Hassan Nassor Moyo Hassan, Rais wa Zanzibar na Waziri Kiongizi ambaye hakuwa ingawa alitajwa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
HASSAN NASSOR MOYO RAIS WA ZANZIBAR NA WAZIRI KIONGOZI AMBAE HAKUWA INGAWA ALITAJWA

Kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ kilichochapwa Marekani kilipoingia nchini mwaka wa 2010 kilichimbua mengi ambayo yalikuwa ya siri kwa takriban nusu karne.

Ninayoandika hapa ni mazungumzo yangu na Mzee Hassan Moyo ambayo nilifanyanae nyumbani kwake Fuoni Zanzibar jioni moja mwaka wa 2012.

Nakumbuka kama jana vile mazungumzo yale pale nilipoanza mazungumzo yetu kwa kumgusia moja ya siri kubwa za Zanzibar ambazo hazikupata kuvuja kwa musa mrefu hadi Dr. Ghassany alipoeleza historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ndani ya kitabu chake.

Nilianza kwa kumweleza Mzee Moyo kuwa ninazo taarifa zake kuwa baada ya mauaji ya Karume mwaka wa 1972 Baraza la Mapinduzi lilikutana ndani ya kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya mkutano kuchagua rais wa kushika nafasi ya Mzee Karume.

Nikamwambia kuwa ingawa taarifa hizi zipo ndani ya kitabu na kwa hiyo si siri tena ana khiyari ya kulikalia kimya swali langu au akipenda anijibu.

Nikamweleza Mzee Moyo kuwa hapo niliposoma taarifa hizo ndani ya kitabu jina la mtoa taarifa halikuwekwa na mimi ingawa nafahamiana na mwandishi kwa kule kufanya staha sikumuuliza Dr. Ghassany chanzo cha taarifa zile zake lau kama Daktari akinichukua mimi kama msaidizi wake wa karibu katika utafiti wa kitabu kile.

Mzee Moyo akaniambia angependa awe kimya katika swali hilo.

Mzee Moyo hakuwa mgeni kwangu alikuwa ni mzee wangu na nimeishi jirani ya nyumba yake Tanga na nikimtembelea kwake na wakati mwingine akiniita kwake ikiwa ana utumwa wowote kwangu kwa hiyo tulikuwa tunafahamiana vyema.
Nilisisitiza anijibu na nikampa sababu zangu.

Nilimwammbia nataka anijibu swali lile ili niijue nafasi yake katika historia ya Zanzibar.

Mzee Moyo akawa ananisikiliza kimya huku akinitazama kama vile ana kitu anakiwaza.

Mzee Moyo alianza kujibu swali langu kuanzia siku mzee Karume alipouawa Kisiwandui akiwa na marafiki zake Thabit Kombo, Mtoro Rehani na watu wengine.

Mzee Moyo anasema siku ile ya mauaji ya Mzee Karume alifika hospitali ya Mapinduzi Kongwe kwa matibabu ya mwanae wa kike Zainab ambae aligongwa na nyoka hana hili wala lile kuwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Karume ameuawa muda mfupi uliopita na maiti yake imehifadhiwa pale hospitali.

Lakini Mzee Moyo anasema wakati yuko njiani anaendesha gari kuja mjini kumleta mwanae hospitali aliona hali ambayo haikuwa ya kawaida kwani barabara ilikuwa shwari kuliko kawaida na kote kimya hata chembelecho kunguru hawaruki.

Sasa wakati anaingia hospitali ndipo akamwona Mzee Thabit Kombo amelazwa kwenye machela inasukumwa huku pembeni kuna kijana Afisa Usalama wa Taifa ambae yeye akimfahamu ameshika, ‘’machine gun,’’ anamsindikiza.

Mzee Moyo akawa anamwita Thabit Kombo kwa jina lakini hakuitika.

Mpaka hapo hakuna aliyemweleza nini kimetokea au kuna nini pale hospitali hadi alipopanda juu hospitali anaingia kwenye chumba kimoja ndiyo anamkuta Mzee Karume kalazwa kwenye kitanda na madaktari wawili, Dr. Mahfoudh na Dr. Hassan wanajaribu kumsaidia.

