Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Tunamshuhudia msemaji wa serikali akizunguka mikoa ya nchi hii kila mkoa akiingia kwenye redio za eneo hilo na kuinadi serikali.
Anatumia gharama kubwa za safari hizo na kujilipa posho zisizo za lazima. Per diem yake ni kubwa na wale wanaofuatana nae wanalipwa pia, madereva na watu kadhaa anaoongozana nao kwenye msurulu wake.
Tunajiuliza kwanini Abbas anazunguka kila kona kufanya kampeni za kipropaganda kunadi maendeleo anayoyaita yaliyofanywa na JPM kwa miaka mitatu?
Anajaribu kuhubiri mno JPM anachokifanya, anaweka ushawishi kwenye maendeleo, yaani kuwaambia wananchi ni nini JPM kafanya.
Hivi maendeleo ya kweli yanahitaji airtime ili tuyaone? Kwani maendeleo yanataka mtu akae studio aanze kuyataja moja mpaka la mwisho ndio tuelewe? Maendeleo ni kitu hai na halisi, hayahitaji hesabu za kikokotoo ni swala la udhihiriko halisi.
Serikali ya awamu hii imefanya vitu vibaya mpaka imeamua kujikita kua serikali Ongo kuwahitokea nchini.
Kwani kama lengo ni kuongea na redio, kwanini asingeenda kwenye redio kama Clouds na nyinginezo zenye coverage kubwa na kusemea huko huko alipo na nchi nzima ikajua.
Cha ajabu kaomba fungu la kuzunguka nchi nzima akaongee na redio za mikoani ambazo hata coverage zake ni hafifu. Kikubwa alipwe mamilioni ya safari.
Abbas hakuna cha maana kimefanywa na serikali hii hasa kwa kuyagusa maisha ya mtu masikini moja kwa moja. Zaidi ya kuzindua majengo na madaraja, ile hali watu wanakosa kula wanakosa kusomesha watoto wao elimu za juu na elimu za uhakika.
Watu wanakosa kazi na haki kua ngumu, watu wanakandamizwa na kodi za TRA mpaka wanaamua kufunga biashara kila siku.
Hebu achaneni na siasa za North Korea za kipuuzi, mje na akili za kuiendeleza nchi sio kujiendeleza nyie na chama chenu. Mnaingia maofisi ya umma mkiwa masikini mnatoka mkiwa matajiri wakubwa na masikini wamezidi kua kapuku wakutupwa.
Serikali inapofanya maendeleo haihitaji kupayuka payuka, kwakua maendeleo hai hayajifichi yanaonekana wazi wazi, kuanzia kwa watu mpaka kwa miji yao.