Hata sahaulika ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hata sahaulika !

Discussion in 'Celebrities Forum' started by GeniusBrain, May 23, 2011.

 1. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Na Waandishi Wetu
  Kwa namna ya kipekee, gwiji wa unajimu barani Afrika, marehemu Sheikh Yahya Hussein aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita, hatasahaulika kutokana na historia yake.

  Umati wa kihistoria uliojitokeza kwenda kumhifadhi kwenye nyumba yake ya dawamu, juzi (Jumamosi) na msisimko wenye hadhi ya kitaifa ni pointi nyingine iliyoacha gumzo la kukumbukwa.
  Mwili wa marehemu Sheikh Yahya, ulisaliwa nje nyumbani kwake, Magomeni, baadaye ulipelekwa Msikiti wa Manyema, Kariakoo kwa ajili ya sala nyingine kabla ya kuzikwa kwenye makaburi ya Tambaza, Dar es Salaam.

  Idadi kubwa ya watu waliokuwepo, iliizidi nguvu serikali ambayo ilipanga kuwe na msafara wa pikipiki na magari kuelekea Msikiti wa Manyema.
  Awali, ilipangwa kuwa waombolezaji watembea kwa miguu wangebeba mwili wa marehemu katika jeneza kutoka Magomeni Mikumi hadi Usalama (mataa) ambako ungepakiwa kwenye gari maalumu litakaloongozwa na trafiki mwenye pikipiki ya king’ora.

  Hata hivyo, watu hao waligoma walipofika Usalama, walikataa kumpandisha kwenye gari na kuubeba kwa miguu mpaka Msikiti wa Manyema na baadaye waliuchukua hadi Tambaza.
  Walipokuwa wanagoma, watu hao walipaza sauti kuwa hawawezi kumpandisha Sheikh wao kwenye gari, wakati uwezo wa kumbeba wanao.
  KAULI YA MWISHO
  Sheikh Yahya, alifariki dunia Ijumaa iliyopita njiani akipelekwa Hospitali ya Mt. Mkombozi, Morocco, Kinondoni, Dar es Salaam.

  Hata hivyo, Sheikh ambaye alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu, siku hiyo aliamka salama na kuanza kazi ya kuwahudumia wateja wake (kuwatibu) kama kawaida.
  Gazeti hili limeelezwa kuwa watu wa kwanza kufika ofisini kwake ni 12 ambao aliwahudumia wote.
  Imeelezwa kuwa mtu wa mwisho kuhudumiwa na Sheikh ni mwanamke anayeitwa Winnie.
  Habari zinasema kuwa baada ya kumtibu Winnie, Sheikh aliwaambia wasaidizi wake kuwa amemaliza kazi na kuwataka wampeleke hospitali ambapo alifariki dunia akiwa kwenye gari njiani.

  VIONGOZI SIMANZI
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na makamu wake, Dk. Mohamed Gharib Bilal walihudhuria mazishi hayo.
  Dk. Bilal alikuwa wa kanza kufika, kwani aliwasili nyumbani kwa marehemu saa 4:00 asubuhi na baada ya kutoa salamu za rambirambi aliondoka.
  Aidha, Rais Kikwete alikuwa wa kwanza kufika makaburini, kwani umati ukiwa na mwili wa marehemu ulipofika, ulikuta ameshatangulia.

  Viongozi wengine waliohudhuria mazishi ya mnajimu huyo ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa UPD, John Cheyo na Mchungaji wa Kanisa la GRC, Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’.
  Viongozi hao kwa nyakati tofauti walisema Sheikh Yahya alikuwa mtu wa watu, mpenda amani na aliyekuwa akihimiza mshikamano wa kitaifa bila kujali itikadi za kisiasa.

  Wengine waliokuwepo ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela, Afisa wa ngazi ya juu wa polisi makao makuu, Jamal Rwambow, Mbunge wa Ilala, Musa Zungu, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa, Mbunge wa Ubungo, John Mnyika na Mbunge wa Wawi (CUF), Hamadi Rashid.
  VURUGU
  Vurugu zilizotokea ni zile ambazo ziliifanya serikali izidiwe nguvu na wananchi ambao walishindwa kufuata utaratibu uliowekwa wa kumsindikiza kaburini kiongozi huyo wa dini.

  Mwili wa marehemu Sheikh Yahya ulipofika eneo la Usalama karibu Hoteli ya Travertine, kulitokea mabishano kati ya waombolezaji watembea kwa miguu na mwenyekiti wa mazishi, Sheikh Alhaj Musa Salum ambaye ni Sheikh Mkuu wa Dar es Salaam.
  Sheikh Salum aliwataka waombolezaji kufuata utaratibu uliopangwa lakini waligoma, hivyo kuibua mabishano makubwa ikiwemo kunyang’anyana mwili wa marehemu.

