Hati ya mashitaka ya Mhe. Lema baada ya mengine kutupiliwa.

Hati ya mashitaka ya Mhe. Lema baada ya mengine kutupiliwa.

Ni ujinga mwingine. "kama kwenda kwenye send-off" ni lugha iliyotumika kuonyesha kuwa mkuu wa mkoa hakulipa uzito unaostahili tukio la kifo na hivyo alikwenda kwa kuchelewa. Ni kweli alichelewa mno. Isitoshe alipofika hakuonyesha majonzi yeyote zaidi ya kuleta nyodo za kitoto za kutotaka kuongea na wafiwa mpaka apewe mic wakati Lema muda wote aliweza kuongea na wanafunzi walimsikiliza bila ya mic. Amedhihirisha kwa matendo yake kuwa pale palikuwa na send-off maana ni kiongozi mjinga anayedai mic kwenye msiba usiotarajiwa! Send-off inaandaliwa na mic zinakuwepo. Baada ya kupewa mic Uso wa mkuu wa mkoa ulionyesha dharau na kebehi hata kabla ya kuongea. Hayo ni baadhi ya mambo yaliyoanza kuwakera wanafunzi. Wakajikuta wanamzomea.
Halafu wanasema ni shitaka la jamhuri dhidi ya Lema? Jamhuri gani hiyo yenye kushitaki watu kwa makosa mepesi kiasi hicho? Kwa kweli ifikie wakati tuanze kuona aibu kwa mambo haya. Yaani kumwambia mtu umekuja kama unaenda kwenye 'send-off' ni uchochezi?
 
Hawa watu hawana kazi ya kufanya,sa hapo kamtusi au kamsifia hajui mwendo wa sendoff ni wa taratib ka kinyonga,hili zee shamba kwelikweli
 
Tumeidhihirishia dunia kuwa viongozi wa serikali ya Tanzania ni maskini wa akili. Hii ni kesi inayofunguliwa na Jamhuri kwa raia wake?!?! Kweli tuna DPPP? Kweli tuna askari? kweli tuna mkuu wa mkoa?! Tupoteze kodi zetu kusimamia kesi ya kijinga namna hii? Hii kweli ni nchi aliyoiasisi Mwl. Nyerere??? Naam, nchi ipo kwenye pango la wanyang'anyi.
 
You must be joking... hivi haya nayo alishitakiwa nayo?
Sitanii ndiyo ukweli wenyewe, ndiyo maana leo watu wa Arusha walikuwa tayari kwa lolote maana serikali wanafanya uhuni wa hali ya juu, huwezi amini makosa ndiyo hayo mpaka polisi wakaenda kuruka ukuta na mbwa zaidi ya 20, magari ya polisi 5, pikipiki....
 
Huyo STATE ATTORNEY aliyekubali kuandika Hati ya Mashtaka ya kipuuzi kiasi iki anadhalilisha proffessional yetu na namuheshimu sana kaka angu HARUNI MATAGANE tokea tukiwa UDSM hivi jamani mmeshindwa kabisa kufanya mambo kwa uweledi na kuwakatalia hawa watawala kama MULONGO kufanya maamuzi ya kipuuzi na kibabe.
 
Kama haya maneno ni kosa la jinai basi ina maana Mwigulu, Lusinde au hata Nape wangekuwa jela miaka mingi sana !!

Hiyo ni hati ya mashtaka au ni maneno ya kijembe vijiweni? Kweli kanda ya Arusha DPP mmeandaa haya mashtaka au ni kuchekesha watanzania wakubwa zangu? Why wasting taxpayers money? Nimeshangaa sana. Yaani kesi ya ajabu sana hii. Mbona maneno ya kawaida hayo? Yale maneno aliyosema mkuu wa mkoa ndiyo yaliyoamsha hasira za wanafunzi na si ya Lema.
 
Watu wanachezea muda wa mahakama bure kabisa, kuna kesi za msingi nyingi sana ambazo watu wamekwama mahabusu na wengine wanasotea haki mitaani.

Huwezi kumshtaki mwanasiasa kwa kauli kama hiyo na ukategemea conviction ya mahakama. Viongozi waiache mahakama itumie muda wake vizuri kutoa haki kwa wananchi na wanasiasa wakamalizane kwenye forums zao.
 
Kwa hiyo kuvamiwa nyumbani kwake usiku wa manane na zaidi wa maaskari 25 ambao walipanda ukuta na kuingia ndani wakiwa na mabomu ya machozi na silaha nzito.. ilikuwa kwa ajili ya kosa hili ambalo lipo kwenye sheet hii..? WABHEJASANA umeona hii lakini..? Maana wewe ulifungua uzi wa kumsema Lema ati anatafuta umaarufu wa kisiasa.. Hapo kweli Lema ndo anaetafuta au mnamlazimishia wenyewe..????
 
mbona hayo maneno ya uchochezi ya Lema hawajayatafasiri kwa kimombo???

Is DPP ki-english not rechabo??
 
Hivi huyo Mkuu wa Mkoa bado tu hajafukuzwa kazi? Ni ajabu sana kama tunaweza kuwa na viongozi wajinga kiasi hiki.
 
DSC04928.JPG
DSC04951.JPG
DSC04994.JPG
DSC04918.JPG
DSC04965.JPG
Watu wa Arusha leo walikuwa walichafukwa Roho
 
Kama haya maneno ni kosa la jinai basi ina maana Mwigulu, Lusinde au hata Nape wangekuwa jela miaka mingi sana !!

Hawa wako ndani ya CCM hivyo wanahaki ya kutukana matusi yoyote hata ya nguoni,kama alivyofanya Peter Serukamba na Naibu Spika akaona safiii,Kazi kwa wabunge waupinzania hata ukisema UNAOMBA MWONGOZO lazima utolewe nje, kisa unataka sana kuongea na kuleta fujo Bungeni,hivyo kaka usishangae.
 
Back
Top Bottom