Hassan Aziz akamatwa na madawa ya kulevya 1kg

Nuraty J

JF-Expert Member
Sep 18, 2018
1,729
3,829
Kuna kijana anaitwa Mfungeni Aziz alikamatwaga mwaka Jana na madawa ya kulevya yupo segerea,
Juzi tena amekamatwa kaka Yake anaitwa Hassan Aziz, amekamatwa na unga kg 1, wote wakazi wa ununio,

MAKONDA ana mabaya Yake ila yeye ndo muanzilishi wa hii oparesheni inayoendelea ya madawa ya kulevya, miaka mitatu ijayo unga utaisha kabisa Tanzania, ukitaka kujua unga haufai uwe na nduguyo anatumia unga, ni hatari
 
Na hapa uzi tayari.
Mkuu wangu,
madawa ya unga hayawezi kuisha eti kisa Aziz amekamatwa na kilo moja huko ununio.
Huyo ni sawa na mmoja ndani ya milion,
Kuna watu hiyo ndiyo kazi yao na haukuti hata siku moja eti amesumbuliwa na huyo makonda au yeyote.
Akikamatwa mmoja haimaanishi eti ndiyo biashara inaenda kuisha.
 
ila hao pia ni wauzaji wakubwa
 
Vita kama vita ilikuwa mzuri sana, tena sana lakini alivyokuwa ameiendesha, haikuwa sahihi hata kidogo!

Haikuwa sahihi kwa sababu sio tu ilitoa uwezekano wa ku-expose watu kwamba wanauza dawa za kulevya wakati wengine sio kweli bali pia ilikuwa inatoa mwanya wa kuficha ushahidi!!

Kwa mfano, staili yake ilikuwa ni kutaja watu hadharani na kuwaambia "...kesho kutwa nenda karipoti Central"! Halafu hiyo kesho kutwa mtu akienda kuripoti, eti ndipo askari wanafuatana nae kwenda kupekua nyumbani!

Ni mpumbavu gani duniani angeendelea kuacha ushahidi ndani pamoja na kujua kwamba hatimae polisi watabisha hodi?

Ni kutokana na ujinga wake huu ndio maana wale ambao walionekana ni barons hawakukutwa na kitu! Na hii ndio sababu kuu ambayo ilinifanya nipinge operesheni ile ya Makonda... kwa sababu haikuonesha nia thabiti ya kuwatia nguvuni Drug Lords!
 
Drug lord kina Kiboko, Mfungeni azizi , Hassan aziz, Hussein pambakali, etc ,mbona wengi wapo jela, ila makonda ndo muanzilishi, wenye kazi yao wakaioboresha,
Unajua sasaivi kuna kikosi kazi kipo chini ya office ya rais cha kupambana na drugs, hao wakimkamata muuza unga hata kama atatangaza kuonga billion awapokei,
Mzee kiboko alitaka kuwapa milioni mia nne wakakataa, wakamuambia huna ela Ya kutuonga, wakamtolea madola ambayo ambayo ni maalum kwa kuwanasa wauzaji ikibidi kujifanya wanunuzi
 
Kuwa Kiongozi katika Nchi hii kunahitaji mambo mengi sana ikiwemo Majungu,fitna,husda,uongo,ushirikina nk nk ukiondoa uwezo binafsi wa mtu alionao kuwa kiongozi..hii inasababisha wakati mwingine kukosa viongozi wazuri wenye maono na fikra za kuipeleka mbele nchi yetu..

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Chakwale
Mungu Ibariki Morogoro
 
Drug lord kina Kiboko, Mfungeni azizi , Hassan aziz, Hussein pambakali, etc ,mbona wengi wapo jela, ila makonda ndo muanzilishi, wenye kazi yao wakaioboresha,
Unajua sasaivi kuna kikosi kazi kipo chini ya office ya rais cha kupambana na drugs, hao wakimkamata muuza unga hata kama atatangaza kuonga billion awapokei,
Mzee kiboko alitaka kuwapa milioni mia nne wakakataa, wakamuambia huna ela Ya kutuonga, wakamtolea madola ambayo ambayo ni maalum kwa kuwanasa wauzaji ikibidi kujifanya wanunuzi
Hiki Kikosi Kazi kipo tangia enzi za JK sema kilikuwa hakifahamiki kwa sababu staili yao ilikuwa tofauti na ile ya Makonda iliyofanya ndo ioneshe mapambano rasmi dhidi ya wauza unga!

Ngoja nikukumbushe!

Unakumbuka ile Orodha ya Wauza Unga enzi za JK ambayo JK akawa anashambuliwa sana kwamba amewagwaya wauza unga?!

Ile orodha ilijaa Punda na sio Drug Barons wenyewe!! Sasa baada ya kutolewa ile orodha, ndipo ikaundwa hiyo Task Force!

Hii Task Force ilianza kula sahani moja na wale waliokuwa wametajwa ambao wengi wao walikuwa Punda tu! Hata hivyo, baadae wakagundua wana-deal na matawi na sio mashina!

Wakabadilisha style... badala ya ku-deal na Punda wakaanza ku-deal na wenyewe kimya kimya!! Ndo vile tu vita yenyewe haikuwa inaendeshwa kwa mbwembwe sana but am telling you, Drug Barons walikamatwa enzi za JK na sio sasa, sema hapakuwa na kelele!!

Chukulia yule Mchungaji Fake wa Nigeria anayefahamika kwa jina la Chid Okechukwi! Nimejaribu ku-Google lakini nimeshangaa kutoona taarifa zake kutoka kwenye serious media, lakini angalau Global Publishers waliripoti!
Mchungaji kutoka Nigeria, Chid Okechukwi aliyekamatwa na kikosi kazi (task force) cha kudhibiti na kupambana na madawa ya kulevya nchini akiwa na kilo 81 za madawa ya kulevya aina ya cocaine amehukumiwa kwenda jela miaka 30 na faini ya shilingi bilioni tisa akitoka mwaka 2045.

Mchungaji Okechukwi wa kanisa moja la kiroho nchi humo alikamatwa Machi 12, 2013 maeneo ya Kunduchi jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akiishi.
Kama unavyoona, badala ya kubadili strategy, huyo jamaa akadakwa na Kilo 81!

Sidhani kama kuna mtu kwa sasa aliyedakwa na mzigo mkubwa kama huo!! Na pamoja na huyo Okechukwi, pia habari imemtaja Fred Chonde ambae nae alikamatwa wakati mwingine na alihumiwa miaka 20!

Tukiacha hao, nadhani wengi tunamkumbuka Morine Lyumba, Binti wa Amatus Lyumba ambae mwaka 2012 alikamatwa Lindi na zaidi ya Kilo 200 ya dawa za kulevya!!

Kama hiyo habari ilikupita, Google tu "Morine Lyumba Dawa za Kulevya"! Huyu habari zake zilitangazwa sana kutokana na umaarufu wa baba yake!!

Kukamatwa kwa Morine kukapelekea kukamatwa kwa Kubwa la Maadui, Shikuba mwaka 2014!! Shikuba alikuwa pia anatafutwa Marekani!

Baada ya kuchomoka US, akakimbilia Tanzania! Baada ya kuona TZ hapasomeki, akakimbilia South Africa lakini ambacho hakufahamu ni kwamba alikuwa anafuatiliwa kila hatua anayopiga kimya kimya.

Akachomoka tena South Africa akataka kurudi Dar bila kufahamu kwamba alikuwa bado anafuatiliwa kimya kimya... na alipogusa mguu tu airport Dar es salaam, akadakwa!

Achana na hizo gunia mbili za dawa za kulevya alizokuwa amekamatwa nazo Moreen mwaka 2012, lakini Kituo cha Habari cha UN Dar es salaam mwaka 2016 kilitoa ripoti kuhusu mihadarati, na sehemu ya taarifa yake ilisema:-
Katika miezi minane ya mwaka 2014, vyombo vya dola vilikamata zaidi ya kilo 321 za heroin, kiasi ambacho ni zaidi ya kilichokamatwa mwaka 2013. Heroin iliyokamatwa ilikuwa ikisafirishwa kutoka Afghanistan, India, Iran na Pakistan na ilikuwa ikipelekwa China, Japan, Afrika Kusini, Uturuki, Amerika na nchi za Bara Ulaya.

Hata "Millionea Mtoto" Lwitiko Adamson, ambae nadhani nae amepelekwa Marekani kuunganishwa na akina Shikuba, na mwenywe alidakwa nyumbani kwake Magomeni hata kabla Makonda hajateuliwa kuwa RC!

Lwitiko alidakwa kipindi cha Kitwanga... na kama utakumbuka, Kitwana alikuwa analalamika kwamba wanaomkalia kooni kuhusu sakata la LUGUMI ni wauza dawa za kulevya!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, sio kwamba kabla ya Makonda hapakuwapo na hiyo vita... ilikuwapo! Na hata hiyo Task Force ilianza kuundwa wakati wa JK.

Hivi sasa inaonekana kwamba ni Makonda ndie mwasisi wa hii vita kwa sababu yeye alikuja kwa mbwembwe wakati wenzake walikuwa wanafanya kimya kimya!!

Na kwa kelele zile za Makonda, there's no way mtu kama Shikuba angekamatwa! There's no way mtu kama Moreen au yule Mchungaji Fake wangekamatwa!!!

Hata hivyo, ufanisi wa sasa ingawaje sijasikia barons wa ukweli wakikamwatwa, kwa sasa wauza unga ni waoga sana ukilinganisha na kipindi cha JK! Ingawaje hata wakati wa JK hiyo vita ilikuwepo lakini ya kimya kimya, kukosekana kwa uoga wakati ule ni kwa sababu walijua kuhonga ilikuwa rahisi zaidi ukilinganisha na sasa ambapo kila mtu ni muoga!
 
Back
Top Bottom