Hatimae Marekani yasalimu amri katika vita ya kiuchumi na Venezuala

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,194
10,929
Kwa miaka mingi Marekani imekuwa ikiiwekea ajenda za kuikwamisha Venezuela hasa katika sekta ya mafuta.

Vikwazo hivyo viliitikisa sana Venezuela na kuirudisha nyuma kiasi kwamba watu walipanga foleni kwa siku kadhaa kupata lita moja ya petroli, taifa shujaa la Iran lilisimama na wavenezuela na kuwafikishia mafuta kwa njia zote kaitkati ya vikwazo hivyo vya Uchumi.

Ghafka bin vuu Marekani imelitaka shirika la mafuta la Chevron kwend Venezuela kuchima na kusafisha mafuta ya nchini humo.Nicholas Maduro aliyerithi kwa mwamba mwenzake Hugo Chavez wameibuka kidedea.

1669613948483.png
 
Marekani yeye anaangalia maslahi yake wala sio kitu kingine kama mafamba wanavyodai eti anajali haki sijui za binadamu sijui demokrasia, hapa kakubali kampuni ikachimbe sio kwamba kuna kilichobadilika venezuela ila kwa sasa anahitaji mafuta tu.
 
Venezuela hawezi kujali Russia atasemaje kwa sababu Russia wenyewe wachovu hawawezi kumsaidia chochote wakati na wenyewe njaa inawaua.
 
Hùyo maduro bila russia angekua ameshangolewa na mabeberu. Rassia ilipeleka askari 100 venezuela na ndege 2 aina su 35.hapo marekani shughuli ikaishia hapo.na sharti alilotowa maduro kwa marekani kabla ya mazungumzo amtambue maduro ndio rais wa venezuela
 
Hilo shart gumu sn Kwa USA maana inabidi Aachie mali zote za Venezuela alizoshikilia maana pesa yote ya Venezuela anampa mpinzani wa madulo kwakuwa ndio anamtambua.
 
Kwahiyo Maduro kamgeuka swahiba wake Puttin? Maana ameruhusu mafuta yake yachimbwe ili kuziba mwanya wa yale ya Russia.
Hapa sio kumgeuka Urusi.Amepima ni wapi kuna nafuu.Watu wasife njaa kwa faida ndogo ya kuisaidia Urusi kwa sababu Urusi ana mianya mingi ya kupandisha uchumi wake na kukwepa vikwazo kuliko anachoweza Kufanya Venezuela bila kuchimba mafuta.
 
Marekani yeye anaangalia maslahi yake wala sio kitu kingine kama mafamba wanavyodai eti anajali haki sijui za binadamu sijui demokrasia, hapa kakubali kampuni ikachimbe sio kwamba kuna kilichobadilika venezuela ila kwa sasa anahitaji mafuta tu.
Nocholaus Madro,Rais wa Venezuela amekubali kukaa meza moja na mpinzani wake Juan Guaido ili kuandaa Uchaguzi wa Kidemokrasia ambalo ndilo lilikuwa Sharti kubwa la Kulegezewa vikwazo.

Kwahiyo Maduro amekaza shingo mbele ya Marekani lakini mwisho wa siku amekubali kukaa meza moja na Guaido ambaye amehukumiwa kifungo Cha maisha kwa uhaini na Serikali ya Maduro.
 
Venezuela hawezi kujali Russia atasemaje kwa sababu Russia wenyewe wachovu hawawezi kumsaidia chochote wakati na wenyewe njaa inawaua.
Ungejua Venezuela ipo hapo ilipo sababu ya Urusi usingeongea utumbo huu
 
Back
Top Bottom