kweli Hamad Rashid alikubali kuachishwa kuwa naibu wazri wa fedha wa Jamhuri ya muungano kwa kukosekana tume ya pamoj ya fedha?. Hivi ni kweli tatizo na kero za Zanzibar katika muungano ni kukosekana kwa tume ya pamoja ya fedha? Hii ndio ile khiana tulioizungumzia kule mwanzo. Hamad Rashid amethibitika sasa hasimami tena katika ile misingi mikuu ya wazanzibari ya kudai haki, hadhi na heshma ya Zanzibar katika muungano. Tokea alipoanza kuvitawala vyombo vya habari kwa kuibua kwake madai dhidi ya CUF hajawahi kusikika kutumia nafasi hiyo kukosoa mfumo wa muungano au kuzizungumzia shida za wazanzibari katika muungano huu.

Hivi karibuni Maalim Seif aliitisha Mkutano wa Hadhara kibanda maiti Unguja wenye lengo la kuwafahamisha wazanzibari juu ya mambo muhimu ya kuzingatiwa wakati wa mchakato wa katiba mpya ikiwemo nafasi, heshma na hadhi ya Zanzibar katika katiba mpya. Hamad Rashid amejitokeza na kutoa machapisho kuhoji uhalali wa Maalim Seif kutoa maelekezo hayo, hasa katika kipengele cha Zanzibar kuwa na benki kuu yake na sarafu yake. Pia pale Maalim Seif aliposema kama ni serikali mbili basi kila mmoja na yake. Lengo lake ni kujaribu kuonyesha kwamba Maalim Seif ni hatari (threat) ndani ya Serikali ya Zanzibar.

Hii ndio ile khiana tulioisema mwanzoni. Kuzusha mgogoro huu ni khiana yake katika kufikia lengo lake. Sayyidna Ali (AS) anasema, "asiyeweza kuficha siri yake hawezi kuficha ya wengine, watu wanafiki hujipamba kwa uongo. Achukiza sana mtu mwenye nyuso mbili". Lakini sasa mma umeshafahamu, khiana haina tena nafasi.

Forward forever! Backword never!
 
Aje lkn asiruhusiwe hata kugombea uongozi wowote ndani ya cdm mpaka miaka10 ipite,
 
"MS alikuwepo Zanzibar. kama Mwandishi wa habari, akishuhudia Hamad Rashid akifurushwa"
Jana Jioni nilikuwa Jos kona Ngome kuu ya Cuf iliopo Soko Muhogo Baada Ali Salehe kuripoti kupitia BBC, washabiki wa CUF
walipiga mayoe kwa furaha, yaani ukiwahoji ni wazi wamemchoka Hamad Rashid.
Saa 1:00 jioni. Mtaa wa Mtendeni, makao makuu ya CUF. cuf haikuzaliwa Arusha. moshi, Tabora. Imezaliwa Malindi na kama kufa itafia malindi, hamad Rashid ziiiiiiiiiii

Saa 2:30 usiku nilipofika maskani ya CUF Jangombe gengeni, mazungumzo Hamad Rashid kesha, akachume karafuu Pemba. hali ni shwari.
Saa 3:00 Usiku. Ngome nyengine ya CUF Jangombe kwa maharuki anapotoka mmoja wa vijana waliofukuzwa yaani Saanani. maneno ni hayo hayo. Aende tu Chadema. acheze na Ndevu za Seif asicheze na akili ya Seif(Maalim seif)
Leo saa2:00 asubuhi. daraja bovu,Ofisi ndogo ya CUF . Hamad rashidi ni m-mboya tu, akatafute Ubunge Moshi. hapa nooo.

Magomeni ngome ya CUF:matangazo yao" Hamad rashid kavuna alichopanda. aanzishe chama Chake, yeye na familia yake"

Vituo vya Magazeti.
Yakheeeeee, kakie hamad umemsikia? eti anataka kuwa mbunge wa Mahakama. kanchoka tena.
Sawa hawa ni wanachama wa CUF Zanzibar - Je, huko bara umekutazama?... Yaani sasa hivi kila mwanaCUF kahamia CCM kwa taarifa yako CUF bara kwisheny...Tatizo lenu mnasahau kwamba kuna Wazanzibara pia yale yale ya Nyerere!...
Utasikia utambi ukiwashwa Tanga na Kusini hivi karibuni.
 
Hivi MS ni mwandishi wa habari??
hizo habari unazoleta na kuziandika zina typing error kibao wanaosoma habari zako wana roho ya Paka...

Mkuu usishangae, watu wengi wanafikiri kujua kuandika ni sawa sawa na kuwa Mwandishi wa habari, ogopa sana watu wa aina hiyo, wengi wamevamia fani na kuihaaribu sana, simply wanajua kuandika matokeo yake tunayaona, any way, katupasha kitu fulani walau
 
Back
Top Bottom