Hasira za Wazanzibar kuchoshwa na Muungano

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
0
Na Awadh A. Said

MAKALA ya Tundu Lissu iliyochapishwa na gazeti hili chini ya kichwa cha habari, Muungano wa Tanzania sasa umekuwa dhaifu zaidi imenishawishi kutoa maoni kwa kuona inaelekeza watu sivyo.

Lissu, ambaye ni mwanasheria mwenzangu, anasema mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yamedhoofisha muungano wa Tanzania kwa "kumong'onyoa misingi karibu yote ya muungano huo, kubadili sura ya muungano wenyewe, mipaka yake na muundo wake." Ana khofu mabadiliko hayo "yanaweza kuwa chanzo kikuu cha kubomoka kwa Muungano na hata tishio kwa usalama wa mipaka ya Taifa."

Anaamini mabadiliko hayo yaliitangaza Zanzibar '‘kuwa nchi yenye mipaka kamili" na kwamba "Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa." Anaegemea kifungu cha kwanza cha Katiba ya Zanzibar kabla ya marekebisho, kinachosema, '‘Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Hapa kuna mambo mawili: Kwanza kuwa mabadiliko hayo ndio yaliyoitangaza Zanzibar nchi, na pili ndiyo yaliyobainisha mipaka ya Zanzibar ambayo mwanzo haikutajwa. Yote haya si kweli.

Zanzibar ilianza kuwa na katiba yake ya kwanza baada ya Mapinduzi ya 1964. Ilikuwa mwaka 1979. Baadaye ilifutwa na kuandikwa upya mwaka 1984 ilipoandikwa inayoendelea mpaka sasa. Ndiyo iliyofanyiwa marekebisho mara 10 yakiwemo haya yanayojadiliwa sasa. Je, Katiba hiyo haikutaja Zanzibar kama nchi hadi yalipokuja mabadiliko ya kumi? Ni kweli Katiba ya Zanzibar ya 1984 kabla ya marekebisho ya kumi ilieleza katika kifungu cha 1 kuwa "Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Lakini ukiwacha kifungu hicho, vifungu kadhaa au tuseme katiba yote inaitaja Zanzibar ni nchi.

(9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.
(9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …
(10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:
(10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.
(12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.
(21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI…
(23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…

Inaonyesha Lissu alitazama tu kifungu hicho cha kwanza, akapuuza vingine. Katiba ya Zanzibar imebaki na idadi ileile ya vifungu 135 hata baada ya marekebisho ya kumi.

Msingi mkuu wa katika kanuni za kutafsiri sheria, ni kuwa ili uweze kupata tafsiri sahihi kwa waraka wowote (iwe ni Katiba, Sheria, Mkataba n.k.) unapaswa kusoma waraka wote ndipo upate maana, tafsiri au dhamira inayopatikana katika waraka huo kuhusiana na jambo husika. Ni dhahiri huwezi kuchopoa kifungu kimoja tu ukapata usahihi.

Hebu tuangalie hichohicho kifungu cha kwanza kisemacho '‘Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano." Ni sawa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri Ya Muungano, lakini inasimama katika utambulisho upi? Ni sehemu kama Mkoa, Wilaya, Tarafa, Jimbo, Kata au kitongoji? Zanzibar ina katiba yake, ina Rais wake, ina Mahkama zake, ina mawaziri wake, ina Baraza lake la kutunga sheria (Baraza la Wawakilishi), ina watu wake (tena wana vitambulisho), ina bendera yake, ina wimbo wake wa Taifa, ina Mamlaka yake ya serikali za mitaa, ina magereza yake (Vyuo vya Mafunzo), ina vikosi vyake maalum vya ulinzi, ina mapato yake na bajeti yake n.k. Jee kuna Mkoa au Wilaya yenye yote hayo? Na yamekuwepo kabla ya mabadiliko yaliyofanywa.

Lissu anasema, "Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa." Kabla ya mabadiliko ya kumi, Katiba ya Zanzibar 1984, kifungu cha 2(i) kinasema:

2(i) "Eneo la Zanzibar ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar." Baada ya mabadiliko ya kumi, kifungu hicho kinaendelea kuwepo kikisema: Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar."

Hoja ya pili ya Lissu ni mabadiliko haya yanadhoofisha Muungano kwa vile yameondoa mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika mikoa kutoka mikononi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kuweka mamlaka hayo kwa Rais wa Zanzibar. Hili ni kweli limefanyika katika mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar. Tujiulize sababu. Inaeleweka wazi kuwa ni Rais wa Zanzibar ambae kipindi chote tokea Muungano wa Tanzania uasisiwe 1964, ndie anayeigawa Zanzibar katika mikoa na wilaya.

Hakuna kumbukumbu inayoonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano amewahi kuigawa Zanzibar katika Mikoa au Wilaya. Sasa kwa takriban miaka 47 mamlaka hayo yalikuwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kikatiba lakini kiutendaji na kiutekelezaji Rais wa Zanzibar ndiye aliyekuwa anatekeleza mamlaka hayo. Mabadiliko yametambua hilo na kurekebisha. Haiwezekani tukadumisha vifungu ndani ya katiba ambavyo vinaonekana ni pambo tu. Bali hili litoshe kuonesha mkanganyiko unaozikumba katiba zetu mbili.

Hoja ya tatu ya Lissu ni kuwa mabadiliko ya kumi yamepunguza mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Anasema: "Mabadiliko yamekiuka katiba kwa kuinyang'anya Mahakama ya Rufaa mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar."

Hata mara moja tangu ianzishwe, haijawahi kutokea kwa Mahkama ya Rufaa kuwa na mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahkama Kuu ya Zanzibar. Katiba ya Zanzibar iliipa mamlaka mahkama hiyo kwa baadhi ya kesi tu.

Kifungu cha 99 cha Katiba ya Zanzibar kinasema, Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania itakuwa na uwezo wa kusikiliza rufani toka Mahkama Kuu ya Zanzibar isipokuwa kesi zozote zinazohusika na:

Tafsiri ya katiba hii
Mambo ya kiislamu ambayo yameanza katika Mahkama za Kadhi.

Mambo mengine yoyote yaliyoainishwa katika katiba hii na sheria nyengine yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.

Ndio kusema mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar hayakuongeza kitu kwani pamoja na ukweli kwamba mahakama hiyo haitokuwa na uwezo wa kusikiliza rufani kutoka Mahkama Kuu ya Zanzibar iliyotokana na mambo kuhusiana na vifungu vya haki za binadamu, inajulikana mamlaka ya Mahkama ya Rufaa ya Tanzania kwa Zanzibar ni kwa baadhi ya kesi tu.

Ieleweke kuwa kifungu cha 99(b) cha Katiba ya Zanzibar kimetaja kwa ufupi tu "mambo yaliyoanzia Mahakama ya Kadhi" lakini kwa mujibu wa Sheria Na. 3 ya mwaka 1985 iliyounda Mahakama ya Kadhi, mambo yote yanayohusu ndoa, talaka, mirathi na haki stahiki za mtoto yanasikilizwa katika mahakama za kadhi endapo wahusika wote ni waumini wa dini ya Kiislamu.

Hivyo pamoja na ukweli wa kuwa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar kwa kutumia kifungu cha 99(c) yameondoa uwezo wa Mahkama ya Rufaa kusikiliza masuala ya haki za binadamu, hakuna jipya. Lakini hata kama tukihoji busara iliyotumika katika kuliondoa suala la haki za Binadamu katika mamlaka ya Mahakama ya Rufaa bado si sahihi kujenga hoja kama kwamba hili la kuondoa baadhi ya mambo katika mamlaka ya Mahkama ya Rufaa ni jambo jipya lililokuja kwa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar.

Lissu anasema mabadikilo ya Katiba ya Zanzibar yamekiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano na kudhoofisha Muungano kwa vile sasa Zanzibar "imehalalisha uwepo wa vikosi vya Jeshi vya SMZ inavyoviita Idara Maalum." Idara Maalum imekuwepo hata kabla ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ikijumuisha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo (cha wahalifu) na kifungu hichi hakikubadilishwa hata nukta wala namba za vifungu.

Lakini tujiulize hivi Zanzibar chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina uwezo wa kuunda majeshi? Tena tutumie hiyohiyo katiba ya Jamhuri ya Muungano aliyozungumzia Lissu.

Ni kweli, kama alivyosema kuwa ibara ya 147(i) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema '‘ni marufuku kwa mtu yeyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania Jeshi la aina yoyote."

Laitani mwandishi angeangalia kifungu cha 151 cha katiba hiyo akaona neno "Serikali" lilivyotafsiriwa angeondoa shaka yoyote juu ya uwezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweza kuunda na kuweka jeshi. Neno serikali linatafsiriwa kama:

"Serikali maana yake ni pamoja na serikali ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au Halmashauri ya Wilaya au Mji, na pia mtu yeyote anaetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali au Halmashauri."

Tafsiri hii katika Katiba ya Muungano 1977 yenyewe inatoa fursa kwa serikali (ikiwemo SMZ) kama zilivyotafsiriwa na katiba hiyohiyo zilivyo na uwezo wa kuunda na kuweka jeshi.

