Hassan Ngoma @ Clouds 360 : Rais yupo kwenye Kwaresma asichokozwe

Binti Msichana

Senior Member
Oct 9, 2016
109
247
Akiwa na mtangazaji mwenza Baby Kabaya wametoa rai kwa watendaji wa serikali wasimchokoze rais kwani kipindi hiki ni cha kujizuia na kutafakari maisha ya Yesu.

Hivyo wasimlazimishe rais atumbue tumbue kwa utendaji wao mbovu badala yake wasimamie maadili ya Nazi.

Aliyasema hayo kwenye kipindi cha Clouds 360 cha leo asubuhi.
 
Ya kaisari......... Hapa kazi tu.kila siku unatakiwa kujua Mungu yuko na unatakiwa kutubu dhambi zako. Inamaana tokea mwaka jana hakumjua Mungu hadi kuanzia jana? Inamaana angekufa jumatatu angeenda upande gani?
 
Clouds media na watendaji wake wanajaribu sana kutetea issue ya makonda ila wakae wakijua hakuna mwenye nguvu zaidi ya umma umma ukiamua umeamua kwaiyo nyie pigeni kelele ila suala la David Albert bashite ni noted kuanzia ngazi ya shina, kijiji, mtaa, tarafa , wilaya, mpaka mkoa na sasa ipo taifa Daudi akiachwa basi itakuwa mfano kwa kizazi chetu so mshaulini tu Mh Rais atengue uteuzi wake Na afikishe mahakamani kujibu tuhuma
 
Nilitegemea clouds wamshauri Magu katika kipindi hiki atubu dhambi alizowafanyia aliowatumbua kimakosa, amlilie aliyekuwa mkurugenzi wa jiji la dar marehemu Wilson Kabwe, aruhusu mikutano ya hadhara, aziache mahakama ziwe huru, bunge liwe huru, arudishe bunge live, kifupi atubu dhambi na kuzijutia.
 
Kwa Kabwe wacha bwana yule alikuwa mkurugenzi wa wakurugenzi apumzike kwa amani ila hakustahili kuendelea kuwepo kwenye nafasi ile kama jiji LA Mwanza,kingine kwani wakati anagombea alituambia kipindi ili cha siku 40 asisumbuliwe,mbona wana wa Israel walitesa kwa miaka 40 kutoka utumwa kwenda nchi ya Ahadi,ni lazima akubali changamoto zote
 
Clouds ina washereheshaji si watangazaji
Hivi yule jombaa wa mawingu media si alitajwa kwenye list ya Bashite kwamba nae pia anajihusisha na biashara ya Ngada, mbona kama issue yake ilipotea kimya kimya?
 
Imenikumbusha comment ya mtu mmoja katika uchaguzi wa nchi moja ya ughaibuni aliyekuwa akiwaasa watu eti wasimchague mtu wa jinsia fulani kwenye nafasi ya maamuzi makubwa kwa maana kuna wakati anakuwa katika siku fulani fulani na ikitakiwa maamuzi ya haraka nchi itakwama!
Kuna haja ya kuainisha ili katika katiba kama lilivyo la kumuweka mtu mahabusu miezi sita kwa dhamana iliyo wazi!
 
Hakifanya Kazi kwa mujibu Wa sheria sizani kama nikosa na nafikiri akitumbua atakuwa anapata swawabu kubwa kwa Mungu maana bado atakua anawasaidia wananchi wenye kuitaji maendeleo na kwa kipindi hiki tunashauriwa kuwasidia wenye kuitaji.Mi naona ndo kipindi bora kabsa cha kufagia wale wasiotenda mema kwa wananchi
 
Nimegundua asilimia 95 ya waliyomo humu ni mashabiki wa kutupwa wa CLOUDS radio na tv hahahahah nilifikiri mnaumia na clouds kumbe ndiyo njia yenu ya Kuisapoti Hongereni sana wazee wa Clouds lakini ndiyo radio pekee nchini ukubali ukatae
 
Akiwa na mtangazaji mwenza Baby Kabaya wametoa rai kwa watendaji wa serikali wasimchokoze rais kwani kipindi hiki ni cha kujizuia na kutafakari maisha ya Yesu.

Hivyo wasimlazimishe rais atumbue tumbue kwa utendaji wao mbovu badala yake wasimamie maadili ya Nazi.

Aliyasema hayo kwenye kipindi cha Clouds 360 cha leo asubuhi.
Kama ni hivyo Rais achukue likizo kipindi hiki cha kwaresma ili asikwaze na masuala ktk utendaji wake bali akae akifunga na kuomba kwa siku 40...
 
Back
Top Bottom