Hatari Same; Makundi ya tembo yanatishia uhai, Waziri Ndumbaro chukua hatua

Asante kwa taarifa.
Inatia moyo sana kama wewe ni mhusika kwenye swala hili. Tembo wanaua watu na wanamaliza mazao ya watu hata bila fidia. Hivi prioriy katika hili jambo ni nini, nani ana prioity ya kuishi kati ya tembo na binadamu? Siku mimi nikiwa na mamlaka, binadamu mmoja anauawa na tembo, tembo wote hawatakuwepo tena eneo hilo milele, nitajua nini cha kufanya, sitaki kukisema kwa sasa
Ni binadamu kwanza, tembo baadaye. Kama binadamu na tembo hawawezi ku-co-exist, basi tembo ndiyo anatakkiwa asiwepo. Hatuwezi kuwa tunauza uhai wa binadamu, kisa fedha za utalii unaotokana na uwepo wa tembo. Hii maana yake tunauza uhai wa binadamu kwa fedha zinazotokana na utalii wa tembo, ambacho ni kitu kibaya sana. Hivi imeshindikana kabisa hata kuweka namna ya fencing ili kukomesha kabisa tembo wasivamie makazi ya watu ikiwa ni pamoja na mashamba yao?
 
Hii ni habari njema kwetu sisi watunza mazingira pamoja na uhifadhi wa wanyama pori!!!

Maana yake UJANGIRI UMETOWEKA hivyo kusababisha wanyama kuzaliana kwa wingi na kuongezeka

NB: KINANA SHIKAMOO
 
Mkuu Same kuna mapito ya wanyama toka wapi?
Taveta?
Mkomazi?
Kuelekea wapi?
Umewahi kuona simba, twiga, swala au tembo Same, Mwanga au Hedaru?
ukiongea na wazee wa kipare sababu yawao kukaa milimini ni pamoja na tembo, zamani kulikua na tembo wengi sana ikapelekea wao kwenda milimani
 
Hii ni habari njema kwetu sisi watunza mazingira pamoja na uhifadhi wa wanyama pori!!!

Maana yake UJANGIRI UMETOWEKA hivyo kusababisha wanyama kuzaliana kwa wingi na kuongezeka

NB: KINANA SHIKAMOO
Kinana atarudi kwenye system tena afanye yake
 
Habari wana JF wenzangu,

Ni miaka mingi nimekuwa mtumiaji wa barabara ya kuelekea Mikoa ya kaskazini mwa nchi yetu yaani Kilimanjaro na Arusha bila kuona wanyama wowote wakali kama simba au tembo.

Lakini jambo la kushangaza, hivi karibuni yameibuka makundi makubwa sana ya Tembo wengi sana wakiwa wamezunguka makazi ya watu kilomita sio chache kama 3 hadi 5 kutoka Same Mjini.

Hili ni jambo la hatari sana kwa wakazi wa Same na watumia barabara hii ya kazini hasa nyakati za usiku kwani madereva wengi hawajazoea hivyo huwa wanatembea kwa spidi bila tahadhari.

Kwa hatari hii nashauri waziri wa maliasili na utali achukue tahadhari ili kulinda maisha ya wakazi wa Same na watumia barabara hii ya kaskazini mwa nchi.

Wanatokea hifadhi ya mkomazi Grannie's zangu wamepakana na mpk wa hifadhi hiyo mida yeyote tu jiandae kukimbia maana wakitoka huko wakikukanyaga habari yako inaishia hapo.
 
Wanatokea hifadhi ya mkomazi Grannie's zangu wamepakana na mpk wa hifadhi hiyo mida yeyote tu jiandae kukimbia maana wakitoka huko wakikukanyaga habari yako inaishia hapo.
Uko sahihi.
Hivi karibuni nilikuwa Same niliuliza swali hili nikajibiwa kuwa wanatokea Mkomazi hasa nyakati za ukame
 
Wanatokea hifadhi ya mkomazi Grannie's zangu wamepakana na mpk wa hifadhi hiyo mida yeyote tu jiandae kukimbia maana wakitoka huko wakikukanyaga habari yako inaishia hapo.
Wanunue drones. Drones ni kiboko ya tembo, ndege na wanyama wote waharibifu.
Maana wakiona drones ukimbia balaa
 
Unaweza pia tumia drones kupambana na wafugaji waharibifu wanaoonea wakulima. Tumia zile agriculture drones funga spray za maji yawashayo
 
Back
Top Bottom