  Mabishano hayo yalichukua dakika tano, baadaye watembea kwa miguu walishinda na kuufikisha mwili wa marehemu kwenye Msikiti wa Manyema na kupokewa na Imamu wake, Sheikh Ahmed Jongo.
  Baada ya sala ya marehemu, ilitakiwa mwili uwekwe kwenye gari lakini wananchi waligoma, hivyo waliubeba hadi Tambaza.
  KAULI YA SHEIKH SALUM
  Katika kumuweka sawa Rais Kikwete, mara tu mwili wa marehemu ulipofikishwa makaburini, Sheikh Salum alisema kwa kutumia kipaza sauti huku akimwangalia kiongozi huyo wa nchi:

  “Mheshimiwa Rais, Sheikh Yahya Hussein alikuwa mtu wa vijana, anapokaa alikuwa akizungukwa na vijana japokuwa alikuwa mtu mzima. Ndiyo maana vijana hawa wamelibeba jeneza hili kutoka nyumbani kwake hadi hapa makaburini licha ya kuwa kulikuwa na gari maalumu la kubeba mwili wa sheikh wetu.”
  MATUKIO YA KUKUMBUKWA
  Katibu wa Halmashauri Kuu CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipopata nafasi ya kuzungumza kwenye mazishi hayo, alisema, Sheikh Yahya hatasahaulika kutokana na utabiri wake uliokuwa ukihimiza amani na mshikamano.

  Alisema, Sheikh Yahya alitabiri CCM na CUF kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na baadaye ikawa hivyo.
  Utabiri mwingine wa Sheikh Yahya ni ule ambao alisema Rais Benjamin Mkapa angeongezewa muda wa kutawala mwaka 2005 na kweli ilitokea hivyo. Hii ilisababisha wanasiasa wengi kukiri kuwa hakuwa mtu wa kawaida.

  Aidha, Sheikh Yahya Hussein aliwahi kutabiri kuwa uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2000 utarudiwa na ikawa hivyo.
  Mnajimu huyo aliwahi kutabiri kesi ya mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya’ na watoto wake watatu waliofungwa jela maisha wataachiwa huru.

  Walipokata rufaa, watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza waliachiwa huru na kuacha mkongwe huyo wa muziki wa dansi akiendelea kutumikia kifungo cha maisha jela na mwanaye mmoja, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’.


  Baada ya hukumu hiyo, sheikh Yahya alisema: “Utabiri wangu haukukosea kabisa, nimepata nusu na nimefeli nusu, lakini naona kinyota Nguza yupo huru, tusubiri mbele ya safari.”

  Mnajimu huyo aliwahi pia kumtabiria aliyekuwa Rais wa Uganda Dikteta Iddi Amini kupinduliwa baada ya miezi sita alipokutana naye jijini Kampala na ikawa hivyo baada ya kupigwa na majeshi ya Tanzania.
  Sheikh Yahya, anakumbukwa na Wakenya baada kutabiri kuwa waziri mmoja wa nchi hiyo angepigwa risasi akiwa karibu na duka la dawa na ikawa hivyo baada ya Tom Mboya kuuawa kama alivyosema.

  Mwaka 2002, alitabiri kuwa atakayeshinda urais Kenya atakuwa na sauti mbuzi na ataapishwa akiwa kwenye kiti cha magurudumu (wheel chair) na ikawa kweli, kwani alishinda Rais Mwai Kibaki na kula kiapo siku chache baada ya ajali ya gari.
  Aidha, aliwatabiria Rais Kikwete kushinda urais, Dk. Ali Mohamed Shein kuwa Makamu wa Rais, akatabiri vifo vya aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk.
  Omar Ali Juma na Waziri Mkuu Mstaafu, Rashid Mfaume
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  May 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Atakumbukwa kama mchawi na mfuga majini mashuuri Afrika mashariki na kati. not otherwise.
   
 3. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #3
  May 23, 2011
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,035
  Trophy Points: 280
  duh....kweli atakumbukwa
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  May 23, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mnajimu huyo aliwahi kutabiri kesi ya mwanamuziki Nguza Viking ‘Babu Seya' na watoto wake watatu waliofungwa jela maisha wataachiwa huru.[/FONT][/SIZE]

  Walipokata rufaa, watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu na Francis Nguza waliachiwa huru na kuacha mkongwe huyo wa muziki wa dansi akiendelea kutumikia kifungo cha maisha jela na mwanaye mmoja, Johnson Nguza ‘Papii Kocha'.
  [/QUOTE]

  Mkuu, nimepoteza kumbukumbu: Hivi waliachiwa watoto wawili au mmoja?
   
 5. Esperance

  Esperance JF-Expert Member

  #5
  May 23, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaman basi tena mwachen akapumzike kila siku thread zake, kesho ntamuanzishia nyingine.
   
