Hataki kuelewa

The Hidden

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
246
102
Habari wanaJF!? Natumai mko poa.

Inatokea mnaweka pamoja mipango kadhaa ya maendeleo na binti unayetarajia kumuoa, ili kutimiza mipango hiyo unatoa robo tatu ya mtaji nayeye anatoa robo tu, mnakubaliana pesa ya matumizi itatokana na hii biashara na hiyo ya mshahara(ambao ni sawa)kila mmoja atachukua kiasi kadhaa tu nyingine yote itunzwe hadi wakati fulani tutakapo itumia kufanya shughuli fulani ...anakubali, tatizo unakuja kugundua kuwa si mtunzaji mzuri wa fedha unaamua kumwambia "pesa ya mshahara inayotakiwa kutunzwa amishiaga kwangu kwa sababu hizo" linakuja tatizo kwamba hataki kufanya hivyo, hapa tatizo liko wapi wadau au kuna makosa kumwambia hivyo mpenzi wako!?
 
Umtunzie pesa we Benji,acha atunze pesa take mwenyewe kwani we mumewe?jibu ni LA hasha,unataka hakuamin kwa kipato chake?haipo hyo
 
Asa benji ndo inatunza pesa mzee, afu hii yote ni kama hamuaminiani "UPENDO KUVUMILIANA UPENDO KUAMINIANA " Hayo ni maneno ya bible mzee
 
Na yeye anataka nimfungulie salon ambayo ni zaidi ya milion na nimekubali, sasa kama yeye haniamini mi nimekuwa mjinga kukubali ombi lake?
 
Mchumba unamfungulia biashara,? Muda si mrefu utaanza kuongea peke yako. Hao watu usiwaamini ndugu.
 
Habari wanaJF!? Natumai mko poa.

Inatokea mnaweka pamoja mipango kadhaa ya maendeleo na binti unayetarajia kumuoa, ili kutimiza mipango hiyo unatoa robo tatu ya mtaji nayeye anatoa robo tu, mnakubaliana pesa ya matumizi itatokana na hii biashara na hiyo ya mshahara(ambao ni sawa)kila mmoja atachukua kiasi kadhaa tu nyingine yote itunzwe hadi wakati fulani tutakapo itumia kufanya shughuli fulani ...anakubali, tatizo unakuja kugundua kuwa si mtunzaji mzuri wa fedha unaamua kumwambia "pesa ya mshahara inayotakiwa kutunzwa amishiaga kwangu kwa sababu hizo" linakuja tatizo kwamba hataki kufanya hivyo, hapa tatizo liko wapi wadau au kuna makosa kumwambia hivyo mpenzi wako!?
Kwel changamoto hiyo ipo,ila kwann msiweke akiba bank tuu ata fixed accnt,kuna watu unakuta kwel anania lkn hajui nidhamu ya PESA.
 
Asa benji ndo inatunza pesa mzee, afu hii yote ni kama hamuaminiani "UPENDO KUVUMILIANA UPENDO KUAMINIANA " Hayo ni maneno ya bible mzee
Bible IPO wazi kuaminiana katika ndoa sio uhuni uhuni tu.hapo ni benki mkuu
 
Na yeye anataka nimfungulie salon ambayo ni zaidi ya milion na nimekubali, sasa kama yeye haniamini mi nimekuwa mjinga kukubali ombi lake?
Wajinga ndio waliwao m sorry to tell you this hamna namna na huyo mwenzako ana plan b..
 
Hakipo kiumbe ambacho sikiamini na sitakaa hata siku moja nikiamini kama MWANAMKE kwa lolote lile tena kuhusu pesa yaani wali ulio pikwa umebakia kuliwa tu bora tuchangie damu sio pesa
 
Mwanamke ni mtu wa kitimiziwa tu, ukitaka ajitimizie au akusaidie kumtimizia, mziki utaucheza! Ukimtimizia mahitaji yake mahusiano utayaona mazuri. Hata kama utakuwa unakwama kwama sehemu Fulani Fulani, lakini wewe ndiyo ubebe jukumu la kumtimizia.
 
Mbona wengi tunawaona tu wanasaidiana? asa kuna faida gani ya kuoa mfanya kazi ni heri asiye na kazi basi umpe biashara akusaidie
 
Habari wanaJF!? Natumai mko poa.

Inatokea mnaweka pamoja mipango kadhaa ya maendeleo na binti unayetarajia kumuoa, ili kutimiza mipango hiyo unatoa robo tatu ya mtaji nayeye anatoa robo tu, mnakubaliana pesa ya matumizi itatokana na hii biashara na hiyo ya mshahara(ambao ni sawa)kila mmoja atachukua kiasi kadhaa tu nyingine yote itunzwe hadi wakati fulani tutakapo itumia kufanya shughuli fulani ...anakubali, tatizo unakuja kugundua kuwa si mtunzaji mzuri wa fedha unaamua kumwambia "pesa ya mshahara inayotakiwa kutunzwa amishiaga kwangu kwa sababu hizo" linakuja tatizo kwamba hataki kufanya hivyo, hapa tatizo liko wapi wadau au kuna makosa kumwambia hivyo mpenzi wako!?

Pesa ya mwanamke ni ya kwake na pesa ya mwanaume ni ya familia period!! Nimejifumza hilo in a hard way
 
Mbona wengi tunawaona tu wanasaidiana? asa kuna faida gani ya kuoa mfanya kazi ni heri asiye na kazi basi umpe biashara akusaidie
Hawasaidiani, Mwanaume anasaidiwa. Ingekuwa wanasaidiana ungeona na Mwanaume anafua, anapika, anapiga deki. Na hiyo kitu unayoiita kusaidiana, ndiyo inayowavimbisha kichwa wanawake na kusababisha vurugu ndani ya ndoa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom