Hatima ya CHADEMA Bukoba iko Mikononi mwa Lwakatare na Conchester, Vinginevyo CCM Itapeta tu

Mnusaji

Member
Feb 16, 2012
67
20
Kumekuwa na mgogoro usiomalizika kati ya Wilfred Lwakatare ambaye ni M/Kiti wa CHADEMA mkoa na Mbunge wa viti Maalum Conchester Lwamlaza.

Kumekuwa na usuluhishi wa mara kwa mara lakini kauli ya nimesamehe huwa inatoka kinywani tu ila moyoni bado mgogoro unaendelea.

matokeo yake kwa sasa kila anayejitokeza kukipigania chama....inabidi ijulikane kama yuko upande wa Lwakatare au Lwamlaza. Kitu asichopenda kusikia Lwakatare na kambi yake ni kuwa kwa sasa hana mvuto wala ubavu wa kupambana na Kagasheki.

Ikisemwa hivo wanasema kama hana mvuto basi mwenye mvuto ajitokeze mpaka sasa hajajitokeza. Ilikuwa aje Gration Mukoba lakini kwa vile Lwakatare kasimika na kuna kambi mbili jamaa ameona kuwa atakuja kujiharibia bure.

Wadau wa ndani wanadai kuwa chanzo cha mgogoro ni kukiukwa kwa makubaliano kati ya Lwakatare na Lwamlaza. Ni kwamba Lwamlaza alipata nafasi ya Ubunge kwa sababu ya kura alizokuwa kapigiwa Lwakatare, lakini fadhila hasa katika kutumia kukijenga chama ikawa ni Hamna.

Hivo kila anayetaka kujitokeza kujenga chama swali linakuja uko upande gani? Hali hii imesababisha mgawanyiko mkubwa utakaoinufaisha CCM. Na inaonekana makao makuu wameshindwa hii kitu.
 
Hii kitu ni shida. Mkiti wa Manispaa yuko kwa Lwakatare ambapo mipango inaanzia. Kusema ukweli tatizo hili lisipo tatuliwa CDM watakuwa wanatimiza wajibu kushiriki uchaguzi.
 
CHADEMA tafuta mgombea mpya kabisa, hawa wote hawana jipya mbele ya wananchi wa Bukoba. Kiujumla jimbo halina mgombea na mkizembea CCM wanabeba tena kwa sababu Bukoba hatuchagui chama ila Tunachagua mtu
 
  • Thanks
Reactions: R.B
Hii kitu ni shida. Mkiti wa Manispaa yuko kwa Lwakatare ambapo mipango inaanzia. Kusema ukweli tatizo hili lisipo tatuliwa CDM watakuwa wanatimiza wajibu kushiriki uchaguzi.
Nadhani chama wangepeleka watu huko watafiti kiini haswa vinginevyo hao wawili watoswe wote maana watagawa wapiga kura
 
Chini ya uongozi wa serikali ya ccm kila utakalo utalipata, bkb fursa kibao ila hamuishi kulalama, kwani siku unapotoa ahadi ya meli ndo siku hiyo inaanza kujengwa? Meli si kachumbali wala mayai ya kukaanga. Inachukuwa muda kutokana na nature ya kazi yenyewe. Mbona usemi barabara ya Kagoma - Rusahunga, Kyaka - Bugene, Uwanja wa ndege Bkb, Maji Kibeta?

Macho yako umeyaelekeza kuona udhaifu kidogo ila mambo mazuri huyasemi tabia hii alikuwa nayo LUSIFA kule mbinguni kwa kuona kila MUNGU alichofanya kwamba hakifai. Serikali hutekeleza mambo yake kwa mpango si kwa kukurupuka.

We hujitambui. Hivi unaweza kujisifu kumnunulia mwanao nguo ili asitembee uchi wakati umemzaa mwenyewe. Hivo unasema vimefanyika kuna aliyetoa mfukoni mwake au ni kodi zetu. Tunachochangia , raslimali tulizonazo na unachojisifia kwa chama chako nakushangaa.

Akili ya mtu pekee na busara za kiongozi ndo zinahusu hapa huo ujinga mwingine kaongee ukiwa kwenye vikao vya chama chako ambapo huwa mnajitoa akili na kuona hakuna shida.

Miaka 19 hata ingesemwa kuwa kila samaki anayevuliwa ziwa victoriamachangie shilingi 30/= meli ingesha kuja. Assume kwa mwaka wanavuliwa samaki milioni 3 kisha zidisha mara tsh 30 kisha mara miaka 15 walau. Kisha nenda internet uangalie bei ya meli mpya denmark. Umeshafanywa vibaya ndugu.
 
Dawa sahihi ya kumaliza tatizo hili na kwa faida ya chama wote wawili wawekwe pembeni
 
hivi kuna mtu hapo bukoba aliyetumikia cdm kwa kiwango kilichotukuka kumzidi kamanda lwakatare ? hivi huu mvuto mnaoutaja hapa ni wa sura au maendeleo ?
 
We hujitambui. Hivi unaweza kujisifu kumnunulia mwanao nguo ili asitembee uchi wakati umemzaa mwenyewe. Hivo unasema vimefanyika kuna aliyetoa mfukoni mwake au ni kodi zetu. Tunachochangia , raslimali tulizonazo na unachojisifia kwa chama chako nakushangaa.

Akili ya mtu pekee na busara za kiongozi ndo zinahusu hapa huo ujinga mwingine kaongee ukiwa kwenye vikao vya chama chako ambapo huwa mnajitoa akili na kuona hakuna shida.

Miaka 19 hata ingesemwa kuwa kila samaki anayevuliwa ziwa victoriamachangie shilingi 30/= meli ingesha kuja. Assume kwa mwaka wanavuliwa samaki milioni 3 kisha zidisha mara tsh 30 kisha mara miaka 15 walau. Kisha nenda internet uangalie bei ya meli mpya denmark. Umeshafanywa vibaya ndugu.
Wakola Ta Muganyizi. Unajua kuna watu wanashabikia vitu hata pasipo kujiuliza. Mfano kama mtu alitoa ahadi ya meli je, aliahidi itatengenezwa muda gani? Kama aliahidi itatengenezwa miaka 20 ijayo tusimlaumu. Lakini kama aliahidi itatengenezwa kipindi cha uongozi wake halafu ndo tunaona anafikia mwisho bila kutwambia hatua ambayo imeshachukuliwa, basi huyo hafai hata kwenye familia yake.
 
CDM watatakiwa kulaumiwa kwa kushindwa kujipanga alafu inakuwaje jambo dogo kama hili linakishinda chama? kwanini wote wasiondolewe na mchakato ukatafuta watu wapya kabisa make kama leo haya yanawashinda basi haikuwa na sababu ya kuwazomea CCM kwamba walishindwa kuumaliza mgogoro wa meya na mbunge wake, hatupaswi kuwacheka CCM kupelekeshwa na kundi la Membe na Lowassa.
Alafu haya mambo ya kuachiana hivi ni kanuni za chama ama ndo siasa mpya iliyoibuka, kwanini chama kinaacha eti watu wakubaliane kwa masrahi ya chama na wakati kanuni za chama zipo? hii ni hatari sana kwasababu ndo tunaona leo watu wanaitana wanamitandao na kambi huku CCM na yanakipasua chama sasa, CDM bado ni changa, haya mambo ya mitandao waachane nayo kwanza vinginevyo majuto ni mjukuu na chama kitapotea sashivi
 
Baada ya kichapo ndo watajipanga.....yaani watu wanajitoa akili na kujifanya hawaoni kinachoendelea
 
Lwakatare wee baki na USALAMA WA CHAMA. Hadi leo ni wewe umeshaonja joto ya kurekodiwa LIVE na hivyo ninafahamu utakuwa umeshajiandaa vyema ili lisirudie tena hili swala.
Pia chama kilikupigania hadi kesi yako ikaisha na sasa umerudi kuwa Mkuu wa Kitengo cha USALAMA.

Hiki ni kitengo muhimu sana kuzidi hata ubunge unaoweza kuupata. Usalama wa viongozi wa Chadema utategemea sana wewe umejipanga vipi. Pia waksihakuwa na uhakika wako salama, watawanyuka vyema CCM wakijua utawalinda.

Nina imani BUSARA zitatawala na mwakani CCM kitakuwa chama cha KAWAIDA tu hapa Tanzania. Ntapigana sana kisife kwani CHADEMA au UKAWA wakitawala, baada ya muda wakikosa UPINZANI, watakuwa kama CCM vilevile....
 
hivi kuna mtu hapo bukoba aliyetumikia cdm kwa kiwango kilichotukuka kumzidi kamanda lwakatare ? hivi huu mvuto mnaoutaja hapa ni wa sura au maendeleo ?

Lwakatare alishapoteza mvuto alioewa miaka 5 akashindwa..tunahitaji sura mpya kwenye kinyang'anyiro hiki.
 
Back
Top Bottom