Mzee Karume hakuamka na kipindi hicho baadhi ya wajumbe wa Baraza la Mpinduzi walikuwa wameshafika pale hospitali.

Pamoja wakachukua maiti ya Mzee Karume kuipeleka Ikulu.

Mzee Moyo anasema wakaamua usiku ule ule kifanyike kikao cha Baraza la Mapinduzi kuchagua Rais mpya wa Zanzibar.

Kikao hiki kikafanyika Makao Makuu ya JWTZ na Mwenyekiti wa kikao kile alikuwa Mzee Aboud Jumbe ambae alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais.

Said Washoto yeye ndiye alitaja jina la Hassan Moyo awe mrithi wa Karume.

‘’Huyu Mngoni mtani wangu anafaa,’’ Said Washoto alisema, Mzee Moyo anahadithia.

Yusuf Himidi yeye akasema kuwa itafaa Aboud Jumbe achukue nafasi ile na Nassor Moyo awe Waziri wa Nchi na Katibu wa Mipango wa ASP nafasi alizokuwanazo Aboud Jumbe.

Mzee Moyo akaniambia kuwa hivi ndivyo ilivyokuwa jinsi Baraza la Mapinduzi lilivyoweza kuhamisha madaraka katika hali ya utulivu bila mvutano wowote.

Historia hii ingelibaki kuwa siri na pengine hii historia isingejulikana kabisa kama Dr. Ghassany asingeeleza katika kitabu chake kuwa jina la Hassan Nassor Moyo lilipendekezwa katika uteuzi wa kushika nafasi ya urais wa Zanzibar baada ya kifo cha Mzee Karume mwaka wa 1972.

Katika historia hii kuna mengi ya kuzingatiwa katika kuyafahanu mapinduzi na historia nzima ya Zanzibar.

Dr. Ghassany kalamu yake ni chokonozi sana.

Dr. Ghassany ingelitosha akasimama hapo na historia ya Mzee Moyo ika wa imefika tamati.

Daktari hakufanya hivyo aliendelea katika kitabu chake kueleza kuwa Hassan Nassor Moyo kuwa alipendekezwa kuwa Waziri Kiongozi lakini Said Abdallah Natepe akatoa fikra kuwa nafasi hiyo bora apewe Seif Sharif Hamad kwa kuwa anatoka Pemba.

Ikawa kwa mara ya pili nafasi kubwa juu kabisa katika utawala wa Zanzibar ikampitia kwa mbali.

Mzee Hassan Moyo alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa Vijana wa ASP mwaka wa 1960 na anaeleza kuwa ni Mzee Karume aliyemchagua yeye aanzishe umoja huo ili kuweka uwiano mzuri katika siasa za kudai uhuru wa Zanzibar kutokana na kuwa kulikuwa na chama cha vijana maarufu kwa jina la Young Africans Socialist Union (YASU).

Chama hiki kilijumuisha vijana waliokuwa kwa nyakati zile wakijiona wao wameelimika na walijitahidi kadri ya uwezo wao kuweka mizania sawa baina ya siasa za ZNP na ASP lakini Mzee Karume alichelea kuwa YASU ilikuwa wepesi kuchepukia wakaruka mfereji wakaenda Hizbu kuliko kubakia katikati au kuja ASP.

Kwa ajili hii Mzee Karume asubuhi moja akamwendea Hassan Nassor Moyo ofisni kwake Miembeni wakati ule Mzee Moyo alikuwa katika vyama vya wafanyakazi pamoja na Ahmed Hassan Diria kumtaka awakusanye wenzake waanzishe umoja wao wa vijana wa ASP.

Siku ile Karume alikuwa amealikwa chai ya jioni na YASU na dhifa ile ilikuwa nyumbani kwa Othman Shariff na mzee

Katika mazungumzo kijana mmoja wa YASU akamuuliza Mzee Karume swali akamwambia vipi yeye anadai uhuru ilhali watu wake elimu hata chembe?

