Hatimae fomu ya rufaa ya Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia CHADEMA, Bi. Amina Ally Saguti imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya

Hatimae fomu ya rufaa ya Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia CHADEMA, Bi. Amina Ally Saguti imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe, Ndugu Frolian Kimaro baada ya malumbano marefu, ambapo mamlaka zinazohusika zilikuwa zimekataa kuipokea.

Katika rufaa hiyo Mgombea Bi. Saguti anapinga, pamoja na masuala mengine, uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe Vijijini kumtangaza mgombea ubunge wa CCM kuwa amepita bila kupingwa, huku kukiwepo na ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi nchini.

Hadi mwisho wa kupokea rufaa hiyo ulipokuwa unakaribia jioni hii, kwa mara nyingine tena uteuzi wa mgombea huyo wa CHADEMA ulikuwa bado unawekewa vikwazo baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kukataa kupokea fomu hiyo tangu mchana.

Mgombea huyo akiambatana na Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, walifika ofisini kwa msimamizi leo mchana kuwasilisha fomu hizo lakini alikumbana na vikwazo hali iliyoonesha kuwa kuna dalili za kuhakikisha uamuzi wa juzi haubadiliki ili CCM ipite bila kupingwa katika jimbo hilo.

Fomu hiyo na. 12 ilipatikana jana kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya Uongozi wa CHADEMA ngazi ya taifa kulazimika kufanya mawasiliano ili kupata fomu hiyo kutokana na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe kukataa kutoa.

Chama tayari kimeshamwandikia rasmi Mkurugenzi wa NEC kumtaka achukue hatua za haraka kuingilia kati mwenendo wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe hasa kubatilisha uamuzi wake uliokiuka taratibu zinazosimamia uchaguzi kwa kukataa kupokea fomu za kugombea za Mgombea wa CHADEMA na vyama vingine huku akimtangaza Mgombea wa CCM kupita bila kupingwa kinyume cha sheria na kanuni za uchaguzi.

Tumaini Makene
Naluliza swali moja tu. Kwa nini Wagombea wa Upinzani kila Uchaguzi husubiri hadi siku ya mwisho kuwakilisha fomu zao?
 
Namshauri mgombea wa CCM pia akate rufaa ni kwa nini fomu ya mgombea wa CHADEMA inapokelewa nje ya saa ya uteuzi.
 
Hatimae fomu ya rufaa ya Mgombea Ubunge Jimbo la Korogwe Vijijini kupitia CHADEMA, Bi. Amina Ally Saguti imepokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Korogwe, Ndugu Frolian Kimaro baada ya malumbano marefu, ambapo mamlaka zinazohusika zilikuwa zimekataa kuipokea.

Katika rufaa hiyo Mgombea Bi. Saguti anapinga, pamoja na masuala mengine, uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe Vijijini kumtangaza mgombea ubunge wa CCM kuwa amepita bila kupingwa, huku kukiwepo na ukiukwaji mkubwa wa taratibu zinazosimamia uchaguzi nchini.

Hadi mwisho wa kupokea rufaa hiyo ulipokuwa unakaribia jioni hii, kwa mara nyingine tena uteuzi wa mgombea huyo wa CHADEMA ulikuwa bado unawekewa vikwazo baada ya Msimamizi wa Uchaguzi kukataa kupokea fomu hiyo tangu mchana.

Mgombea huyo akiambatana na Viongozi wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, walifika ofisini kwa msimamizi leo mchana kuwasilisha fomu hizo lakini alikumbana na vikwazo hali iliyoonesha kuwa kuna dalili za kuhakikisha uamuzi wa juzi haubadiliki ili CCM ipite bila kupingwa katika jimbo hilo.

Fomu hiyo na. 12 ilipatikana jana kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya Uongozi wa CHADEMA ngazi ya taifa kulazimika kufanya mawasiliano ili kupata fomu hiyo kutokana na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe kukataa kutoa.

Chama tayari kimeshamwandikia rasmi Mkurugenzi wa NEC kumtaka achukue hatua za haraka kuingilia kati mwenendo wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Korogwe hasa kubatilisha uamuzi wake uliokiuka taratibu zinazosimamia uchaguzi kwa kukataa kupokea fomu za kugombea za Mgombea wa CHADEMA na vyama vingine huku akimtangaza Mgombea wa CCM kupita bila kupingwa kinyume cha sheria na kanuni za uchaguzi.