Lissu amegusia vyeo vipya vya Zanzibar vya Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar vilivyoundwa na mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar. Anasema nayo yamekiuka katiba ya Muungano na hivyo ni '‘batili na hayana nguvu yoyote ya kisheria." Ananukuu kifungu cha 64(3) cha Katiba ya Muungano 1977 kujenga hoja yake. Mbona amekinukuu nusu?

"Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka…."

Lakini kwa mshangao utagundua kuwa kifungu hicho kinaendelea kumalizia kama ifuatavyo (lakini mwandishi ameona hiyo sehemu ya mwisho ya kifungu hicho asiinukuu, kwa nini, haieleweki)

"… na pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka."

Hivi muundo mzima wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vyeo vya viongozi wa Serikali hiyo na watendaji wake ni jambo lililo chini ya mamlaka ya Bunge? Hamna popote katika katiba au sheria yoyote inayotoa mamlaka kwa Bunge juu ya kuunda vyeo au muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Vyeo hivi vya makamo wawili wa Rais wa Zanzibar vimetokana na kundwa kwa Serikali yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa lakini kama vyeo hivi ni batili basi kwanza huo muundo wenyewe uliopelekea kuwepo kwa vyeo ungekuwa ni batili!

Muundo wa SMZ na vyeo katika Serikali tangu Aprili 1964 ni mambo yaliyo kwenye mamlaka ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na yanaongozwa na Katiba ya Zanzibar.

Lissu anaposema ilikuwa vema mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yakafuata misingi ya sheria anaonyesha kuwa sheria zimevunjwa. Hilo si kweli. Kwanza, yapasa atambuwe kuwa ni fikra potofu kuamini katiba ya Muungano ndio katiba mama na ile ya Zanzibar ni mtoto. Katiba zote hizi ni sawa kisheria. Katiba ya Zanzibar ina nguvu juu ya mambo yote ya Zanzibar (yasiyokuwa ya Muungano) wakati ya Muungano ina nguvu kwa mambo ya muungano na yale ya Tanganyika.

Hata kama baadhi ya taasisi, vyombo na vyeo vya Zanzibar vinatambuliwa katika katiba ya Muungano, hiyo haimaanishi kuwa katiba ya Muungano ndio inayosimamia mambo hayo. Juu ya yote haya, bado ninaamini mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ni muhimu kwani iliyopo haitoshelezi wakati.

========================
Muungano wa Tanzania sasa umekuwa dhaifu zaidi | Gazeti la MwanaHalisi
Hapa ipo makala ya Tundu Lissu

Mabadiliko ya katiba ya Zanzibar ni halali | Gazeti la MwanaHalisi
Hapa ipo makala ya Awadh A. Said
 
Attachments

warea

JF-Expert Member
Jan 22, 2010
244
0
Bila shaka mtoa hoja ni Mzanzibari na Lisu tunajua ni Mtanganyika. Kila mtu hapa ana hofu juu ya kupoteza utaifa wake ambao umeletwa na muungano ulioizaa Tanzania.

Ni kweli Zanzibar ilikuwa na katiba yake kabla ya Muungano, na Tanganyika pia ilikuwa na yake.

Baada ya Muungano katiba zote hizi zisingetakiwa kuwepo au kama vipi ziwepo zote. Tatizo linaanza pale panapokuwa na katiba ya Zanzibar wakti ya Tanganyika haipo. Kuna rais wa Zanzibar lakini hakuna wa Tanganyika.

Wengi wetu tulikuwa tunajua Zanzibar ni sehemu ya Tanzania na zamani kulikuwa na mikoa miwili ya Tanzania kwa upande wa Zanzibar kama sijakosea.

Tena tunaona mabadiliko ya katiba baada ya waziri mkuu kutamka kuwa Zanzibar si nchi ila sehemu ya muungano.

Mheshimiwa Lisu ana haki ya kusema kuwa muungano unaelekea kudhoofika, kwa kuangalia mambo haya ya kubadilishwa kwa katiba ya Zanzibar baadaya ya waziri mkuu kusema zanzibar ni sehemu ya nchi ya Tanzania.

Kwa kumsoma Lisu unaona Zanzibar ni nchi inayojitegemea, yenye mipaka yake, rais, mahakama na bunge.

Kwa muundo wa zamani Zanzibar wala Tanganyika zilikuwa sio nchi, bali sehemu za Muungano.
Ila sasa kama Zanzibar ni nchi, Lisu anatakiwa kutafuta nchi yake na katiba ya nchi yake iwepo. Usiwepo ugomvi kati yetu. Kama tunataka muungano wa Tanzania ulioimara, kila mtu lazima aukane uzanzibari au utanganyika. Sio Zanzibar nchi, huku Tanganyika haipo. Hapo tunadanganyana
 
Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,376
2,000
Mimi hili suali linanipa tabu kulifahamu. Vipi nchi ambayo imepata uhuru, ikawa mwanachama wa UN na Jumuiya nyengine za kinchi ipoteze hadhi yake ya kinchi hata kama inaingia katika Muungano na nchi nyengine ?

