Chenge huyu huyu mzee wa vijisenti? Sijui kama itawezekana.Tatizo la Katiba yetu iko 'silent' kuhusu mtu anayekutwa na hatia akiwa tayari kwenye uongozi (mid-way) kama ilivyo kwa Chenge. Lakini la msingi hapa ni kwamba Chenge amepatikana na hatia na amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu (ambayo ni zaidi ya miezi sita) na option ya fine. Anapolipa fine haimaanishi kwamba conviction inafutika. Huyu kisheria ni CONVICT na haruhusiwi kugombea ubunge. Lakini kwa sababu tayari ni mbunge, kwa maoni yangu na interpretation yangu ya sheria hii, moja kwa moja anapoteza sifa ya kuwa mbunge, na Spika anapaswa kulitangaza jimbo lake la uchaguzi kuwa vacant na ni lazima by-election ifanyike.
Chenge huyu huyu mzee wa vijisenti? Sijui kama itawezekana.
Nimeangalia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nimeona hivi kuhusiana na hali inayofanana na hii aliyo nayo Mh. Chenge.
Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
Chenge amekutwa na hatia na amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au faini 700,000Sh.
Sasa hatima ya Chenge inakuwaje baada ya hukumu hiyo?
Naomba wataalamu wa Sheria na katiba mtufafanulie vizuri.
Naona hiyo ya red inawasaidia wengi sana. Hata Chenge hiyo inamrudisha bungeni
sherehe za krismasi na mwaka mpya zimechukua muda wangu sana na kushindwa kuendelea na mjadala wangu kuhusu katiba.
Kulingana na katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania ya sasa hivi, chenge amepoteza sifa za kuwa mbunge kufuatana na ibara ya 71.(1)(a) inayosema kuwa
"mbunge atakoma kuwa mbunge na ataacha kiti chake katika bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo - (a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa
mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya katiba hii;"
hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi laki saba aliyopewa chenge inamuondolea sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge kwa mujibu wa katiba ya tanzania ibara ya 67(2)(c) inayosema "mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na mahakama yoyote katika jamhuri ya muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa
uaminifu; "
kwa hiyo, inabidi tume ya uchaguzi iitishe auchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na chenge. Hata hivyo kwa vile tume hiyo hiyo ya uchaguzi ndiyo iliyokiuka katiba ta tanzania ibara ya 41(6) na kumtangaza kikwete kuwa rais wa tanzania wakati hakupata kura nyingi zaidi ya wagombea wengine, basi inawezekana tume hiyo ikaja na maelezo ya kuhalalisha kwa nini chenge ataendelea kuwa mbunge.
naomba kuuliza hivi ismail aden rage si ameshawahi kuhukumiwa mbona mbunge sasa ! Nothing personal just giving a real example !
bado sijapata kipengele ambacho kinazungumzia kuhusu mbunge au kiongozi akipatikana na kosa wakati tayari ni kiongozi kwenye katiba yetu, kwa hiyo kivuli hiki kinaweza kumvunika Mzee wa vijisent na akaendelea mpaka muda wake wa miaka mitano uishe
Sherehe za krismasi na mwaka mpya zimechukua muda wangu sana na kushindwa kuendelea na mjadala wangu kuhusu katiba.
Kulingana na katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya sasa hivi, Chenge amepoteza sifa za kuwa mbunge kufuatana na ibara ya 71.(1)(a) inayosema kuwa
"Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo - (a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa
Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;"
Hukumu ya kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya shilingi laki saba aliyopewa Chenge inamuondolea sifa za kuchaguliwa kuwa mbunge kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ibara ya 67(2)(c) inayosema "Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa
uaminifu; "
Kwa hiyo, inabidi tume ya uchaguzi iitishe auchaguzi mdogo kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi na Chenge. Hata hivyo kwa vile tume hiyo hiyo ya uchaguzi ndiyo iliyokiuka katiba ta Tanzania ibara ya 41(6) na kumtangaza Kikwete kuwa Rais wa tanzania wakati hakupata kura nyingi zaidi ya wagombea wengine, basi inawezekana tume hiyo ikaja na maelezo ya kuhalalisha kwa nini Chenge ataendelea kuwa mbunge.
bado sijapata kipengele ambacho kinazungumzia kuhusu mbunge au kiongozi akipatikana na kosa wakati tayari ni kiongozi kwenye katiba yetu, kwa hiyo kivuli hiki kinaweza kumvunika Mzee wa vijisent na akaendelea mpaka muda wake wa miaka mitano uishe
kama jf kuna waelewa wengine kama 100 walio na ujuzi kama wako, mimi nakuwa na amani. Chenge amesimamishwa ubunge na Mahakama ya kinondoni kwa kumtia kolokolo kwa zaidi ya miezi 6,au faini sh.lak7,au vyote kwa pamoja. Hakimu kutotaja "vyote kwa pamoja" inamaana chenge hatoenda jela ila kifungu icho kinamhusu na ndo kilichomtia hatiani,labda na kifungu kile kivunje vipengele vpengele ili kwenda jela na kulipa faini vijitegemee. Pili katiba kwa ibara no.67 na 71 ya katika ya Tanzania,chenge si mbunge tena ila asubiri huruma ya Mafisadi ya kumlinda. Nakumbuka wakati anagombea ubunge rais Jakaya alisema ni mtuhumiwa mpaka Mahakama imtie hatiani,akaruhusiwa kugombea,sasa mahakama imemtia hatiani,KIKWETE atamke tena kuwa kwa kuwa maneno aliyotuhaidi yametimia. Ametiwa hatiani,ila ujanja ujanja wa sheria umeifunga nyara/ela lak7 ya jamhuri kiasi cha miaka3 badala ya chenge!
Hivi wachangiaji wengi humu wanakimbilia kutype kabla ya kusoma? Icho kifungu (c) ukisoma utaona kuna comma.
• Tafsiri Mbalimbali za kisheria( toka Mwanachi)
1. Dr. Mvungi
"...kwa mujibu wa sheria Chenge ataendelea kuwa mbunge kwa sababu hajatumikia kifungo na badala yake amelipa faini. ...Kama angeenda moja kwa moja kutumikia kifungo asingekuwa na sifa ya kuitwa mbunge na hata uchaguzi ujao asingeweza kugombea tena lakini, kwa sababu kalipa faini tu, hajapoteza ubunge wake."
Dr wa sheria naye hajui kuwa sheria haisemi kutumikia kifungo bali inasema kuhukumiwa kifungo. Mtu anaweza kuhukumiwa kifungo lakini rais akamsamehe aseinde jela kutumikia kifungo hicho bila kufuta hukumu.
2. Prof. Safari
"...kama zingekuwa zinatumika sheria za zamani, kwa hukumu hiyo, Chenge asingeweza kugombea tena ubunge. Unajua hata sheria mpya ya uchaguzi sijaipitiakuona inasemaje kuhusu suala hili lakini, ninachoweza kukumbuka ni kwamba sheria ya zamani ya makosa yote yaliyokuwa yakihusu ‘mortality' ulikuwa huwezi kugombea tena. Sasa sijui kwa sheria hii ya sasa,".
Profesa wa sheria hajui sheria inasemaje; afadhali yeye hakutoa tafsiri mbovu.
3. Wakili Harlod Sungusia
"...hukumu ya Chenge haina madhara yeyote kwake katika nafasi zake kisiasa. ...Hukumu ilikuwa sahihi wala hakimu hakukosea kuitoa. Kilichopo pale ni kwamba makosa aliyokutwa nayo Chenge si ya kukosa uaminifu hivyo, hayamfutia nafasi yake ya kuendelea kuwa Mbunge,".
Wakili naye anaangallia tafsiri ya uaminifu kwa dirisha dogo sana, anasahau kuwa kuongopa kwa aina yoyote ni kukosa uaminifu. Kutotekeleza wajibu wa kisheria na kujifanya kuwa umetekeleza wajibu huo ni kuongopa. Chenge hakutekeleza wajibu wa kulikatia bima gari lake lakini akaendelea liendesha barabarani kama vile amelikatia bima. Kitendo hicho ni kuidanganya serikali na hivyo kukosa uaminifu.
Hapana yule alitoka kwa msamaha wa rais, na pia nakumbuka wakati wanamuhoji kituo fulani cha redio yeye alisema, siku hiyo ya msamaha asubuhi aliitwa na bwana jela na kuambiwa umepata msamaha wa rais kwa hiyo leo utatoka.
Hakutoka kwa rufaa.