Kwa utulivu mkubwa Karume akajibu yeye hapiganii uhuru wa elimu bali nchi yake iwe huru na akaendelea akimwonyesha kidole Othman Shariff na kusema, ‘’Huyu hapa mkubwa wenu Othman Shariff kasoma na kazi yake ni kupiga ng’ombe sindano.’’

Vijana waliangua kicheko na Karume akaita chai iletwe wanywe, wakanywa chai na kutawanyika.

Siku ya pili akamuendea tena Nassor Moyo kumtia hima aitishe mkutano haraka wa kuunda ASP Youth League.

Mzee Moyo akawatafuta vijana wenzake, Abdallah Said Natepe, Seif Bakari, Khadija Jabi na vijana wengine wakafanya mkutano kwenye mkahawa wa Abbas Hussein Kijangwani na mpiga upatu wa ASP ndiye aliyetembea nchi nzima kuutangaza mkutano ule.
Siku ya mkutano mgahawa ulifurika hadi nje na ASP Youth League ikaanza na nguvu kubwa sana.

Nayakumbuka mazungumzo yangu haya na Mzee Moyo kama vile ni jana tuko barazani kwake Fuoni tumezungukwa na bustani nzuri ya kupendeza Mzee Moyo akichukua kila fursa kunichekesha nami nikimlipa kwa kumwambia, ‘’Mzee Moyo nimeona picha zako za ujana ulikuwa na sura jamil sana.’’

Hapa Mzee Moyo inakuwa zamu yake ya kuangua kicheko.

Yakaja mapinduzi mwaka wa 1964 na Mzee Moyo kayaona yote kwa macho yake na akawa katika Baraza la Mapinduzi.

Mzee Moyo lau kama asili yake ni Songea Tanganyika na hafichi kuwa yeye ni Mngoni, aliipenda sana Zanzibar na pengine mapenzi haya ya kuipenda Zanzibar zaidi kuliko maslahi mengine ndiyo yaliyosababisha yeye kuchukiwa na baadhi ya viongozi wa CCM na kupelekea kufukazwa chama.

Mzee Moyo siku moja mbele ya Samuel Sita aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania alighadhibia pale alipoambiwa asihoji muungano.

Kwa hasira alitoa nyaraka akaziweka juu ya meza akasame huu hapa muungano na una mambo kumi na moja tu.

Mzee Moyo akimtazama Sitta bila ya kupepesa akasema, ‘’Huu utumbo,’’ bila shaka akifanya rejea kwa vipengele vingi vilivyokuja kuongezwa baada ya muungano.

Nilipomshikilia kutaka kujua zaidi Mzee Moyo akasema kuwa wale waliokuja kuhoji mambo ya muungano walikuwa wa wanawaletea Wazanzibari, ‘’upuuzi.’’

Mzee Moyo alikuwa amekanyaga vidole vya baadhi ya wana ASP wenzake ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwani lugha ya kuhoji muungano haikuwa lugha wanayopenda wao kuisikia.

Hassan Nassor Moyo kijana wa Mzee Karume alikwenda mbali zaidi kuwa kusema haoni yeye vibaya kuwa hakuwa katika Kamati ya Watu 14 kwani si kitu cha mtu kujivuia.

Yale yaliyokuja baada ya hapa hakuna aliyeyategemea.

Mzee Moyo akafukuzwa CCM.

Kitu gani kilifanya Mzee Hassan Nassor Moyo afukuzwe CCM ilhal yeye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano baina ya CCM na CUF mazungumzo yaliyoleta utulivu Zanzibar?

Hili lilikuwa jambo lililokuwa linatakiwa na kuombwa katika kila dua ya Mzanzibari.

Mzee Moyo alikuwa Mwenyekiti wa mpango wa udhamini wa wanafunzi wa Zanzibar kutoka Serikali ya Oman, udhamini ambao serikali ya Oman ilijitoea kuwasomesha vijana wa Kizanzibari katika vyuo vikubwa duniani kwa gharama yoyote.

