Hata huku JF wapo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,084
Ni vikongwe, matumbo joto, wajivuni, wanaovutiwa, mashabiki damu, na mashabiki jina

VIKONGWE :hawa ni watu muhimu JF ukongwe wao unatokana kuwepo muda mrefu jamvini wanajua mengi na wana uzoefu mkubwa na jukwaa

MATUMBO JOTO :hawa bila kujali ni wakongwe au la ni watu wa kupaniki na kupata jakamoyo hata kwa kitu kidogo tu kwenye post zao, akipost kitu atatamani kila wakati aingie jamvini aangalie nani kareply nini! Ole wako uende kinyume na msimamo wake

WAJIVUNI :Hili ni tabaka ndani ya JF ambao wao wanajioni ni 'untouchables ' wao ndo wao wao ndio wanajua kupost vitu vya 'maana ' wao ndio wenye hekima wanajiona wao ndio JF na JF ndio wao, hawawakubali newcomers hasa wenye misimamo tofauti na yao

WANAOVUTIWA :Hawa saa nyingine wanachekesha kwelikweli huwa hawaangalii kimepostiwa nini wao wanaangalia kapost nani! Kwao maudhui si tija, tija ni nani kapost

MASHABIKI DAMU :Hawa huwezi kuwaambia kitu kuhusu JF, wakikaa saa nzima bila kuchungulia forumuni wanakuwa kama wagonjwa muda wote wapo hata iwe ni usiku wa manane wanapost wanalike wanapm, kila kona ya JF wapo, usiwacheke usiwabeze ni mashabiki damu

MASHABIKI JINA :Hawa ni watu wa kufuata mkumbo haijui JF hajasoma masharti na vigezo vyake anaingia mzima mzima anapost uchafu, anacoment upuuzi mara yuko huku mara yuko kule ukimchallenge kidogo tu anakinukisha mbaya

JF ni yetu sote tuvumiliane kwa kila hali wakongwe wawabebe na kuwaelekeza wachanga, wakifinyangwa vizuri ndio the next great thinkers
 
Wewe upo upande gani mkuu?

Siwezi kujihukumu, ushiriki wangu ndani ya JF ndo unaweza kutoa majibu! Nachangia nini napost nini nalike nini vyote hivyo ndio vinaweza kuniweka kwenye kundi mojawapo kati ya hayo
 
kaka mshana jr, kweli umefanya udadisi sasa waonaje tukajipanga huko kwenye magrupu hayo....?

Kabanga haya ni makundi ya kimtazamo na kihaiba yanatokea automatically
 
Last edited by a moderator:
Uchambuzi umetulia sana;
Kamilisha kwa kuujazia nyama;
Kila kipengele weka majina walau mawili au matatu hivi.
 
MASHABIKI JINA :Hawa ni watu wa kufuata mkumbo haijui JF hajasoma masharti na vigezo vyake anaingia mzima mzima anapost uchafu, anacoment upuuzi mara yuko huku mara yuko kule ukimchallenge kidogo tu anakinukisha mbaya
..................... @sayansi kimu
 

Hahahahaaaaaa
 

Hivi huyu Sayansi kimu na Mstahiki meya wapo kweli maana siku nyingi hawajapost mambo yao.
 

ah SAYANSIKIMU anahusika....
 
Last edited by a moderator:
mshanajr,mie nipo kundi gani?
 
Last edited by a moderator:
Natoa huduma ya kumwambia kila mtu kundi lake..

Nianze na nani?
 
Anza na mimi mkuu TANMO then uniambie malipo bei gani kama utafanikiwa au kukaribia na ukweli.
Natoa huduma ya kumwambia kila mtu kundi lake..

Nianze na nani?
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…