Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,255
Ziko tuhuma nyingi za ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya RC Makonda na malalamiko ya wananchi wabunge wa CCM hatimaye itabidi waunde tume ya Bunge kuyachunguza na kubaini mbichi na mbivu.
Wakithibitisha ni tuhuma za kweli, Bunge litapiga kura ya kukosa imani naye na kuishauri Serikali imfute kazi ushauri ambao lazima utaheshimiwa.
Hapo ndipo, tutaachana na harakati za mheshimiwa kufanya atakavyo.
Huu uchunguzi wa DNA bila amri za Mahakama unaweza kuharakisha kufutwa kwake kazi. Yeye machoni pake anaona anajijenga kisiasa kumbe anajimaliza bila kukusudia au kudhamiria.
Jiulize tu ni sheria zipi zinampa mamlaka ya kukusanya huo ushahidi dhidi ya watuhumiwa na ili kuthibitisha tuhuma itabidi awasake watuhumiwa na kuwalazimisha kuwatoa DNA zao kwa malinganisho na watoto husika.
Yote haya yanafanyika nje ya Mahakama bila ulinzi wa haki za watuhumiwa dhidi ya uchakachuaji wa DNA zao.
Bila amri za kimahakama na mazingira hakikiwa na wazi ni dhahiri haki za watuhumiwa kaziweka kibindoni huku hana mamlaka ya kisheria kuchunguza na kutoa maamuzi kwani ni mamlaka kisheria Mahakama tu imepewa.
Watendaji wanapoingilia uhuru wa Mahakama ni dhahiri haki za binadamu ambazo zinalindwa kisheria kujengewa mazingira ya kukiukwa.
Hata haki za watuhumu kutelekezwa kwa sababu bila ya kuwatendea haki watuhumiwa ni dhahiri watuhumu wataathirika vibaya mno pale watuhumiwa watapinga maamuzi ya kiutawala Mahakamani.