Hata hujatolewa mahari unahamia kwa mwanaume

Hata hujatolewa mahari unahamia kwa mwanaume

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,355
Reaction score
16,401
Ni jambo la kushangaza lakini ndio ukweli huo wanawake waliowengi wanakosea sana katika maisha yao wanakubali kujidhalilisha kuhamia nyumbani kwa mwanaume wakati hata mahari hajatolewa kwa wazoefu wa mambo haya wanadai wanawake wa aina hii wana matatizo ya akili kwamba wanajiona ni watu wasio na soko tena na hivyo kulazimisha mapenzi kwa wanaume zao kwa kuhamia nyumbani kwao.

Kama kuna mwanaume anakupenda hawezi kukubali kuishi na wewe nyumbani kwake bila kukutolea mahari lazima atakutolea mahari kwa kufuata taratibu zilizowekwa hata kwenda kanisani au msikitini mkale kiapo mbele ya mungu.Watafiti wanasema mwanamume ambae anaishi na mwanamke bila Kufuata taratibu maana yake halisi ni kwamba hana mapenzi sana ya muda mrefu na mwanamke husika.

Kazi kwenu wasichana na wale mnaokubali kuishi bila taratibu
 
Mwanamke Amegawa Kwa Wanaume Tisa Wote Wamempiga Chini Wameishia Kuunganisha Vikojoleo Vyao Alafu Unajitokeza Jamaa Unamwambia Leo Unabid Ubaki Anze Kusuasua Et Anasubili Upeleke Mali Unafanya Masihara Nini Wewe Ndoa Zinatafutwa Asikwambie Mtu Watu Mpaka Wanadiriki Kusema Sikuhizi Wanaume Hawaoi Huku Ukipita Kila Nyumba Watu Wanaishi Na Wake Zao Ni Kwasababu Amedanganywa Mpaka Bas
 
Tatizo linaanzia katika nyakati tunazoishi...nyakati hizi zimejaa waigizaji na waongo kuliko UKWEL halisi wa mambo...kwanza lazima uelewe dhana nzima ya NDOA maana yake ni nini,lakini pia lazima uelewa kuwa kwenye NDOA lazima uhakikishe unajenga mazingira ya FURAHA kabla yakuingia ndani ya NDOA hiyo...furaha na raha huwa zinajengwa na huwa zinachukua muda mrefu kujengwa..

Huwezi sema utamchunguza nakumuelewa kimtazamo mtu ambaye utaishi nae akiwa mbali...unahitaji mtu ambaye anatambua majukumu yake kama mke au mama wa familia,lakini pia unahitaji mtu ambaye anajua kuwa yeye ndio muangalizi wa kila siku kila mara wa familia na ndio maana jukumu hilo akapewa mwanamke...Mara nyingi tumeona wanaume wakilalamika hapa jukwaan na kwingine kuwa wanawake zao waliwadangaya hiki au kile au maumbile yao yapo hivi mara yapo vile,mara hawajui kuhudumia familia na mambo kama hayo...

lakini pia wanawake nao wamekuwa ni hodari sana kulalamika kuhusu waume zao...ukichunguza kwa umakini utagundua kukosekana kwa hali yakukaa pamoja kwa muda mrefu kumechangia sana hali hii...Ukwel ni kuwa siyo kila mpenzi utayekuwa nae ni mume au mke wako...lakini utajuaje au kupata majibu hayo??ni watu kukaa pamoja,ili kama unaona unaweza ishi nae lakini ukamrekebisha kidogo baadhi ya mambo ndo wakat huo...ni ngumu sana kumrekebisha mtu mkishaingia ndani ya ndoa...Kwa hiyo ndio kusema ni vyema kukaa na mtu ili mfahamiane vizuri kuliko kufahamiana mkishafunga ndoa....
 
Sisi ndo tuliofanya kufahamiana kuwe kitu cha muhimu. But religiously and ethically... It ain't important at all

Ni kweli. Ila kufahamiana ni muhimu sana bado. Lazima mjue kama chemistry ipo. Sio kuja kufika mbele, halafu mnagundua hakuna combination kati yenu.
 
Tumesikia....ila tukishapenda huwa hatuambiliki
Teh Teh bora umesema wewe mwenzao! Katika hili hata ungefanya nini halitoweza kubadilika kabisa labda mwanamke kama hajapenda na ana malezi ya aina yake!

Wanawake kila leo wanapewa somo ili lakini haliwaingii kamwe...
 
