Nimeiangalia video mpya ya Diamond. Kusema kweli pamoja na kashfa mbalimbali zinazomuandama huyu kijana,kwenye game anakaza. Ni video fupi lakini yenye quality na message. Ingawa umri wake si mkubwa lakini nashauri wasanii wengi hata wakubwa wajaribu kupata ushauri toka kwake ni jinsi gani anafanikiwa kisanaa na kimaisha. Si mpenzi sana wa bongoflavour lakini pale msanii akitoa kitu kizuri huwa nashindwa jizuia kumsifia na kumtia moyo.