KISHINDO
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 2,202
- 1,957
Hatimaye uhamiaji wameshindwa kuvumilia kukaa na majina ya vijana, wayatoa majina hayo leo. Tafuta gazeti la Mwananchi la leo 26 May, 2014 ili ucheki jina lako. Kila la kheri wandugu mlioitwa.
Baada ya kimya kirefu hatimae uhamiaji wametoa majina kwa koplo na makonstebo kwa maelezo mazuri nunua gazeti la mwananchi
Hallow Watanzania wenzangu,
Naombeni msaada wenu kufahamu ukweli kuhusu walioitwa kwenye usaili wa idara ya uhamiaji kwa nafasi za konstebo na koplo wa uhamiaji. Sijui kama majina yale ni ya kweli.
Kwanza napenda tu nieleze wasiwasi wangu kuhusu yale majina, baada ya kuyaona kwenye blogs flani (ajira zetu), nilienda moja kwa moja kwenye website yao (Welcome to the Official Website of Immigration Services Department of Tanzania) kuangalia kama yatakuwepo pale sababu ndio sehemu husika lakini kwa kweli sikuyaona.
La pili majina yale yametolewa kwenye format ya pictures ambapo ni vigumu sana kutafuta jina lako, kila nikijaribu kutafuta kwenye format nyingine nimeshindwa kwa kweli so najiuliza wizara ilishindwa kutype majina mpaka wascan tu kama sio ubabaishaji tu?
Pia kitu kingine idara ya uhamiaji ilitoa nafasi nyingi sana, mkaguzi msaidizi wa uhamiaji (nafasi 70)) na koplo wa uhamiaji (nafasi 100) ila ukiangalia tatizo la ajira liliopo hapa Tanzania ni kubwa sana cha kushangaza majina yaliotolewa ni machache sana ukilinganisha na hizo nafasi zao.
Pia kwanini hawajaita watu kwenye interview yao? sisi tutajuaje kama wamewachagua watu bila kufuata utaratibu, kanuni na sheria za ajira,kwanini mambo yanaenda kimya kimya tu?
Kwa kweli tukiendelea hivi inatukatisha tamaa sana, Inauma sana, najua sio watu wote wanaoathirika na haya madudu sababu wengine wana watu wao huko serikalini. Ila mungu anajua tu, mtatawala hapa duniani lakini sio peponi, tutakutana siku ya mwisho.