Hata Mungu hapendwi na wafuasi wa shetani

sheiza

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
7,565
11,479
Juzi kama kawaida ya kupokea maneno kwa baadhi ya watanzania na kuyachukua bila kuyafanyia tathmini, kuliibuka taarifa ya Rais Magufuli kuumwa na wakati huo huo kudai kafa. Taarifa hii ilianzishwa na kikundi cha watu ambao ni kawaida vikundi kama hivyo kuwepo katika jamii zetu hizi za kiafrika. Japo ilishadadiwa zaidi na wanasiasa ambao ni mtandao wa kikundi hicho.

Baadhi ya wafuasi wao na wale ambao wako tofauti na utawala huu walishabikia na kufurahia. Ikumbukwe kuwa kulikuwa na watu hususani wanasiasa na wafanyakazi wa serikali wachache ambao waliishi kama wako peponi kwa kutumia jasho la wengi.

Mifumo ya upigaji dili kupitia wafanyakazi hewa, bandari, TRA, vyeti feki, safari zisizo na tija, kutengeneza vikao na warsha na kujilipa posho, biashara zao kuchajiwa VAT, matumizi mabaya ya majukwaa ya siasa, udhibiti wa fedha haramu, udhibiti wa madawa ya kulevya, sheria kali za kulinda mali asili kama tembo, misitu na faru na mambo mengine vimeyafanya haya makundi kuibuka na hoja za mara kwa kujaribu kuionyesha jamii kuwa JPM hatoshi.

Wengi wamekuwa wakipuuzwa na maoni hayo wakiwemo kina zitto sababu wanafahamika walipotoka na walipo sasa kupitia ukwasi walio nao.

Haya ni makundi ambayo yanaonyesha chuki ya wazi baada ya kushindwa kumdhibiti mtawala kama walivyofanikiwa tawala zilizopita.

Hii si mara ya kwanza sababu hata Rais Kikwete alitukanwa sana yeye na familia yake na alichukiwa waziwazi. Yeye alizomewa waziwazi na hata kupopolewa mawe kwenye misafara yake kama pale Tegeta na kuzomewa na wanachuo wa UDSM.

Lakini kazi kubwa inayofanywa na Rais Magufuli inamgusa mtu mmoja mmoja. Mkulima ataguswa na miundo mbinu ya barabara, kuondoa tozo, na uhakika wa soko la mazao. Mfugaji halikadhalika uondoaji wa tozo na kutengewa maeneo ya ufugaji. Mtoto wa maskini sasa ana uhakika wa kusoma kuanzia la kwanza hadi chuo kikuu.

Mfanyabiashara ana uhakika wa kusafiri nje na ndani ya Tanzania haraka kwa kutumia usafiri wa ndege ambapo sasa kila mkoa ndege zinatua baada ya uboreshaji wa viwanja na ununuzi wa ndege.

Machinga anafanya biashara bila mawazo. Anapoamkia asubui ndipo anapifungia biashara. Hana tena wasiwasi wa kukimbizwa kama yupo uwanja wa vita kwani wameletewa vitambulisho kama utambulisho wai. Raia sasa anapata huduma bila mawazo ya kuweka rushwa kwanza ili ahudumiwe kwenye sekta zote za serikali.

Kilichotokea hiyo ni hulka ya wafuasi wa shetani. Wafuasi wa shetani huwa hawampendi Imamu, Sheikh, Askofu wala Mchungaji. Sisi tunasema Magufuli umekanyaga penyewe, vile visiki umeviondoa na vimeonekana waziwazi.

HATA MUNGU HAPENDWI NA WAFUASI WA SHETANI.
 
Shetani ni yule aliyesema maiti za Ruvu ni kawaida.aliyewabomolea nyumba Kimara.Akala rambirambi za kagera.Akamuuwa mawazo na kumpoteza saa8,akamimina risasi kwa Lissu.Ana chuki na ukabila huyu ni mfuasi wa shetani.shetani hawezi kupendwa na wana wa Nuru ambao wanataka haki.Nuru na giza haziwezi kukaa sawa.

Eti wengi wanaunga mkono.
 
Mleta mada umenena kwa ufasaha sana,
Tatizo ni kwamba hata hii JF kiongozi wake ni mmoja wa washereheshaji.
So humu ni sebuleni kwao pa kutoloa sumu.
 
Ni kweli kabisa,Hata shetani anachukiwa na kukemewa sana na wafuasi watiifu wa Mungu.Na shetani anapokemewa na wafuasi wa Mungu anajitutumua sana lakini baadaye lazima atii nguvu ya Mungu.
 
