Hatimaye fedha kurudi mitaani

Mkuu hizi habari siyo za kuaminika sana!
 
Inategemea serikali inakwenda kulipa kina nani na hizo pesa. Kama watalipwa wakandarasi ni dhahiri mzunguko hautakuwepo kwani wanufaika ni wachache sasa na pengine pesa nyingine zitahama kwa maana ya manunuzi ya kutoka nje ya nchi.

Labda pesa hizo zikalipe zile million 50 za kila kijiji; walimu na watumishi wengine kama wana madai wakilipwa ndoposa pesa itarudi kwenye mzunguko
 
Nauliza zile billion 900 za mkopo ambaza samia alisema wanazitumia kilipa madeni ya jk bado wanalipa mpaka Leo
 
huyu naye katoka kitivo gani? isijekuwa anatoka idara ya mambo kale leo anachambua uchumi wa nchi
 
Dah!!! Huyu Profesa kiboko. Au wamemnukuu vibaya??
 
Hat mi sio mchumi ila ninacho jua wangesema serikali imeanza kutekeleza baadhi ya miradi ndo hela hurudi mtaani maana sehemu panapo fanyika mradi ajira mbalimbali huanza kupatikana na ndo hela za mtaani zinavyo anza kupatikana
Ngoja mchumi aje kukujubu am out
 
Hii haijakaa sawa.....mfano Mtu afiche chakula chake ndani....kisha aende kuomba chakula kwa jirani....!! Hapa ni kwamba hali ya mambo Kifedha itazidi kuwa ngumu...
 
Yesu urudi sasa, lini unarudi..? kila ishara zimetimia, tunaomba urudi haraka Bwana..

Hadi Prof. wa Chuo Kikuu anasema haya..? Kweli
sielewi anafundisha nn chuo, Serikali kukopa Benki binafsi za ndani, eti itaongeza mzunguko wa fedha mitaani? Wakati hii ni kinyume chake kabisa.. money circulation itakuwa ndogo kuliko ilivyo sasa serikali ikikopa benki binafsi za ndani ndio hali itakuwa ngumu sana..

Ama kweli, ishi uyaone..!!
 

Sio kila mhadhiri anaakili hata proffessor Li alikuwa mhadhiri chuo kikuu
 
Dr.Silas pamoja na kuwa aliwahi kuwa mwalimu wangu ila hapa asee sikubaliani nae,kitendo cha serikali kukopa fedha kwenye mabank binafsi kinapunguza bank liquidity na maana yake bank zitakuwa na uwezo mdogo wa kukopesha wateja wake na itachochea interest rate kuwa juu katika hali kama hiyo pesa kurudi mtaani ni mgumu.
Pia kusudi pesa irudi mtaani lazima tujue inaenda kutumika katika shughuli gani!?serikali ya sasa inatumia fedha nyingi kwenye miradi ambayo return yake ni ya muda mrefu hilo pia linaathiri,hata hiyo miradi wanufaika wake si watu wanaozitumia ama kuziweka fedha hizo hapahapa nchini zinaenda kwenye nchi zao huko sasa hapo fedha inarudi vipi mtaani!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…