Hii ilikuwa ndoto ya kila kijana wa Kizanzibari kuwa ndugu zao walikuwa wamefungua hazina yao kuwasomesha ndugu zao Zanzibar katika vyuo vikubwa vyenye sifa ulimwenguni.

Msaada huu mkubwa kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar hakufika mbali umekufa na kila unaemuuliza kimetokea nini hana jibu.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyotokea baada ya maridhiano baiana ya CCM na CUF pia imekufa kama zilivyokuwa scholarship za Serikali ya Oman ambazo Mwenyekiti wake na aliyezipokea pale State University of Zanzibar (SUZA) alikuwa marehemu Mzee Hassan Moyo.

Mzee Moyo katuacha wakati Zanzibar inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu na hakuna asiyejua nini hutokea katika chaguzi za Zanzibar.

Laiti mariadhiano yangekuwapo Zanzibar wengi wangelala usingizi usio na lepe ya hofu na mashaka kila wanapofikiria Uchaguzi wa Zanzibar.

Mzee wetu Hassan Nassor Moyo aliipenda Zanzibar na aliwapenda Wazanzibari na aliipenda amani amani ya Zanzibar na maendeleo yake akijua kuwa ufungua wa maendeleo ya Zanzibar ni kuwapo na amani ya kudumu na maelewano baina ya raia wake wote bila ya ubaguzi.

Tunamwomba Allah amghufurie mzee wetu madhambi yake na amtie peponi.

Amin.

Picha: Hassan Nassor Moyo katika ujana wake wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar, picha ya pili akiwa SUZA baada ya kupokea ''scholarship,'' za Serikali ya Oman kwa Zanzibar pembeni yake ni Dr. Harith Ghassany, akiwa na mwandishi na picha ya mwisho akisoma kitabu cha Dr. Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''
IMG-20200818-WA0040.jpg
IMG-20200818-WA0041.jpg
IMG-20200818-WA0039.jpg
IMG-20200818-WA0038.jpg
 
Hassan Nassor Moyo pamoja na Karume inamaana hawakuwa na asili ya Unguja. Karume Malawi na Moyo Songea. Mwinyi pwani mkuranga. Ndio maana ccm inawaendesha.
 
HASSAN NASSOR MOYO RAIS WA ZANZIBAR NA WAZIRI KIONGOZI AMBAE HAKUWA INGAWA ALITAJWA

Kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ kilichochapwa Marekani kilipoingia nchini mwaka wa 2010 kilichimbua mengi ambayo yalikuwa ya siri kwa takriban nusu karne.

Ninayoandika hapa ni mazungumzo yangu na Mzee Hassan Moyo ambayo nilifanyanae nyumbani kwake Fuoni Zanzibar jioni moja mwaka wa 2012.

Nakumbuka kama jana vile mazungumzo yale pale nilipoanza mazungumzo yetu kwa kumgusia moja ya siri kubwa za Zanzibar ambazo hazikupata kuvuja kwa musa mrefu hadi Dr. Ghassany alipoeleza historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ndani ya kitabu chake.

Nilianza kwa kumweleza Mzee Moyo kuwa ninazo taarifa zake kuwa baada ya mauaji ya Karume mwaka wa 1972 Baraza la Mapinduzi lilikutana ndani ya kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kufanya mkutano kuchagua rais wa kushika nafasi ya Mzee Karume.

Nikamwambia kuwa ingawa taarifa hizi zipo ndani ya kitabu na kwa hiyo si siri tena ana khiyari ya kulikalia kimya swali langu au akipenda anijibu.

Nikamweleza Mzee Moyo kuwa hapo niliposoma taarifa hizo ndani ya kitabu jina la mtoa taarifa halikuwekwa na mimi ingawa nafahamiana na mwandishi kwa kule kufanya staha sikumuuliza Dr. Ghassany chanzo cha taarifa zile zake lau kama Daktari akinichukua mimi kama msaidizi wake wa karibu katika utafiti wa kitabu kile.

Mzee Moyo akaniambia angependa awe kimya katika swali hilo.

