Hatimaye aliyemchinja yule kada wa CHADEMA Arumeru akamatwa!

Status
Not open for further replies.
MTUHUMIWA HUYO ALMAARUFU KWA JINA LA (CHEWAJA)ALIKUWA NI MPANGAJI KATIKA NYUMBA YA MAREHEMUNI (waliishiwote myumba moja) NI MZALIWA WA SINGIDA,MKAZI WA ARUMERU MASHARIKI,AMEKAMATWA DODOMA AKIWA KWA MGANGA WA KIENYEJI,AWATAJA ALIOSHIRIKIANA NAO KATIKA MAUAJI HAYO MMOJA WAPO NI KADA WA CCM NA PIA NI MWANYEKITI WA KIJIJI,VILIO VILITAWALA BAADA YA MTUHUMIWA HUYO KURUDISHWA KIJIJINI CHINI YA ULINZI MKALI WA JESHI LA POLISI KUONYESHA OLIKOFICHA VIFAA VYA MAUAJI WANANCHI WAPANDWA NA HASIRA WATAKA KUMUUA ASKARI WAZUIA,SILAHA ZAKUTWA SHAMBANI KWA MWENYEKITI ZIKIWA ZIMEFUKIWA CHINI AMBAPO BAADA YA KUFUKUA WALIKUTA BUNDUKI MBILI,KISU PANGA,NA MASHINE YA KUKATIA MITI ILIYO TUMIKA KUMCHINJIA MAREHEMU ALIFANYA MAUAJI HAYO KWA UJIRA WA SHILINGI ZA KITANZANIA MILIONI MBILI(SH.2.000,000/=)YASEMEKANA HATA UKO SINGIDA ALIKIMBIA KESI YA MAUAJI.

source:MIMI MWENYEWE LIVE KUTOKA KATIKA TUKIO.
Hawa jamaa wote inatakiwa kabla ya kuhukumiwa, bunge likae kwa dharura ili kupitisha sheria ya hukumu ya kifo kwa kuchinjwa hadharani, kisha ndipo wahukumiwe kwa humumu hiyo mpya, ni kisha itekelezwe ndani ya saa zisizozidi 24 tangu kutolewa kwake.
 
Hapana shegaboy! Usihukumu haraka hivyo kwamba ccm ni wauaji kwa maana sidhani kama kulikuwa na kikao cha ccm kilichokaa na kupanga mauaji.Kinachotokea Arumeru Mashariki ni kama kilichotokea Nduli Iringa. Ya Iringa tuyaache maana yapo mahakamani. Lipo tatizo za ukereketwa mkali. Wapo wanachama wa ccm ambao wanajiona wao ndo ccm yenyewe. Chama chake kikishindwa anaona ni yeye ameshindwa na anaumia sana kuliko mwenyekiti wake wa taifa. Ndo hao wanafanya vitendo vya ajabu si chama.

Kwa hiyo tofautisha matendo ya mtu binafsi na misimamo ya chama.

Sitakubaliana na wewe kamwe labda hujui waliouawa kisiasa na CCM orodha ni ndefu baadhi tu

Shija, Kibona Kolimba, --------, karibuni Igunga 15, Jaribio la kuwaua wabunge Mwanza, Arumeru mashariki na sisi tunaouawa kiuchumi
 
Lazima kinamwigulu wanamjua, si wa kwao huko singida na kumbukeni wakati wa kampeni igunga dr.slaa alisema kuna kambi ya vijana inafunzwa huko kwa nchemba singida...ebu tukumbushane
Kweli mkuu, ila mie nafikiria zaidi..huyu jamaa inamaana ni profeshono muuji? Ccm walikuwa wanamjua wakamkodi!
Kuna maswali mengi hapa!
 
Haihusiani na siasa, alikuwa mpangaji wake.

Unaweza kuwa sahihi. Lakini soma hiki kipande -labda ulikiruka,

"....AWATAJA ALIOSHIRIKIANA NAO KATIKA MAUAJI HAYO MMOJA WAPO NI KADA WA CCM NA PIA NI MWANYEKITI WA KIJIJI,....VILIO VILITAWALA BAADA YA MTUHUMIWA HUYO KURUDISHWA KIJIJINI CHINI YA ULINZI MKALI WA JESHI LA POLISI KUONYESHA OLIKOFICHA VIFAA VYA MAUAJI ...SILAHA ZAKUTWA SHAMBANI KWA MWENYEKITI ZIKIWA ZIMEFUKIWA CHINI ..."
 
Nikisomaga habari za aina hii huwa najiulizaga adhabu stahili za mtu wa aina hii ni nini?,kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa kisha kurudishwa Gerezani kusubiria kwa miaka mi'5 na zaidi signature ya Rais ili adhabu itekelezwe na si ajabu isitekelezwe kabisa na haya ma'kampeni yao ya kupinga adhabu za vifo siyo muafaka kabisa.
 
Jana Mitaa ya Leganga ilijaa watu wenye mchanganyiko wa hasira na furaha mida ya Jioni baada ya mtuhumiwa wa mauaji kuletwa Leganga.
Wananchi waliomba wapewe japo dakika mbili nae wapoze hasira zao, ilikuwa ni purukushani sana kiasi ilikasoro kidogo sana gari alimowekwa kupinduliwa na wananchi.
Aliletwa ili nyumba yake ikaguliwe. Alikutwa na Silaha tofauti tofauti ikiwamo Bunduki, Panga na mavazi ya kuvaa kuficha uso.

Story Iko Hivi:
Jamaa baada ya tukio la mauaji walikimbia mmoja akakamatiwa Dodoma. Na inasemekana ana history ya kuua. Na vifaa vilivokutwa kwake vimewahi kutumika kwenye uharibifu mwingine.
Inadaiwa gharama ya kufanya tukio hilo ilikuwa ni 2M (Million mbili za kitanzania).


Swala hili linafanyika kisiri sana na watuhumiwa wengine wako ndani kimya kimya.
 
Hawa jamaa wote inatakiwa kabla ya kuhukumiwa, bunge likae kwa dharura ili kupitisha sheria ya hukumu ya kifo kwa kuchinjwa hadharani, kisha ndipo wahukumiwe kwa humumu hiyo mpya, ni kisha itekelezwe ndani ya saa zisizozidi 24 tangu kutolewa kwake.

Naunga mkono na mguu hoja,dawa ya watu wa namna hii ilipaswa iwe ya style hiyo.
 
....kama kulikuwa na ujira inamaanisha kuna mtu iliaajiri kufanya kitendo hicho; je, ni nani huyo? Na ni nani aliwalipa ujira huo?
 
kwahiyo ni muuaji mzoefu. ingependeza sana endapo watu kama hawa wangefanywa kitu ambacho kinakuwa mfano kwa wengine wote.
 
watch out huyo jamaa wa ccm atauwawa kiaina kupoteza ushahidi coz am sure kuna vigogo nyuma yke...hawezi kupata 2m kiulaini namna hiyo

Hilo nalo neno ingewaje si busara sana ku-conclude kwamba yalikuwa ni mauaji ya kisiasa. Kwa sehemu kama Arumeu ambako wananchi wamehamasika sana katika siasa then si ajabu kukuta wengi wao ni makada wa chama fulani na hivyo kila unapotokea uhalifu unaweza kuhusisha makada wa vyama hata kama uhalif huo hautakuwa ni wa kisiasa. ni mtazamo tu,
 
....kama kulikuwa na ujira inamaanisha kuna mtu iliaajiri kufanya kitendo hicho; je, ni nani huyo? Na ni nani aliwalipa ujira huo?

mkuu nataka swali liwe hivi,"Kama kuna ujira maana yake kuna mwaajiri,na kama kuna mwajiri maana yake kuna malengo ya ajira,Swali nani mwajiri na nini lengo la ajira?Polisi wana nia ya dhati kuwatafuta waajiri wa mtuhumiwa?
 
Dah....watu wana roho ngumu sana. Yaani mpaka kuchinjana kwa sababu ya siasa tu!

tena kwa chain saw! My tears are droping remmembering how we cut trees at home then that machine passing on a human neck. Ee Mungu baba wa rehema walaani ccm na watu wao wote kwa kunuia na kutimiza kutuvurugia amani ya nchi yetu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom