Hata kama una haki....

Hata kama una haki....

Kosa halihalalishwi na kosa ...JPM kuropoka sometimes ni kosa pia ....hao akina Lissu ndio walipaswa kuwa mfano wa hekima na busara ...aache kuropoka hovyo kwasababu tu ni haki yake ....
 


Hata kama tuna haki ya kuwasema wale wote tuliowapa mamlaka...

Hata kama tuna haki ya kuwakosoa wale wote tuliowapa mamlaka...

Hata kama tuna haki ya kuwakemea wale wote tuliowapa mamlaka...

Wewe Tundu Lissu wewe...kuwa tu na haki ya kufanya jambo fulani haimaanishi ndo ujitoe kabisa fahamu na kuanza kuropoka ropoka kama mwendawazimu.

Kuwa tu na haki ya kusema, kukosoa, na kukemea haimaanishi ndiyo usitumie hekima na busara katika kufanya hivyo.

Ni lazima uwe mwangalifu. Ni muhimu kuchagua maneno yako vizuri hususan kama wewe ni mmoja wa viongozi wenye ushawishi kwenye jamii.

Kusema rais Magufuli anaendesha nchi kwa upendeleo wa kikabila na kikanda ni uongo. Ni uzushi. Na ulikosea.

Hata kama una haki ya kusema hayo uliyoyasema, huna haki ya kuzusha mambo ili tu ujipatie pointi za kisiasa.

Leo hii likitokea sokomoko kati ya wananchi wa kanda ya ziwa na wa kwingine kisa hayo maneno yako, utalizuia? Si ajabu utajificha kama ulivyojificha mahakamani kule Dodoma ukiogopa kupandishwa kwenye Difenda😀.

Kuwa na haki si sababu ya kuacha kuwa makini. Jirekebishe.


Usisikilize Bongo flava tu, vipi kuhusu 'muziki wa dansi'?

 
Kosa halihalalishwi na kosa ...JPM kuropoka sometimes ni kosa pia ....hao akina Lissu ndio walipaswa kuwa mfano wa hekima na busara ...aache kuropoka hovyo kwasababu tu ni haki yake ....

Exactly!

Halafu ni mara ngapi humu tumemsema Magufuli kwa uropokaji wake?

Watu wana selective moral outrage na selective amnesia ya ajabu sana.
 
Lisu nilikua simuelewi ila sasa namuelewa sana usipomuelewa leo utamuelewa kesho, The guy is genius anatambua mambo mapema sana hata kabla wengi wetu hatujaona, Anafaa kutumiwa kama dira na mwenye mamlaka.

Sent using Jamii Forums mobile app

Lissu ni genius?

Genius aliyeshindwa kutambua blunder ya kumkaribisha Lowassa CHADEMA na kumteua kuwa mgombea wao wa urais?

Really? Seriously?
 
Huyo Magufuli alitutukana sana Wahaya, tena matusi ya nguoni , isitoshe akatufanyia dhuluma kubwa kwenye pesa zetu ambazo watanzania wenye huruma walituchangia.

Ipo siku........





Sent using Jamii Forums mobile app

Lakini si tunaambiwa anapendelea kanda ya ziwa? Iweje sasa aliwatukana na kuwadhulumu pesa zenu mlizochangiwa na Watanzania?
 
Kosa halihalalishwi na kosa ...JPM kuropoka sometimes ni kosa pia ....hao akina Lissu ndio walipaswa kuwa mfano wa hekima na busara ...aache kuropoka hovyo kwasababu tu ni haki yake ....
Unapata wapi uhalali wa kumkosoa wa pili na hujamkosoa wa kwanza wakati wamefanya kosa lile lile?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom