LACK
Senior Member
- Aug 1, 2013
- 129
- 43
Nyani ni mtaalam sana wa kujua ugumu na uimara wa miti mbali mbali katika msitu. Tangu anazariwa mpaka anapo ondoka kwenye uso wa dunia, maisha yake hutegemea kuwepo kwa miti. Uhusiano wa nyani na miti unatofautiana kidogo sana na uhusiano wa samaki na maji. Nyani kama ilivyo samaki kwenye maji huwezi kuwa kuta wakiendesha familia zao na kuongezeka katika mahali pasipo na miti.
Binadam ni kiumbe wa ajabu ambaye mambo makubwa yanayomtofautisha na wanyama ni uwezo wake wa kuwaza, na kuchakata mawazo yake na hatimaye kuamua limpasalo kufanya. Binadamu hakuweza kugundua matunda yafaayo kwa chakula kama asingeuliza hekima kutoka kwa nyani. Si hivyo tu binadamu asingejua kuogelea kama si kuchota hekima ya samaki katika kufanya jambo hilo. Maskini binadamu asingeweza kutengeneza ndege kama asinge angalia kwa kunguru ambaye mara nyingi huligeuza anga kawa njia yake kuu.
Binadamu asingeweza kujenga nyumba ya kuishi kama si kuwepo kwa baridi na wanyama wengine waliochanganyikiwa. Je vifaru wanyama wasinge kuwepo, hawa vifaru wengine wanao tumika kuua binadamu wangeitwa jina gani? Nani ajuae kama kusingekuwepo mvua kama tungeweka paa za nyumba zetu? Kitugani ama ni kiumbe gani ambaye hafai kuwepo kwa sababu ya kuto kuwa na faida? Itoshe kusema Mungu ni baba wa sana zote!!
Mungu aliviumba vitu vyote ili vitegemeane na kwa asili hakuna kitu au kiumbe ambacho hakitegemei kuwepo kwa kiumbe chenzie duniani. Tunayosababu kubwa ya kuheshimiana na kila mmoja wetu kumhesabu mwenzie kwamba anafaa kuliko yeye maana uwepo wake unategemea sana kuwepo kwa huyo mwingine ambaye kwa namna moja ama nyingine anaweza kuonekana hafai!
Si ajabu kusikia watu wakitoleana macho kwamba sisi ni wamaana kuliko wengine na hawa wengine wakisema sisi ni zaidi. Mtu anaye dhani anafaa kuishi peke yake duniani ana mapungufu katika fikara zake!
Tumeishi kama wanadamu ambao kwa mujibu wa biblia tunatokana na mwanadamu wa kwanza na mmoja ambaye ni Adamu. Lakini tumeamua kurithi dhambi ya Kaini kwa kuona kwamba watu wengine hawawezi kubarikiwa ila sisi.
Wenzetu wa Burundi kwa kujua amakutokujua mmeamua kukalia kuti kavu kwa kuamini na kuweka misingi yenu katika matengano na vulugu! Mmeacha makazi yenu na nyuba zenu kwa amani na kuhamia msituni. Mmeharibu hatima ya watoto wenu kwa kuwakosesha elimu na amani ambayo ni sababu kuu ambayo ingesababisha maisha yao kuwa mazuri.
Najiuliza maswali mengi sana juu ya hili. Je mpaka lini mtapata amani kwa njia mnazozitumia kutafuta amani? Hivi ukimfukuzia adui yako ama ndugu yako polini kwa kutokutaka mgawane kile kidogo kilichopo utalala ndani ya nyumba yako kuche?? Siamini!! Usiku mzima utakuwa macho ukiwaza “inawezekana akarudi kuniunguzia ndani ya nyumba hii!” nawe pia utaamua kulala nje! Je hayo ndiyo maisha mliyoyachagua ya kuacha nyumba zenu ili muwe mnalala nje?
Mnafanya kazi ya kurithishana chuki kutoka kizazi kimoja hata kingine, je mwisho wake utakuwa nini? Piganeni lakini mkumbuke hata kama mngeuana wote mlioko katika nchi hiyo bado tatizo halitaisha kwa maana kuna ndugu zenu walioko nje ambao nao ama kwa kutokujua wamegawanyika vivyohivyo katika makundi.
Mumeyafanya maisha yenu kuwa magumu na gharama yake imekuwa kubwa kuliko hata mngekubari kuongozwa tu kwa miaka hii mitano hatakama halikuwa chaguo lenu! Na hasara imekuwa kubwa kwa kiongozi kuongoza miaka mingine 5 ambayo kama siyo Mungu kuingilia kati itakuwa ni miaka ya kuharibu kazi yako njema uliyoifanya kwa miaka yote uliyoongoza huko nyuma. Nani ajuaye kama kuachia ngazi kwa amani kusingekupa heshima kubwa kuliko uliyonayo sasa? Mwangalie Goodluck Nigeria namna anavyoheshimika duniani wakati aliiongoza nchi yake kwa mhura mmoja tu!!!!
Warundi sasa hawawezi kujenga nyumba zao maana mmeijaza mioyo yao hofu na kuyafanya maisha yao kuwa yasiyo na matumaini! Vijana nao kwa kutumiwa wamejazwa chuki na mioyo yao imejaa visasi maana wengine waliondokewa na wapendwa wao tena kwa vifo vya kusikitisha!! Mmelifanya jina la nchi yenu kuwa kama tusi maana warundi wenyewe hawapendi kutambuliwa kwa taifa lao! Ni maombi yangu kwamba Mungu awakumbuke na kuwakumbusha kwamba katika chuki na visasi hapatatokea amani yenu ya kweli.
Jifunzeni kwa Tanzania, wapo wengi ambao hawakuridhishwa na uchaguzi na matokeo yake lakini wamekubari kuendelea kuwa watulivu hata katika mazingira hayo.
Jifunzeni hata kwa wanyama basi!! Nyani pamoja na kwamba si binadamu hawezi kukaria kuti kavu maana anajua kitakachotokea!