 6. olele

  olele JF-Expert Member

  #6
  May 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 814
  Likes Received: 339
  Trophy Points: 80
  hatasahulika for what?, kwa kutumiwa na jk au ccm, au kwa kutabiria wenzake.
   
 7. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #7
  May 23, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Aliwahi kutabiri rais atakayeshinda mwaka 2005 atatokea Zanzibar na kama atatokea bara atakuwa MWANAMKE.(ikawa kweli)
  SITAMSAHAU.
   
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  May 23, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kwa ukumbusho tu - ilikuwa tarehe 25, Machi 2010 !

  MTABIRI maarufu Afrika Mashariki na Kati, Shekhe Yahya Hussein amesema kutokana na viashiria alivyoviona katika mwaka wa kinyota ulioanzia Machi 21 mwaka huu, ametabiri kuwa, wenye majina yanayoanzia na S na T nyota zao zinaonekana kung’ara.

  Kutokana na hilo amesema Spika wa Bunge, Samuel Sita, iwapo kutakuwa na uchaguzi, ataibuka kidedea bila kupingwa, huku aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, akipata nafasi mwaka 2015 lakini si katika uchaguzi huu ambao alisema hautafanyika.

  “Siwezi kuzungumzia zaidi kuhusu kwa nini hakutakuwa na uchaguzi kwa sababu nikisema mtasema ni siasa, lakini nasema tena kwa kujiamini, mwaka huu hakuna uchaguzi,” alisema wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake Dar es Salaam jana.

  Alisema Januari 15 mwaka huu unaotawaliwa na nyota ya kumi ambayo ni ya Mbuzi jua lilipatwa; na Zanzibar ina sura ya mbuzi inayosimamiwa na sayari ya Saturn au Zohal na inahusika na mambo mabaya kama vile kutenganisha wanandoa, vita, kukusanya zana za vita, kuvunjika mambo, kuvunjika shughuli zozote, kufifia kwa mambo, kukithiri fitina, uvumi au mambo ya umbea, kugombanisha watu na kutokea ugomvi kati ya viongozi wa kisiasa.

  Pia alisema kupatwa huko kwa jua kunaashiria vurugu, umwagikaji wa damu, harakati za kijeshi na kashfa za kipolisi, mabadiliko ya uongozi katika ngazi mbalimbali, uasi wa ghafla katika serikali za nchi zilizopitiwa na kupatwa kwa jua hilo ambazo ni Chad, Somalia, Tanzania, Zanzibar, Kongo, Kenya, India, Sri Lanka, Bangladesh na Maynmar.

  Vile vile kutatokea harusi za viongozi na mazishi ya kitaifa, vifo vya watu maarufu vitaendelea hadi Julai mwaka huu, matatizo ya kifedha na uchumi, ukame, matetemeko ya ardhi, kulipuka kwa volkano na habari nyingi zitakuwa ni zinazohusiana na majanga ya kidunia, alisema.

  Alisema pia kutatokea vurugu za uchaguzi katika nchi hizo, watu kufanya maasi na matukio ya kigaidi, kushambuliwa kwa vyombo vya usafiri, kupotea kwa maisha ya watu na mali.

  “Kutokana na hayo natabiri kuwa hakutakuwa na uchaguzi mkuu mwaka huu, hakutakuwa na mpasuko ndani ya CCM, uchaguzi ujao robo tatu ya wabunge walioko madarakani wataanguka na Bunge lijalo litakuwa na sura nyingi mpya na wanawake wataongezeka sana,” alisema.

  Aidha alitabiri kuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, ataongezwa muda wa urais kwa kipindi kingine ambapo pia urais Tanzania na Zanzibar utakuwa na ushindani mkubwa kuliko miaka mingine yoyote. Pamoja na hayo alisema kuanzishwa kwa Chama Cha Jamii (CCJ) kulilenga kuivunja CCM kupitia wanachama wake, hata hivyo akatabiri kuwa chama hicho hakitafanikiwa, kwa kuwa jina lililotimia la CCJ kinyota halikufaa na kama angepewa nafasi ya kuteua jina angetumia CCN.

  Aidha, alisema katika utabiri alioutoa Desemba 27 mwaka jana, watu wengi hawakumwelewa au wengine hawakukubaliana nao kwa maslahi yao.

  “Ninawahakikishia na kuwafahamisha kwamba mimi ninapotoa utabiri wangu huwa simlengi mtu wala simtabirii mtu, natoa utabiri kwa manufaa ya jamii, kwa hiyo ni wajibu wa kila mtu ama kukubali au kukataa haya ambayo ninayasema,” alisema.

  Alisema katika mkutano huo alitabiri kutokea kifo cha kiongozi wa zamani wa kitaifa na baada ya siku chache alifariki dunia aliyekuwa Waziri Mkuu Rashidi Kawawa, pia alitabiri atakayempinga Rais Jakaya Kikwete ndani ya CCM atakufa ghafla.

  Alisema kauli hiyo ilileta utata mkubwa na kuongeza kuwa bado suala hilo lipo kwa sababu muda wake bado. “Na kwa ufafanuzi sikusema viongozi wa upinzani nilisema ndani ya CCM, pia nilitabiri upinzani ndani na nje ya CCM, kutokea kwa Serikali ya Mseto, hali ya uchumi Tanzania itaboreka na Waziri Mkuu ajaye atatokea Upinzani,” aliongeza.

  Huyo ndiye alikuwa Mlinzi Mkuu wa Jakaya Mrisho Kikwete !
   
 9. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Maskini wanapaswa kuwa na sauti moja, sauti ya Umoja na ikiwezekana lazima kuwa na chama ambacho wanakiamini kuwa kitajali maslahi na haki zao! Huo ndio ulikuwa Msingi wa CCM enzi za Mwalimu Nyerere. Takribani miongo miwili sasa Maskini wa Tanzania wanatafuta chama na chombo ambacho kitawaunganisha na kuwa sauti yao mara baada ya CCM kuwa kengeuka. Hivi sasa maskini wa Tanzania hawana pa kushika si mbele ya Serikali yao ya CCM wala si Mbele ya Dini zao wanazoabudia, Matajiri a.k.a Mafisadi wameshika hatamu katika kona zote za nchni tokea ndani ya vyama, makanisani hadi Misikitini.

  Nimeandika hayo maneno hapo katika aya ya kwanza nikishangazwa inakuwaje Yahya kuzikwa kwa heshima zote za Dini ya Kiislam wakati matendo na mambo yote aliyokuwa anafanya wakati wa uhai wake ni ushirikina na Mwenyezi Mungu hapendi Ushirikina, Dini ya Kiislam pia haikubaliani na Ushirikina.

  Jibu rahisi na la haraka ni kuwa wenyewe pesa wanafunguliwa milango haraka makanisani na misikitini na hata katika vyama vya siasa bila kujali hizo pesa wamezipata wapi! hii ndio maana tumeona mara kadhaa pamoja na dhambi ambayo mtu kama RA ameitendea TZ bado utamuona anakaribishwa kanisani kwenye harambee ya kununua vyombo vya music kwa ajili ya kwaya kwenye kanisa fulani fulani! Bado utasikia Dini fulani fulani kwao yanayofanywa na CCM na serikali yake ni sawa na yemepitishwa mbele ya Mungu kwa sababu pesa inaweza kupatika kwa haraka iwapo utawatetea hao viongozi wa CCM; Mstakabali wa Taifa upo mashakani, hivi sasa watanzania wanatupa turufu yao ya mwisho kwa kuweka matumani kwa CDM, lakini nayo kama chama cha siasa lolote laweza kutoka mbeleni, huo ndio utakao kuwa mwanzo na mwisho wa Amani ya Tanzania, maana tamaa itakatwa na liwalo linaweza kuwepo, siombei tufike huko lakini matendo yetu yatatufikisha tusipo angalia hatua zetu.

  Nilazima makanisa na misikiti pia ijiangalie kama haijawa mapango ya wanyanganyi na kama bado ni tumaini la wanyonge waliodhoofika mioyo, roho na miili yao.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
   
 10. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Yaani unatumia muda wote kutashauri kumkumbuka mchawi na mtu aliyeiharibu ikulu kwa uchawi? Siwasomi mjue!
   
 11. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Ama kweli ilikula kwetu! Alituharibia sana rais kumbadilisha! Ona sasa tunavyopata shida
   
 12. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  kwa hiyo huyo rais aliyetokea bara ni mwanamke?
   
 13. a

  andry surlbaran Senior Member

  #13
  May 26, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha ha ha ha dahh kuna watu wana maneno mmh!!
   
 14. c

  chetuntu R I P

  #14
  May 26, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 954
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  inawezekana aisee kumbe kinyota alishaliona. Mmmh tumkague vizur ukute ni ke.
   
 15. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  katangulia, tumuache apumzike sasa kwa amani ashafanya sehemu yake duniani.
   
 16. Mamushka

  Mamushka JF-Expert Member

  #16
  May 28, 2011
  Joined: Feb 17, 2010
  Messages: 1,609
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Afunguliwe babu sea, afunguliwe babu sea afunguliwe babu seaaaaaaaaaaaaaaaaa! aaah Shehe kapumzika basi, babu sea atolewe bana imetosha bana aaa.
   
 17. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #17
  May 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Yuko na Osama jehanamu hii ni fact!
   
 18. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #18
  May 28, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,164
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  Hatasahaulika kwa kushirik kikamilifu kwny kitengo cha propaganda cha ccm.
   
Loading...