Hatari gani aliyonayo Harmonize mpaka alindwe hivi?

Mabouncer njaa kali wa elfu 10,10 hivi,tekno,whizzy na Davido,P square wana hela chafu hawana mlinzi hata mmoja popote pale
 
Acheni alindwe hao walinzi wana familia aseee unoko unoko sio mzuri,wakipunguzwa then harmo akawa anatembea peke ake hao majamaa wakaja mtaani kutukaba mtaanza mlalamikia nani?

Hivi hizo mbavu zikikosa kazi then zikawa zinakuvizia wewe umetoka kazini wakutie kabali hv utaacha toa kila kitu kweli? hadi ambavyo hujaambiwa unaweza ukatoa.

N sawa na wale wanaochongea wenzao wenye vyeti feki..hivi unamchongea mtu anacheti feki akifukuzwa kazi wewe unafaidika nini? basi bora afukuzwe kazi then nafasi yake apewe baba ako au ndugu yako ila nafasi anapewa mwingineeeee kbsaaaaa hata humjui halafu unachekelea.

Mnapata faida gani kuwa na vihere here na maisha na kula za watu wengine aseee,ifike tu mahali muwe mnaongelea ,mambo ya familia zenu na kuacha maisha ya watu maana huo ndio Uchawi,sema mmekosa vifaaa tu vya kupaaa angani.
#umetixha mkuu
 
Yaani mtu katafuta pesa kwa jasho lake alafu wakati anatumia unamuita mshamba,.Aaah mkuu mwache kijana atumie.
mpaka natoa jibu hilo nimetazama mbali sana mkuu nimeshindwa tu kumwambia mjinga ambalo kiukweli ndivyo anavyostahili kuambiwa na mjinga sio tusi ila ni mtu ambaye hajaelimishwa vizuri.
hivyo kijana bado hana elimu ya kutosha juu ya fedha na ndio maana anajikuta anamatumizi yasiyostahili hivyo kupoza makali ya maneno bora tumwite mshamba kwa kuwa hajui thamani ya hiyo hela kwa miaka kumi ijayo itakuwaje? na hajachukua taadhari za kutosha iwapo soko la muziki likianguka atakuwa na fedha kiasi gani cha kuhimili kulipa short term liabilities so vyote hivi tunaangalia.
fedha ni sawa na ugonjwa, kichwa kikiuma utakunywa maji,kikizidi utakwenda duka la dawa kikiendelea utamwona daktari. ndivyo na fedha zilivyo zinahitaji wataalamu waweze kuzichunga na kukuelekeza yasije yakatokea kama ya yule aliyekuwa na hoteli ya Makondeko iliyojengwa kwa gharama kubwa lakini haikuweza kuleta return iliyotarajiwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom