Hatimaye ADC yapata Usajili wa Kudumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye ADC yapata Usajili wa Kudumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hasan124, Aug 28, 2012.

 1. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Leo Jumanne tar.28-08-2012 majira ya saa4 hivi za ASUBUHI chama chetu cha ADC kilichojizolea umaarufu mkubwa katika Nyanja za Siasa NCHINI Tanzania hata Kabla ya kuanza rasmi kazi za kisiasa, kimefanikiwa kupata usajili WA kudumu baada ya kukamilisha zoezi la UHAKIKI katika mikoa kumi (10).

  Mikoa iliyohakikiwa na ofisi ya Msajili WA vyama vya Siasa CHINI ya MHE. john Tendwa ni pamoja na Tanga, Mwanza, Pemba, Mara, Unguja, Tabora, Dodoma, Lindi, Mtwara na Dar ES Salaam ambapo chama kilifanikiwa kuvuka idadi iliyo kuwa inahitajika na ofisi ya Msajili ya wanachama wadhamini 200 kwa kila Mkoa.

  Tukio hili la kihistoria linaashiria mwanzo WA Harakati za chama cha ADC katika duru la Siasa NCHINI Tanzania, Kama ambavyo moja kati ya Madhumuni yake kuwa (1) Kushika dola kwa njia halali na za kidemokrasia.
  Akizungumza na waandishi WA Habari mara baada ya kukabidhiwa HATI ya Usajili Mwenyekiti WA ADC TAIFA MHE. Said Miraji alinukuliwa akielezea furaha Yao ya kukamilisha sehemu ya kwanza na nyeti ya kupata usajili WA kudumu na Leo hii katika Hotel ya Lamada Ilala chama kinafanya MKUTANO MKUU WA KWANZA KAMA CHAMA RASMI CHA SIASA ambapo watapata fursa ya kupitisha Katiba ya chama pamoja na Kuchagua viongozi WA Kitaifa WA chama.
  GOD BLESS ALLIANCE FOR DEMOCRATIC CHANGE.

  ADC - DIRA ya Mtanzania.
  +++++++++++++++++++++++++++++++++
  Latest Picture Mkutano Mkuu wa Kwanza ADC Taifa mara baada ya usajili wa kudumu 28-08-2012 Lamada Hotel and Apartment Ilala.

  ADC Mkutano Mkuu.JPG Mkutano Mkuu ADC.JPG
  Wajumbe wa Mkutano Mkuu ADC Taifa.JPG
   
 2. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,614
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Baada ya kulamba posho ya uchaguzi ujao tutawasoma vizuri!
   
 3. Mangaline

  Mangaline JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 1,052
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Karibuni sana katika uwanja wa kupigwa risasi za moto na mabomu ya machozi, labda muwe chama D.
   
 4. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Safari ni ndefu, mpaka mfikie kupigwa mabomu, mjue bado sana.
   
 5. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ccm C. Ulitegemea msipate...? Wadhamini ni wanachama wa ccm.
   
 6. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #6
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Badilisheni hizo rangi za bendera acheni ugense!
   
 7. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Madhumuni yetu ni:
  (1) Kushika Dola kwa njia hatlali na za kidemokrasia.
  (2) Kujenga Umoja na Mshikamano imara kwa waTanzania wote.
  (3) Kujenga uchumi imara na kulinda raslimali za Nchi kwa manufaa ya waTanzania wote.
  (4) KUPINGA KWA NGUVU ZOTE AINA ZOTE ZA UBAGUZI NA UKANDAMIZAJI.
  Naona Namba NNE (4) itakuonyesha msimamo wetu katika Hilo la risasi za moto na mabomu.
   
 8. A

  Aristides Pastory JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hamna jipya Ccm_d
   
 9. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Hicho chama kweli ni mitambo kama wewe ndio wamekupa kazi ya kueneza na unaweka andiko dhaifu hivyo kweli mnayo! karibuni sana.
   
 10. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mzee nimegee ushahidi ili tuwe wote tuwazomee.
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,615
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Walevi wa madaraka,yupo wapi kafulila.mpaka muishikie chadema chini miaka 30 ijayo
   
 12. B

  Big Dady Member

  #12
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilichofanyika ni kuongeza idadi ya vyama na si kupata chama bora. Kama miongoni mwa vyama vilivyopo hawakuona cha kuwafaa unategemea wao wanakuja na jipya gani.
   
 13. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #13
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tunaanza na Bububu Znz ndio mtajua ADC iko vipi.....hatubipu sisi.
   
 14. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #14
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,397
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  . hasan124 Kuna uhusiano wowote kati ya chama hiki na Hamad Rashid Mohamed?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #15
  Aug 28, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,614
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Then we know who you are!
   
 16. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #16
  Aug 28, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  sikua najua kama unguja na pemba ni mikoa asante ADC.
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Aug 28, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,228
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  acha wehu wako, sio kila chama ni ccm.au unataka wote tuwe wachaga ndio uridhike
   
 18. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #18
  Aug 28, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,408
  Likes Received: 1,877
  Trophy Points: 280
  Sera za chama ni muhimu,hiki chama kinafuata mlengo gani wa siasa?
   
 19. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #19
  Aug 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  I hope nyie sie kile chama cha kaskazini kama cha wenzetu fulani wapenda vurugu na kutofuata sheria. Ila hiyo rangi nyekundu kwenu yamaanisha nn? kwani kwa wenzenu ina maana ' TUTAMWAGA DAMU KWA NJIA YOYOTE ILI MRADI TUINGIE IKULU'.

   
 20. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #20
  Aug 28, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  NDIO.......MHE. Hamad Rashid Mohamed ni mlezi WA ADC Kama alivyo Sabodo kwa Chadema.
   
Loading...