Mzee Moyo hakuwa mgeni kwangu alikuwa ni mzee wangu na nimeishi jirani ya nyumba yake Tanga na nikimtembelea kwake na wakati mwingine akiniita kwake ikiwa ana utumwa wowote kwangu kwa hiyo tulikuwa tunafahamiana vyema.
Nilisisitiza anijibu na nikampa sababu zangu.

Nilimwammbia nataka anijibu swali lile ili niijue nafasi yake katika historia ya Zanzibar.

Mzee Moyo akawa ananisikiliza kimya huku akinitazama kama vile ana kitu anakiwaza.

Mzee Moyo alianza kujibu swali langu kuanzia siku mzee Karume alipouawa Kisiwandui akiwa na marafiki zake Thabit Kombo, Mtoro Rehani na watu wengine.

Mzee Moyo anasema siku ile ya mauaji ya Mzee Karume alifika hospitali ya Mapinduzi Kongwe kwa matibabu ya mwanae wa kike Zainab ambae aligongwa na nyoka hana hili wala lile kuwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Karume ameuawa muda mfupi uliopita na maiti yake imehifadhiwa pale hospitali.

Lakini Mzee Moyo anasema wakati yuko njiani anaendesha gari kuja mjini kumleta mwanae hospitali aliona hali ambayo haikuwa ya kawaida kwani barabara ilikuwa shwari kuliko kawaida na kote kimya hata chembelecho kunguru hawaruki.

Sasa wakati anaingia hospitali ndipo akamwona Mzee Thabit Kombo amelazwa kwenye machela inasukumwa huku pembeni kuna kijana Afisa Usalama wa Taifa ambae yeye akimfahamu ameshika, ‘’machine gun,’’ anamsindikiza.

Mzee Moyo akawa anamwita Thabit Kombo kwa jina lakini hakuitika.

Mpaka hapo hakuna aliyemweleza nini kimetokea au kuna nini pale hospitali hadi alipopanda juu hospitali anaingia kwenye chumba kimoja ndiyo anamkuta Mzee Karume kalazwa kwenye kitanda na madaktari wawili, Dr. Mahfoudh na Dr. Hassan wanajaribu kumsaidia.

Mzee Karume hakuamka na kipindi hicho baadhi ya wajumbe wa Baraza la Mpinduzi walikuwa wameshafika pale hospitali.

Pamoja wakachukua maiti ya Mzee Karume kuipeleka Ikulu.

Mzee Moyo anasema wakaamua usiku ule ule kifanyike kikao cha Baraza la Mapinduzi kuchagua Rais mpya wa Zanzibar.

Kikao hiki kikafanyika Makao Makuu ya JWTZ na Mwenyekiti wa kikao kile alikuwa Mzee Aboud Jumbe ambae alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais.

Said Washoto yeye ndiye alitaja jina la Hassan Moyo awe mrithi wa Karume.

‘’Huyu Mngoni mtani wangu anafaa,’’ Said Washoto alisema, Mzee Moyo anahadithia.

Yusuf Himidi yeye akasema kuwa itafaa Aboud Jumbe achukue nafasi ile na Nassor Moyo awe Waziri wa Nchi na Katibu wa Mipango wa ASP nafasi alizokuwanazo Aboud Jumbe.

Mzee Moyo akaniambia kuwa hivi ndivyo ilivyokuwa jinsi Baraza la Mapinduzi lilivyoweza kuhamisha madaraka katika hali ya utulivu bila mvutano wowote.

Historia hii ingelibaki kuwa siri na pengine hii historia isingejulikana kabisa kama Dr. Ghassany asingeeleza katika kitabu chake kuwa jina la Hassan Nassor Moyo lilipendekezwa katika uteuzi wa kushika nafasi ya urais wa Zanzibar baada ya kifo cha Mzee Karume mwaka wa 1972.

Katika historia hii kuna mengi ya kuzingatiwa katika kuyafahanu mapinduzi na historia nzima ya Zanzibar.

Dr. Ghassany kalamu yake ni chokonozi sana.

