Mimi ni mtanzania kama walivyo watanzania wengine. Ila tofauti ya wengine mie naridhika na aina hii ya muungano wetu ambayo kwa kweli ni tunu ya kipekee sana.
Ni nani huyo ambaye hataki? Tunaweza kumsema hadharani hapa??na je kama hao mlioungana nao hawataki muungano.. utalazimisha..??!!
Ni nani huyo ambaye hataki? Tunaweza kumsema hadharani hapa??
Walishasema sababu za kuukataa muungano?? Au ni kama wameamka na kusema hawataki muungano?? Leo mwanao akisema hataki kwenda shule basi utamwambia lala au utafanyeje?? Ni vipi baada ya miaka 47 ndio waje waseme hawautaki muungano?? Ukivunjika muungano ndo matatizo ya Zanzibar yataisha??
Kajichome moto basi kama Boazizi ili uonesha mapenzi yako nahuo muungano, na pia utakuwa umeutetea vuzuri.Mimi nipo tayari kuutetea muungano huu hata kama itanigharimu maisha. Nawakilisha....
Wakati tukielekea katika sherehe za kuadhimisha miaka 47 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, nimeona nijotekeze hapa kwenye jamvi na kuhoji ni nani kati yetu hapa anayeweza kusimama mbele yetu na kukiri kuwa muungano wetu ni muungano si wa nchi kwa nchi bali ni muungano wa ndugu wanaopaswa kuishi pamoja. Kwa nini nasema hayupo wa kusema hayo mbele ya kadamnasi na kuwa tayari hata kufa kuutetea muungano huu?? Ni kwa sababu tumeshuhudia katika miaka ya hivi karibuni mengi yakisemwa juu ya muungano huu. Tumeshuhudia wazanzibari wakisema walibakwa na sasa wanataka talaka yao baada ya miaka 47 ya ndoa wasiyoifurahia. Na tukawasikia watanganyika wakidai kwa nini tuwabembeleze acha waende. Na vitimbi vya kila aina ya hivyo lakini sikupata kusikia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wala rais wa Zanzibar au mawaziri wao wakitoka hadharani wakisema kitu chenye kuwafanya watu waamini kuwa wana ufahamu japo kidogo kuhusu huu muungano. Tulichoambulia ni kupata msamiati mpya eti "kero za muungano". Nani kasema ndugu wanaishi bila kero ili leo kero ndio liwe jambo kubwa mnoo la kulijadili??? Nani kasema huu muungano ulilazimishwa mpaka leo ndoa ivunjwe?? Sisi hatujawa ndugu kwa sababu ya Nyerere na Karume. Siye ni ndugu tuliyeishi pamoja kabla hata neno Zanzibar wala Tanganyika hayajakuwepo kwenye ramani ya dunia hii. Hivi bado baada ya miaka yote ya wakoloni kuondoka nchini mwetu leo hii mtu ana simama na kuzungumzia mipaka iliyowekwa na wakoloni ili watutawale?? Huu ni ujuha uliopitiliza. Ndio ni ujaha maana siye hatuwezi kutengeza vya kwetu tukavienzi mpaka vya wakoloni? Kero gani zinazungumziwa miaka 15 zisizoisha???
Watanzania tuna matatizo tena makubwa. Ni kipi tunachokiweza kama hata kuuboresha undugu tuliorithi kutoka kwa babu zetu tunashindwa??
Kuna hoja eti muungano wa serikali tatu ndio suluhu ya matatizo yetu. Kwamba nchi zote duniani huwa ndivyo zinavyojiunga. Huu nao ni ujuha mwingine kwa sababu undugu wetu haufanani na undugu wa Uingereza na Ujerumani wala undugu wa Ufaransa na Italy nk. Huu ni undugu wa aina ya kipekee. Hatuwezi kutengeneza kitu cha kipekee basi mpaka tufanane na wengine??
Jamani ndugu zangu Watanzania, huu si muda wakujiuliza sisi ni ndugu ama si ndugu? Ni muda wakusema tutawajengea maisha yapi watoto na wajukuu zetu ili huu undugu wetu nao waukute na waheshimiane na kuthaminiana kama walivyokuwa babu na mababu wa babu zetu. Mimi nipo tayari kuutetea muungano huu hata kama itanigharimu maisha. Nawakilisha....
Walishasema sababu za kuukataa muungano?? Au ni kama wameamka na kusema hawataki muungano?? Leo mwanao akisema hataki kwenda shule basi utamwambia lala au utafanyeje?? Ni vipi baada ya miaka 47 ndio waje waseme hawautaki muungano?? Ukivunjika muungano ndo matatizo ya Zanzibar yataisha??
Mkuu.Walishasema sababu za kuukataa muungano?? Au ni kama wameamka na kusema hawataki muungano?? Leo mwanao akisema hataki kwenda shule basi utamwambia lala au utafanyeje?? Ni vipi baada ya miaka 47 ndio waje waseme hawautaki muungano?? Ukivunjika muungano ndo matatizo ya Zanzibar yataisha??
Anapoingia Mtawala ktk mji huufisidi, na huwafanya watu wa mji huo madhalili.Aiseeee.....watu hawautaki muungano kwa sababu hauna faida nao.......mfano mdogo tu. mtu akiwa anatoka Zanzibar na mizigo yake ya biashara antakiwa ailipie ushuru. huoni hapo kama ni kulanguliwa halafu uaitwa muungano.......hakuna kitu kama hicho ndugu yangu bora muungano uvunjike ndio tutaheshimiana. na kuwa kila mtu atakuwa na maslahi yake......isitoshe huu muungano ndio ulio hujumu maisha ya wazanzibar. Zanzibar kilikuwa kisiwa chenye nuru na utajiri mkubwa kiasi zanzibar ilikuwa inatoa misaada. leo kiko wapi? kisiwa kimekuwa kinaomba mpaka maji ya kunywaaaaaaaaaaa.....muungano hatuuu takiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
...Jamani ndugu zangu Watanzania, huu si muda wakujiuliza sisi ni ndugu ama si ndugu? Ni muda wakusema tutawajengea maisha yapi watoto na wajukuu zetu ili huu undugu wetu nao waukute na waheshimiane na kuthaminiana kama walivyokuwa babu na mababu wa babu zetu. Mimi nipo tayari kuutetea muungano huu hata kama itanigharimu maisha. Nawakilisha....
Muungano wa nini banaaaaaaaaaa!, aaaaaaaaaaagh, wewe uteetee ugharimu maisha yako, mimi wala sitaki hata kuusikia.
Etu undugu, undugu gani wa lawama na chuki, ufilie mbali tu huu mungano
wadau, hivi Tanganyika inapata faida gani kutoka zanzibar? huwa sipati jibu