Hatimaye Fastjet waanza safari na ndege zao "Mpya"

Hatimaye Fastjet waanza safari na ndege zao "Mpya"

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,944
E 190
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
Fastjet imeshasogeza ndege moja aina ya E190,ambayo itakuwa inafanya safari zake ndani na nje ya nchi.Ndege hiyo imekodiwa toka Kampuni ya ndege ya Bulgaria imeshaanza safari za ndani ya nchi,huku ikitazamiwa kuwa wataongeza nyingine ili kukabiliana na soko la ushindani wa usafiri wa anga Tanzania.

Hii ni dalili kuwa soko la ushindani kati ya ATCL na makampuni binafsi yanayofanya kazi ndani ya soko la ndani ya nchi inaongezeka.Meneja Mkuu wa Fastjet Tz John Corse anasema hili ni ingizo la kwanza tu,wapo mbioni kuongeza nyingine,ili kukabiliana na ushindani wa ndani na kupunguza ghalama za uendeshaji,ambapo hapo awali walipokuwa wanatumia A319,kampuni ilipata sana hasara na kujiendesha kwa kusuasua.

Leo nilikuwa mmoja wa walionja "utamu" wa E190 toka Dsm to Mwanza,ni mwendo wa dakika 50 tu mwanawane;mtu wangu Rockcity native tukutane Jembe Ni Jembe tupasue mifupa ya sato na balimi baridi bia ya mvuvi.

Wazee wa ruchelele,Malimbe na SAUT tukutane Goldcrest ....Sasa ni dakika 50 mate hayajakauka wala mama kuipua mboga mtu upo Dsm from Mwanza.

[HASHTAG]#ATCL[/HASHTAG] tutaendelea kukupenda [HASHTAG]#bombadia[/HASHTAG] ...Hatuachi mbachao kwa msala upitao.
 
View attachment 416413 hio ya kwenu haina spidi kama hii ya kwetu ni dk 30 tu upo mwanza yani hata hujaanza kuhisi njaa umesha tua mwanawane

wadau kama kuna anayejua ubalozi wa dar hapa arusha anielekeze, maana anataka nine nione hizo ndege zinazowaumiza vichwa. Na pia mniambie viza ni tshs ngapi?
Sio vyema sisi mnatuonyesha tu picha.
 
Vipi kati ya hiyo ndege ya FastJet na Bombadier ni ipi inabeba abiria wengi?
 
wadau kama kuna anayejua ubalozi wa dar hapa arusha anielekeze, maana anataka nine nione hizo ndege zinazowaumiza vichwa. Na pia mniambie viza ni tshs ngapi?
Sio vyema sisi mnatuonyesha tu picha.
Upo unga ltd mkabala na nguzo mbili
 
Samahani, hii ndio bombadia, mali mpya, aisee, safi sana. Tumenunua kwa hela yetu wenyewe hii, loh, safi sana, aisle .
Sema kamekondakonda, ila katanenepa tu.


Hahahaaa hahaha
kwa kusemwa kule itanenepaje.
 
Soko la usafiri wa ndege litakuwa na ushindani mkubwa ikiwezekana nauli zidhibitiwe na serikali
 
Back
Top Bottom