Hatimaye Babaj Yawa Zimamoto

heheee kweli viongozi wetu ni unique.
kila siku wanakuja na comedy mpya,kile cha kubebea waja wazito sikuamini macho yangu leo bajaji imekua yakuzimia moto.
 
Huwa sipendi kutumia kauli nzito lakini kwa hili inabidi nitumie.... "SIJAWAHI KUONA VIONGOZI WA NCHI WAPUMBAVU KAMA WALIVYO VIONGOZI WA TANZANIA" yaani wako tayari wenyewe watembelee magari ya milioni 200 na kununua tujigari twa milioni 2 kweli kwa huduma muhimu kama zimamoto na kupeleka wagonjwa hospitali????:bored: Wanakera sana sana hivi hiki kijipikipiki kinaweza kweli kuzima hata kibanda cha kuku kweli!!!
 
Ngoja tusubiri bajaji ijayo itakuwa maalum kwa ajili ya nini?? mi nahisi watabuni bajaji mfano wa trekta...

Bajaj ijayo itatengenezwa kwa ajili ya kuisaidia Taifa Stars ishinde. Itavalishwa jezi ya Taifa stars na kuingizwa uwanjani. CCM oyee
 
Wahindi wameshasoma mawazo ya viongozi wetu kuwa ni finyu, ndo maana wanatengeneza vitu vya ajabu...... NI JUKUMU LETU KUKATAA HIVI VITU. VIONGOZI WETU JAMANI MUWE MACHO NA WAHINDI HAO, NI WAJANJA SANA KWENYE BIASHARA, NA WANAUSHAWISHI MKUBWA SANA KWENYE BIASHARA...... PINDA, NA VIONGOZI WENGINE IKIWEMO MKUU (JK) BE SERIOUS, NA MUWE MAKINI.............
 
Mkubwa mzima Pinda anashangaa kitu cha kitoto sijui ninini hicho!...Tangu lini bajaji ikawa zima moto jamani?
Hivi vidudud ni kama vile vya kubebea wajawazito, nadhani aliyewasupply vile ndo huyohuyo kaleta na hivi tena!
Amewashika masikio hawafurukuti!..Ashagundua kuwa ni mazezeta wote!...my hairs!

hapo utakuta kinauzwa dola elfu kumi
 
208308_1918882580898_1507034707_32048858_6018225_n.jpg
 
hivi kwanini tusifikirie namna ya kuendeleza teknolojia ya usafiri wa ungo kutoka usafiri wa wachawi na kuufanya usafiri wa umma?
Je research ya uchawi iliyofanywa na Prof wa mlimani ina msaada gani kwa taifa letu?
 
Kinachofuata kuhalalisha dawa ya BABU kama dawa rasmi ya kutibu magonjwa sugu na watagawa kwenye ma hospitali.
 
Linganisha bei ya bajaji na zilizotafunwa EPA, DOWANS, RICHMOND, MEREMETA, TWIN TOWERS, BAE n.k
 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akikagua Bajaj ambayo imetengenezwa ili kumudu kazi ya kuzima moto hasa kwenye maeneo yenye barabara nyembamba katika maonesho yaliyoandaliwa na Kampuni ya Spray and Fumigation Services Limited, bungeni Dodoma Alhamisi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

04_11_bcuf58.jpg

wahindi hao na biashara zao za kifisadi. uliza bei hapo; utacheka ufe.
 
Back
Top Bottom