Hata hujatolewa mahari unahamia kwa mwanaume

Hata hujatolewa mahari unahamia kwa mwanaume

Mkachunguze kwanza wazazi wenu walifuata hayo kabla? Haya mambo sio mapya, yapo tangu kale. Uchagani wanaweka begani kisha wanatuma wazee wakatoe taarifa binti yenu yupo kwetu period.

Zama hizi jaribu kuweka begani kama hutafia jela. Hayo mambo ya kuweka begani yalingatuka na mwalimu
 
Ha ha ha ndachuwa andaa disko vumbi pale kwako uone kama hatuja weka begani mpwa wako, ukizubaa hata wewe tunaweka begani.
 
Ni jambo la kushangaza lakini ndio ukweli huo wanawake waliowengi wanakosea sana katika maisha yao wanakubali kujidhalilisha kuhamia nyumbani kwa mwanaume wakati hata mahari hajatolewa kwa wazoefu wa mambo haya wanadai wanawake wa aina hii wana matatizo ya akili kwamba wanajiona ni watu wasio na soko tena na hivyo kulazimisha mapenzi kwa wanaume zao kwa kuhamia nyumbani kwao.

Kama kuna mwanaume anakupenda hawezi kukubali kuishi na wewe nyumbani kwake bila kukutolea mahari lazima atakutolea mahari kwa kufuata taratibu zilizowekwa hata kwenda kanisani au msikitini mkale kiapo mbele ya mungu.Watafiti wanasema mwanamume ambae anaishi na mwanamke bila Kufuata taratibu maana yake halisi ni kwamba hana mapenzi sana ya muda mrefu na mwanamke husika.

Kazi kwenu wasichana na wale mnaokubali kuishi bila taratibu

Kwann unataka kutuharibia.?
 
haya mambo hayatabiriki wapo waliohamia na wakaolewa wapo hawajawahi kuhamia but ndo hvyo tena miaka onaenda
 
Back
Top Bottom