Chama Cha Mashetani
1571388941950.jpeg
 
Juzi kama kawaida ya kupokea maneno kwa baadhi ya watanzania na kuyachukua bila kuyafanyia tathmini, kuliibuka taarifa ya Rais Magufuli kuumwa na wakati huo huo kudai kafa. Taarifa hii ilianzishwa na kikundi cha watu ambao ni kawaida vikundi kama hivyo kuwepo katika jamii zetu hizi za kiafrika. Japo ilishadadiwa zaidi na wanasiasa ambao ni mtandao wa kikundi hicho.

Baadhi ya wafuasi wao na wale ambao wako tofauti na utawala huu walishabikia na kufurahia. Ikumbukwe kuwa kulikuwa na watu hususani wanasiasa na wafanyakazi wa serikali wachache ambao waliishi kama wako peponi kwa kutumia jasho la wengi.

Mifumo ya upigaji dili kupitia wafanyakazi hewa, bandari, TRA, vyeti feki, safari zisizo na tija, kutengeneza vikao na warsha na kujilipa posho, biashara zao kuchajiwa VAT, matumizi mabaya ya majukwaa ya siasa, udhibiti wa fedha haramu, udhibiti wa madawa ya kulevya, sheria kali za kulinda mali asili kama tembo, misitu na faru na mambo mengine vimeyafanya haya makundi kuibuka na hoja za mara kwa kujaribu kuionyesha jamii kuwa JPM hatoshi.

Wengi wamekuwa wakipuuzwa na maoni hayo wakiwemo kina zitto sababu wanafahamika walipotoka na walipo sasa kupitia ukwasi walio nao.

Haya ni makundi ambayo yanaonyesha chuki ya wazi baada ya kushindwa kumdhibiti mtawala kama walivyofanikiwa tawala zilizopita.

Hii si mara ya kwanza sababu hata Rais Kikwete alitukanwa sana yeye na familia yake na alichukiwa waziwazi. Yeye alizomewa waziwazi na hata kupopolewa mawe kwenye misafara yake kama pale Tegeta na kuzomewa na wanachuo wa UDSM.

Lakini kazi kubwa inayofanywa na Rais Magufuli inamgusa mtu mmoja mmoja. Mkulima ataguswa na miundo mbinu ya barabara, kuondoa tozo, na uhakika wa soko la mazao. Mfugaji halikadhalika uondoaji wa tozo na kutengewa maeneo ya ufugaji. Mtoto wa maskini sasa ana uhakika wa kusoma kuanzia la kwanza hadi chuo kikuu.

Mfanyabiashara ana uhakika wa kusafiri nje na ndani ya Tanzania haraka kwa kutumia usafiri wa ndege ambapo sasa kila mkoa ndege zinatua baada ya uboreshaji wa viwanja na ununuzi wa ndege.

Machinga anafanya biashara bila mawazo. Anapoamkia asubui ndipo anapifungia biashara. Hana tena wasiwasi wa kukimbizwa kama yupo uwanja wa vita kwani wameletewa vitambulisho kama utambulisho wai. Raia sasa anapata huduma bila mawazo ya kuweka rushwa kwanza ili ahudumiwe kwenye sekta zote za serikali.

Kilichotokea hiyo ni hulka ya wafuasi wa shetani. Wafuasi wa shetani huwa hawampendi Imamu, Sheikh, Askofu wala Mchungaji. Sisi tunasema Magufuli umekanyaga penyewe, vile visiki umeviondoa na vimeonekana waziwazi.

HATA MUNGU HAPENDWI NA WAFUASI WA SHETANI.
Hivi yule jamaa aliyekunywa damu ya Ben saa8 ambaye pia alitaka kunywa damu ya lissu ni mfuasi wa upande UPI vile??
 
Shetani Hana jema
1. Analeta mateso kwa watu wa mungu (mfano Ayoub mtu wa Usi)
2. Anauwa watu wa mungu ( kaini)

Shetani Hana jema kabisa kazi yake Ni uharibifu tu.
 
Lila na fila.........................
Nuru na giza.........................
ILA watanzania tujikabidhi kwa Mungu na kumrudia ili turudi ktk umoja na mshikamano wetu kama zamani. Tujiombee sana sana ili tusifike kwenye mfarakano mkubwa zaidi kwani ilitakuwa ni kilio na kusaga meno
 
Back
Top Bottom