Hassan Hassanoo au ‘Mpiganaji’ mbaroni Dar kwa Wizi...

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797



Na Dina Ismail


ALIYEWAHI kuwa Katibu wa Klabu ya Simba na Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA), Hassan Othman ‘Hasanoo’ anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni kwa tuhuma za wizi wa madini ya shaba.


Hasanoo alitiwa mbaroni na polisi jijini Dar es Salaam tangu juzi na hadi jana bado alikuwa anaendelea kushikiliwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay.

Akithibitisha kukamatwa kwa ‘Hasanoo’, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema shaba hiyo tani 26 yenye thamani ya sh milioni 400 ilikuwa ikisafirishwa kutoka Zambia kuja jijini Dar es Salaam.


Kamanda Wambura alisema shaba hiyo ilikuwa ikipelekwa bandarini na katika tukio hilo wamewakamata watu wanne akiwamo Hasanoo na wanaendelea kuwahoji kuhusiana na tukio hilo pamoja na mengine ya wizi wa shaba.


Kamanda huyo aliongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea na panapo majaliwa watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani kesho.


Hasanoo au ‘Mpiganaji’ ni mdau wa soka wa muda mrefu, ambapo amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika klabu ya Simba, ikiwamo Katibu Msaidizi, Katibu Mkuu na mjumbe wa kamati mbalimbali za klabu hiyo.

 
Back
Top Bottom