Tumaini Makene
Jamani labda mi sielewi,kwani mkurugenzi wa NEC anateuliwa na nani! wapinzani mna kazi kweli ,watz tunawaonea sana huruma ila tunaogopa kufa maana hii serikali yetu kuua ni simple tu,haya maagizo aliyatoa mkuu kule singida kuwa atahakikisha a anaua upinzani sio kuudhoofisha hvy timu yake ndio hiyo,amaeshaondoa timu Jk yote na sasa timu yake ya ushindi na timu ua pinzani imekamilika na anatafuta sub tu wa kuwaongezea kutoka upinzani yaan wale ambao walikuwa vinara wa upinzani,akiwamaliza hao basi,ni ushindi kabla ya mechi,nyie mnachofanya ni kumshitaki tu kwa Mungu kuwa mlifuatilia na juhudi zenu zimeonekana,pia mnachofanya ni kumtafutia laana na mikosi kwenye serikali yake,maana wananchi wanavyosikitika kuna vitu wanasema hata kama havisikiki,hizi ni dua mbaya saaana,Hizi dua ndio zinasbabisha mkulu anafanya vitu viingi vya maana ila vinakuwa havionekeani kwa wanachi maana ni zao la ubadhlifu,hujuma na chuki,polenei sana wapinzani ila msife mioyo maana wengine ndio kazi zao na kwa sasa upinzani ni deal maana ukiingia kule ukionyesha kuwasumbua sana tayari umejitengenezea ajira CCM watakununua kwa dau lolote hivyo vijana changamkieni fursa
 
Aisee vijana wa baraza la vichaa la chadema huwa mnajua kujitoa ufahamu?? Hebu uje ujaribu kufanya hivyo ndivyo utajua maana ya serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo sio serikali ni Wahuni waliojivika nguo/vyeo vya sirikali,Mkurugenzi kazi yako kuwahudumia watia nia lakini unakimbia ofisi kisha unakurukupuka kusema muda umeisha na kumtangaza mtia nia wa sisiemu kapita bila kupingwa huo si uwendawazimu? Hivi mtu kama huyo unahesabu mtu mwenye akili timamu? Ngoja nizichange nitafute jimbo kisha mkurugenzi alete uhuni naondoka na kichwa chake kwa kuweka preceding.
 
Huwa mko vizuri kwenye social media, lakini vitendo big zero, hivi huyo mgombea wenu angekuwa na akili timamu angerudisha fomu nje ya muda?? Harafu anarudisha kwenye Ofisi ya mwenyekiti wa Halmashauri?? Seriously kweli pumbavu kabisa.Haya zichange halafu ulete huo uwendawazimu uone kama hautashughulikiwa.

Hakuna wa kunishughulikia wewe MBWIGA,Ukitaka kuruka lazima uagane na NYONGA,hauingii kindezi wewe BOYA.
 
Chadema ni chama dume,yaani CCM,pamoja na msaada wote wanaopewa na taasisi za serikali,polisi,mahakama,watumishi wa umma,bado wanakimbizwa kweli kweli na Chadema,sasa hari ikibadirika Chadema wakashika dola,CCM wanaweza kuhimili figisu figisu kama hizi anazopitia Chadema?,au kitakufa kama KANU,!!!
Hongereni sana wana Chadema,kwa uchache wenu,licha ya kupigwa risasi,kufungwa,kuuwawa,lakini mnawakimbiza jamaa vibaya sana,
Mkishika dola,Kwa figisu hizi mnazopata,mkiwapa CCM,watakufa,na kupotea kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makene hapo ni sawa na kuahirisha maumivu tu au ule usemi wa kuanua ngoma juani kama huyo msimamizi ndiye anategemewa kumtangaza mshindi unategemea atamtangaza huyo diwani wetu hata kama atashinda?

Sent using Jamii Forums mobile app
Suala la ushindi wa kiti cha udiwani na ubunge matokeo yanaweza kupingwa mahakamani endapo kutakuwa na ushahidi usio na shaka kwamba kuna udanganyifu ulifanyika katika mchakato wa uchaguzi likiwemo zoezi la kuhesabu kura au hata kasoro nyingine zinazoweza kuharibu zoezi zima la uchaguzi. Ni kweli pia msimamizi wa uchaguzi anaweza kutangaza matokeo ya uchaguzi kinyume na matokeo halisi ili kumbeba mgombea wa chama fulani. Mchakato wa uchaguzi hasa zoezi la kupiga na kuhesabu kura lipo wazi kabisa na kama aliyeshindwa kwenye uchaguzi atakuwa na ushahidi wa kutosha atakimbilia mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi. Na kwa ngazi ya ubunge na udiwani matokeo ni rahisi sana kujulikana endapo mawakala wa chama husika watakuwa waaminifu. Hivyo vyama vya siasa hasa upinzani viache kulalamika bali vijenge mifumo inayoeleweka ndani ya vyama vyao kwanza. PIA WAGOMBEA WAWE NA UTAMADUNI WA KUREJESHA FORM MAPEMA ILI KUEPUKA MATUKIO KAMA HAYA KUTOKEA MAANA HILI SI TUKIO LA KWANZA KWA VYAMA VYA UPINZANI YALISHATOKEA MATUKIO KAMA HAYA MENGI TU HUKO SIKU ZA NYUMA HIVYO NAO SASA WABADILIKE WASIAKE KULALAMIKA TU.
 
Huwa mko vizuri kwenye social media, lakini vitendo big zero, hivi huyo mgombea wenu angekuwa na akili timamu angerudisha fomu nje ya muda?? Harafu anarudisha kwenye Ofisi ya mwenyekiti wa Halmashauri?? Seriously kweli pumbavu kabisa.Haya zichange halafu ulete huo uwendawazimu uone kama hautashughulikiwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu inasaidia kubakiza maneno vinginevyo ulivyo hoji hapo juu vitakurudia.
 
Back
Top Bottom