- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Kumekuwa na machapisho, video na mijadala mtandaoni inayodai kuwa Rais William Ruto aliwaagiza Warundi waondoke Kenya, huku baadhi ya madai hayo yakihusisha kauli yake na visa vya vitisho, unyanyasaji na kufungwa kwa biashara zinazomilikiwa na raia wa Burundi.
Madai hayo yaliongezeka baada ya mamia ya Warundi kufika katika Ubalozi wa Burundi jijini Nairobi kutafuta hati za kusafiria, huku baadhi yao wakisema wanataka kurejea nyumbani kwa sababu hawajisikii salama tena Kenya.
Lakini je, Rais Ruto kweli aliwaambia Warundi waondoke nchini?
Madai hayo yaliongezeka baada ya mamia ya Warundi kufika katika Ubalozi wa Burundi jijini Nairobi kutafuta hati za kusafiria, huku baadhi yao wakisema wanataka kurejea nyumbani kwa sababu hawajisikii salama tena Kenya.
Lakini je, Rais Ruto kweli aliwaambia Warundi waondoke nchini?
- Tunachokijua
- Mnamo Septemba 2, 2026, Rais William Ruto alizungumza kuhusu wafanyabiashara wadogo wa kigeni nchini Kenya, hasa wale wanaojihusisha na uhawking, retail na biashara nyingine ndogo ndogo.
Katika kauli zake zilizothibitishwa, Ruto hakuwataja Warundi moja kwa moja.
Badala yake, alizungumza kwa ujumla kuhusu wafanyabiashara wa kigeni, akisema baadhi ya biashara ndogo ndogo zinapaswa kulindwa kwa ajili ya Wakenya.
Ruto alisema kuna sheria inayolenga kuzuia wageni kujihusisha na baadhi ya aina za biashara ndogo, na akatoa mfano wa mtu kuja kutoka China na kuanza kufanya biashara ya uhawking.
Pia alisema: “Hawa wachuuzi ambao wanafanya biashara ndogo ndogo wafunge…”
Ruto aliongeza kuwa Kenya imejenga mazingira ya kuwavutia wawekezaji, si wageni wanaokuja kufanya biashara za uhawking na retail ndogo ndogo.
Kwa hiyo, ingawa kauli yake ililenga wazi baadhi ya wageni wanaofanya biashara ndogo, hakuna ushahidi katika hotuba hiyo unaoonyesha kuwa alisema moja kwa moja kwamba Warundi waondoke Kenya.
Hata hivyo, athari zilizofuata zilikuwa kubwa. Mamia ya Warundi walifika katika ubalozi wao Nairobi kutafuta hati za kusafiria ili kurejea nyumbani, huku baadhi yao wakisema wamepokea vitisho na wanaogopa kushambuliwa au kunyanyaswa.
Ripoti nyingine pia zimeonyesha kuwa baadhi ya wafanyabiashara wa kigeni walifunga biashara zao, huku wengine wakihofia usalama wao na chanzo chao cha mapato.
Katika eneo la Mowlem, Eastlands, kwa mfano, angalau biashara 20 zinazomilikiwa na wageni ziliripotiwa kufungwa, huku baadhi ya wamiliki wakiondoka eneo hilo kwa hofu ya usalama wao.
Hii ilimaanisha kuwa kwa baadhi ya familia, mjadala haukuwa tena kuhusu siasa pekee, bali kuhusu kupoteza riziki ya kila siku, kodi, chakula na uwezo wa kuhudumia familia zao.