HATIMAE, Yameanza kutimia.............. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HATIMAE, Yameanza kutimia..............

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamageuko, Nov 10, 2010.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Asiye na masikio aweke visoda!

  HABARI NDIO HII:

  AKIONEKANA kuguswa na mambo yanavyokwenda ndani ya CCM kuhusu upatikanaji wa mgombea uspika wa Bunge la Muungano, Mbunge mteule wa Maswa, kupitia Chadema John Shibuda amekihadharisha chama hicho tawala.

  Amewataka wana CCM kufanya uamuzi wa busara juu ya kumpitisha mgombea uspika, vinginevyo watakisambaratisha chama hicho.

  Alisema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili muda mfupi baada ya kufika kwenye viwanja vya Bunge kujisajili, ikiwa ni mojawapo ya ratiba za wabunge wote wateule.

  Shibuda alisema kuna kila sababu ya wana CCM kuwa makini katika kumpitisha mgombea uspika vinginevyo watakuwa wanatengeneza mwanya wa kukisambaratisha chama hicho.

  Chanzo; MAGAZETI YA TANZANIA 10 NOV. 2010

  Hapo ndipo mambo yanapoanzia mkiukumbuka UTABIRI ULEEE......
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Mkuu, tuliona hili mapema sana...Leo jioni tutakuwa tushajua mwelekeo kama watajinusuru au kujichimbia kaburi la akiba!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hakuna wakuzuia anguko la ccm, waleta mizaha wameikamata kila kila kona, mafisadi ndio viumbe wenye Nguvu, waadilifu wachache watajitoa miaka michache Ijayo, kuwezesha mabadiliko ya kweli kutokea, ccm inaenda kufa....wala sitakililia, wala sita kizika , mbwa watakula nyama yao.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  sijakuelewa mkuu....
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nilishawahi kusema hapa kuna wapenda madaraka wanahamia upinzani wanapokosa kwenye main plate.
  Tabia anayoionesha SHIBUDA ni dalili njema ya kumsoma nyendo zake. Huwezi kukihurumia chama ambacho kimehaini malengo na maadili ya taifa.
  Anakishauri kisife ili iweje???
  CCM siyo ya kuishauri sasa. iachwe ijifie mbele maana si riziki kwa taifa ikiendelea kuwepo
   
 6. Avanti

  Avanti JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2010
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 1,209
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Umemsoma eee?
  Ni kweli Shibuda damu yake ni ya CCM hapo kavaa ngozi ya CHDM, sitashangaa miaka ijayo akija kurudi nyumbani kwake.
   
 7. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Shibuda..namuona kama kaongeza idadi ya viti vya upinzani sitegemei kikubwa sana kutoka kwake kama mpinzani halisi..
   
 8. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kwa hakika mliliona, tukaliona ambalo wengi wetu hawataki kuliona, ubaya ni kwamba sote hatuwezi kuona, kwa maana wengine kwa makusudi mazima wanajilazimisha kutoona vinavyoonekana!!:tape:

  hapo ndipo ninaposhindwa kuelewa ama kuna kitu alisahau kule??? ama huku amejikinga tu kwa muda, anasubiri mayunyu yaishe arudi nyumbani kwake... atatuachaje tukishamzoea???:A S angry:
   
 9. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Avanti, siombi kuota ndoto ya aina hiyo hata kidogo, haitishi ila inaogopesha kwa maana ataondoka na kundi lake ah! sijui...:A S angry:
   
 10. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 474
  Trophy Points: 180
  Mawazo mfu na tatizo la kufanya analysis finyu.Shibuda anamaanisha kuwa majority shareholders ndani ya bunge ni CCM iwe isiwe lazima spika atatoka CCM.kWA MAANA NYINGINE LAZIMA CCM waangalie maslahi ya taifa.Pamoja na kwamba wengi wetu tunapinga chenge kuwa mteule wa uspika lakini akiteuliwa na CCM hakuna wa kuzuia.Habari ndo hiyo.Shibuda anawaasa CCM waangalie National interest than group interest.

  Kwa taarifa yako Shibuda hana chake CCM kutana nenda Maswa kaulizie yule ni mpinzani tangu akiwa CCM.usitutie hasira wana-Maswa tupe heshima yetu weeeeeeeeeeeeeeeeeee
  Usituleteee polojo tumefanya kazi ya ziada sana kumpitisha usitukumbushe machungu
   
 11. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  Msiofu waungwana, Shibuda amewawekea sisiemu mtego mkali sana, kumbukeni nguvu ya chadema itategemea sana na aina ya spika. Iwapo chenge atapitishwa ("wengi wape") basi upinzani utabanwa na hatutaona cheche za upinzani.
  Hata mimi naungana na Shibuda ktk hili
   
 12. doup

  doup JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  hapa naona mnawapa ccm mikakati tu
   
 13. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  hahaha
   
 14. P

  PapoKwaPapo JF-Expert Member

  #14
  Nov 10, 2010
  Joined: Jun 5, 2008
  Messages: 380
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Shubia mbona uanwakumbusha tena hao, waache wakafie mabali huko....
   
 15. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #15
  Nov 11, 2010
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  :smile-big: tuko hapa, naamini, hayatapita yale wala misimu ile pasina ukweli kujulikana:smile-big::smile-big:
   
Loading...