Dr. Ghassany ingelitosha akasimama hapo na historia ya Mzee Moyo ika wa imefika tamati.

Daktari hakufanya hivyo aliendelea katika kitabu chake kueleza kuwa Hassan Nassor Moyo kuwa alipendekezwa kuwa Waziri Kiongozi lakini Said Abdallah Natepe akatoa fikra kuwa nafasi hiyo bora apewe Seif Sharif Hamad kwa kuwa anatoka Pemba.

Ikawa kwa mara ya pili nafasi kubwa juu kabisa katika utawala wa Zanzibar ikampitia kwa mbali.

Mzee Hassan Moyo alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Umoja wa Vijana wa ASP mwaka wa 1960 na anaeleza kuwa ni Mzee Karume aliyemchagua yeye aanzishe umoja huo ili kuweka uwiano mzuri katika siasa za kudai uhuru wa Zanzibar kutokana na kuwa kulikuwa na chama cha vijana maarufu kwa jina la Young Africans Social Union (YASU).

Chama hiki kilijumuisha vijana waliokuwa kwa nyakati zile wakijiona wao wameelimika na walijitahidi kadri ya uwezo wao kuweka mizania sawa baina ya siasa za ZNP na ASP lakini Mzee Karume alichelea kuwa YASU ilikuwa wepesi kuchepukia wakaruka mfereji wakaenda Hizbu kuliko kubakia katikati au kuja ASP.

Kwa ajili hii Mzee Karume asubuhi moja akamwendea Hassan Nassor Moyo ofisni kwake Miembeni wakati ule Mzee Moyo alikuwa katika vyama vya wafanyakazi pamoja na Ahmed Hassan Diria kumtaka awakusanye wenzake waanzishe umoja wao wa vijana wa ASP.

Siku ile Karume alikuwa amealikwa chai ya jioni na YASU na dhifa ile ilikuwa nyumbani kwa Othman Shariff na mzee

Katika mazungumzo kijana mmoja wa YASU akamuuliza Mzee Karume swali akamwambia vipi yeye anadai uhuru ilhali watu wake elimu hata chembe?

Kwa utulivu mkubwa Karume akajibu yeye hapiganii uhuru wa elimu bali nchi yake iwe huru na akaendelea akimwonyesha kidole Othman Shariff na kusema, ‘’Huyu hapa mkubwa wenu Othman Shariff kasoma na kazi yake ni kupiga ng’ombe sindano.’’

Vijana waliangua kicheko na Karume akaita chai iletwe wanywe, wakanywa chai na kutawanyika.

Siku ya pili akamuendea tena Nassor Moyo kumtia hima aitishe mkutano haraka wa kuunda ASP Youth League.

Mzee Moyo akawatafuta vijana wenzake, Abdallah Said Natepe, Seif Bakari, Khadija Jabi na vijana wengine wakafanya mkutano kwenye mkahawa wa Abbas Hussein Kijangwani na mpiga upatu wa ASP ndiye aliyetembea nchi nzima kuutangaza mkutano ule.

Siku ya mkutano mgahawa ulifurika hadi nje na ASP Youth League ikaanza na nguvu kubwa sana.

Nayakumbuka mazungumzo yangu haya na Mzee Moyo kama vile ni jana tuko barazani kwake Fuoni tumezungukwa na bustani nzuri ya kupendeza Mzee Moyo akichukua kila fursa kunichekesha nami nikimlipa kwa kumwambia, ‘’Mzee Moyo nimeona picha zako za ujana ulikuwa na sura jamil sana.’’

Hapa Mzee Moyo inakuwa zamu yake ya kuangua kicheko.

Yakaja mapinduzi mwaka wa 1964 na Mzee Moyo kayaona yote kwa macho yake na akawa katika Baraza la Mapinduzi.

Mzee Moyo lau kama asili yake ni Songea Tanganyika na hafichi kuwa yeye ni Mngoni, aliipenda sana Zanzibar na pengine mapenzi haya ya kuipenda Zanzibar zaidi kuliko maslahi mengine ndiyo yaliyosababisha yeye kuchukiwa na baadhi ya viongozi wa CCM na kupelekea kufukazwa chama.

