Hassan Aziz akamatwa na madawa ya kulevya 1kg

Vita kama vita ilikuwa mzuri sana, tena sana lakini alivyokuwa ameiendesha, haikuwa sahihi hata kidogo!

Haikuwa sahihi kwa sababu sio tu ilitoa uwezekano wa ku-expose watu kwamba wanauza dawa za kulevya wakati wengine sio kweli bali pia ilikuwa inatoa mwanya wa kuficha ushahidi!!

Kwa mfano, staili yake ilikuwa ni kutaja watu hadharani na kuwaambia "...kesho kutwa nenda karipoti Central"! Halafu hiyo kesho kutwa mtu akienda kuripoti, eti ndipo askari wanafuatana nae kwenda kupekua nyumbani!

Ni mpumbavu gani duniani angeendelea kuacha ushahidi ndani pamoja na kujua kwamba hatimae polisi watabisha hodi?

Ni kutokana na ujinga wake huu ndio maana wale ambao walionekana ni barons hawakukutwa na kitu! Na hii ndio sababu kuu ambayo ilinifanya nipinge operesheni ile ya Makonda... kwa sababu haikuonesha nia thabiti ya kuwatia nguvuni Drug Lords!
Omba kukosa vyote ila siyo akili,Bashite aliepwa kichwa kikubwa alinyimwa akili,
 
Back
Top Bottom