Mwanamke Amegawa Kwa Wanaume Tisa Wote Wamempiga Chini Wameishia Kuunganisha Vikojoleo Vyao Alafu Unajitokeza Jamaa Unamwambia Leo Unabid Ubaki Anze Kusuasua Et Anasubili Upeleke Mali Unafanya Masihara Nini Wewe Ndoa Zinatafutwa Asikwambie Mtu Watu Mpaka Wanadiriki Kusema Sikuhizi Wanaume Hawaoi Huku Ukipita Kila Nyumba Watu Wanaishi Na Wake Zao Ni Kwasababu Amedanganywa Mpaka Bas

Tatizo linaanzia hapo sasa
 
Tatizo linaanzia katika nyakati tunazoishi...nyakati hizi zimejaa waigizaji na waongo kuliko UKWEL halisi wa mambo...kwanza lazima uelewe dhana nzima ya NDOA maana yake ni nini,lakini pia lazima uelewa kuwa kwenye NDOA lazima uhakikishe unajenga mazingira ya FURAHA kabla yakuingia ndani ya NDOA hiyo...furaha na raha huwa zinajengwa na huwa zinachukua muda mrefu kujengwa..Huwezi sema utamchunguza nakumuelewa kimtazamo mtu ambaye utaishi nae akiwa mbali...unahitaji mtu ambaye anatambua majukumu yake kama mke au mama wa familia,lakini pia unahitaji mtu ambaye anajua kuwa yeye ndio muangalizi wa kila siku kila mara wa familia na ndio maana jukumu hilo akapewa mwanamke...Mara nyingi tumeona wanaume wakilalamika hapa jukwaan na kwingine kuwa wanawake zao waliwadangaya hiki au kile au maumbile yao yapo hivi mara yapo vile,mara hawajui kuhudumia familia na mambo kama hayo...lakini pia wanawake nao wamekuwa ni hodari sana kulalamika kuhusu waume zao...ukichunguza kwa umakini utagundua kukosekana kwa hali yakukaa pamoja kwa muda mrefu kumechangia sana hali hii...Ukwel ni kuwa siyo kila mpenzi utayekuwa nae ni mume au mke wako...lakini utajuaje au kupata majibu hayo??ni watu kukaa pamoja,ili kama unaona unaweza ishi nae lakini ukamrekebisha kidogo baadhi ya mambo ndo wakat huo...ni ngumu sana kumrekebisha mtu mkishaingia ndani ya ndoa...Kwa hiyo ndio kusema ni vyema kukaa na mtu ili mfahamiane vizuri kuliko kufahamiana mkishafunga ndoa....

Tafiti zinaonyesha walio wengi huishia kufukuzwa hata kama wamezaa watoto kisa tu hajatolewa mahari kama njia ya kwenda kanisani Au msikitini
 
Na kufahamiana sio mpaka ahamie kwako nje ya kwako pia mnaweza kufahamiana huku utaratibu wa mahari ukifanyika kwa kua ni kosa kubwa kuishi na mwanamke ambae pande zote mbili za wazazi hazijakubaliana
 
Bado huwa wanaotoa mahali du!,maanake unamnunua mwanamke ,bado haohao wazazi wake watakuwa wanaomba huduma...
 
Katika hili wanalaumiwa wanawake tu kwakuwa desturi inaonyesha hivyo lkn pia kuna wanaume ama vijana wanao hamia kwa wenza wao kabla ya ndoa hili pia linawahusu

Nakubaliana na hoja kwa maana ya misingi ya ndoa na taratibu za kiimani lkn kwa upande mwingine amabao ndiyo unaleta athari zaidi sikubaliani sababu kwa mazingira ya sasa kuna umuhimu wa kuwa na muda wa kutosha kufahamiana japo haufai kuwa mrefu sana, maana tumeona kuna ndoa nyingi zimevunjika kwa sbb ama wanandoa hawakupata kufahamiana vya kutosha hivyo inatoa fursa ikiwezekana kuishi pamoja kwa kipindi cha muda mfupi ili kila mmoja kutambua mwenzake anafaa kuwa mwenza wa ndoa ama la
 
Sasa huoni kama kufanya hivyo ndio atahamia kabisa

Akihamia kabla pia ni poa zaidi. Nitapata nafasi ya kujua kama ningependa kuwa naye maisha yangu yote, ama lah. Kama manzi anastahili mimi kuwa naye, nitakuwa naye tu.
 
Back
Top Bottom