Mzee Moyo siku moja mbele ya Samuel Sita aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania alighadhibia pale alipoambiwa asihoji muungano.

Kwa hasira alitoa nyaraka akaziweka juu ya meza akasame huu hapa muungano na una mambo kumi na moja tu.

Mzee Moyo akimtazama Sitta bila ya kupepesa akasema, ‘’Huu utumbo,’’ bila shaka akifanya rejea kwa vipengele vingi vilivyokuja kuongezwa baada ya muungano.

Nilipomshikilia kutaka kujua zaidi Mzee Moyo akasema kuwa wale waliokuja kuhoji mambo ya muungano walikuwa wa wanawaletea Wazanzibari, ‘’upuuzi.’’

Mzee Moyo alikuwa amekanyaga vidole vya baadhi ya wana ASP wenzake ndani ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwani lugha ya kuhoji muungano haikuwa lugha wanayopenda wao kuisikia.

Hassan Nassor Moyo kijana wa Mzee Karume alikwenda mbali zaidi kuwa kusema haoni yeye vibaya kuwa hakuwa katika Kamati ya Watu 14 kwani si kitu cha mtu kujivuia.

Yale yaliyokuja baada ya hapa hakuna aliyeyategemea.

Mzee Moyo akafukuzwa CCM.

Kitu gani kilifanya Mzee Hassan Nassor Moyo afukuzwe CCM ilhal yeye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano baina ya CCM na CUF mazungumzo yaliyoleta utulivu Zanzibar?

Hili lilikuwa jambo lililokuwa linatakiwa na kuombwa katika kila dua ya Mzanzibari.

Mzee Moyo alikuwa Mwenyekiti wa mpango wa udhamini wa wanafunzi wa Zanzibar kutoka Serikali ya Oman, udhamini ambao serikali ya Oman ilijitoea kuwasomesha vijana wa Kizanzibari katika vyuo vikubwa duniani kwa gharama yoyote.

Hii ilikuwa ndoto ya kila kijana wa Kizanzibari kuwa ndugu zao walikuwa wamefungua hazina yao kuwasomesha ndugu zao Zanzibar katika vyuo vikubwa vyenye sifa ulimwenguni.

Msaada huu mkubwa kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar hakufika mbali umekufa na kila unaemuuliza kimetokea nini hana jibu.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa iliyotokea baada ya maridhiano baiana ya CCM na CUF pia imekufa kama zilivyokuwa scholarship za Serikali ya Oman ambazo Mwenyekiti wake na aliyezipokea pale State University of Zanzibar (SUZA) alikuwa marehemu Mzee Hassan Moyo.

Mzee Moyo katuacha wakati Zanzibar inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu na hakuna asiyejua nini hutokea katika chaguzi za Zanzibar.

Laiti mariadhiano yangekuwapo Zanzibar wengi wangelala usingizi usio na lepe ya hofu na mashaka kila wanapofikiria Uchaguzi wa Zanzibar.

Mzee wetu Hassan Nassor Moyo aliipenda Zanzibar na aliwapenda Wazanzibari na aliipenda amani amani ya Zanzibar na maendeleo yake akijua kuwa ufungua wa maendeleo ya Zanzibar ni kuwapo na amani ya kudumu na maelewano baina ya raia wake wote bila ya ubaguzi.

Tunamwomba Allah amghufurie mzee wetu madhambi yake na amtie peponi.

Amin.

Picha: Hassan Nassor Moyo katika ujana wake wakati wa kupigania uhuru wa Zanzibar, picha ya pili akiwa SUZA baada ya kupokea ''scholarship,'' za Serikali ya Oman kwa Zanzibar pembeni yake ni Dr. Harith Ghassany, akiwa na mwandishi na picha ya mwisho akisoma kitabu cha Dr. Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''

View attachment 1541251View attachment 1541252View attachment 1541253View attachment 1541254
 
Back
Top Bottom