Kwa maana nyengine kuna nchi inayokubali kwa hiyari yake kuwa mkoa au wilaya inapoingia katika muungano na nchi nyengine ?

Kuna wanaosema Tanganyika na Zanzibar waliungana na kuwa nchi moja. Hii dhana ni ukweli na uongo pia.
Dhana hii ni kweli pale usanii wa jina ulipofanyika. Kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamhuri ya Muungano wa TanZania. Na baadae Tanzania tu.

Dhana ya Tanzania ni nchi moja inakuwa ni uongo kwa sababu Jamhuri ya Tanzania haijapata kuwa nchi moja. Uthabiti wa hili ni kuwa Muungano uliofanyika ulikuwa ni wa baadhi ya mambo tu. Kumi na moja kwa idadi na kuwepo kwa mamlaka za kisheria tatu. Ukipitia mkataba wa muungano, The articles of the union between Tanganyika and Zanzibar utayaona hayo. Ni wazi kuwa haikuwa Tanganyika wala Zanzibar zilizo-surrender soveregnity yao yote kwa Muungano.

Vipi Tanganyika ilitoweka hili ndilo jambo kwa wabunge wetu wa Tanganyika kulitafutia jibu.Bila shaka lilianza kwenye kuelekeza kuwa litakapoanza kazi zake Bunge la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lifanye kazi pia kama bunge la Tanganyika na pia katika kubadilisha jina la Muungano.

Nani alielekeza kuwa Bunge la Muungano pia lifanye kazi za Bunge la Tanganyika? Kwa nini aliamua hivi?

Mkanganyiko na mkorogo huu wa muungano wetu, unapata mtihani mgumu sasa hivi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Mambo mengi ya Jumuiya hiyo si mambo ya Muungano kwa hiyo nchi nyengine zinahoji Serikali ya Tanzania inapata wapi uhalali wa kuiwakilisha Zanzibar kwa mambo ambayo si ya Muungano.

Ni vizuri kuona wanasheria wanatoa hoja zao ili kutupa na sisi mwanga.Itatusaidia kupunguza ushabiki.

Kuna haja ya lile G55 kufufuka, Mnyika anaweza kupeleka hoja hii ya kuirudisha Serikali ya Tanganyika na nchi ya Tanganyika ndani ya Muungano na itambulike hivyo.

Kisheria , nchi hii ipo na taasisi zake nyengine zipo na zinaonekana wazi. Kuna Wizara ambazo si za Muungano, mfumo wa mahakama pia kwa Tanganyika. sio sheria zote kuwa ni za Muungano. Hata bajeti kwa mambo ambayo si ya Muungano.

Ni wakati muafaka sasa ule mkataba halisi wa Muungano uwekwe hadharani na pia mfumo wa muungano upitiwe upya.Kero za Muungano zimekuwa ni nyingi ambazo sasa zimeibua hisia za kudhulumiana, manung'uniko,malumbano, kejeli na zinajenga chuki miongoni mwa jamii zetu mbili na watu wake.
 
abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
0
Na Mwinyi Sadallah6th March 2011Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar (DPP), Othman Masoud Othman amesema muundo wa Muungano ulivyo hivi sasa hauleti sura nzuri baada ya Rais wa Zanzibar kuondolewa nafasi ya kuwa makamo wa Rais wa Muungano wa Tanzania kufuatia mabadiliko ya 11 ya katiba.
Hayo ameyaeleza alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu mada ya “Mgongano kati ya mapatano ya Muungano na Katiba ya Tanzania,” katika mjadala wa Katiba mpya uliyofanyika jana katika ukumbi wa EACROTANAL mjini hapa.
Alisema marekebisho hayo ya Katiba yalimaliza muungano kwa kuwa Zanzibar ilipoteza mamlaka ya Rais wa Zanzibar katika muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Muungano huo uliotokana na Jamhuri ya watu wa Zanzibar na Tanganyika.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba kabla ya mabadiliko hayo, Rais wa Zanzibar alikuwa sehemu ya Muungano na kushiriki katika vikao mbalimbali tofauti na hali ilivyo hivi sasa jambo ambalo halileti sura mzuri katika kuimarisha Muungano.
Alisema pamoja na kuanzisha nafasi ya Makamo wa Rais wa Muungano bado mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Katiba hana mamlaka ya kiutendaji kwa Zanzibar kwa vile si mjumbe wa Baraza la Mawaziri Zanzibar wala sio mtendaji katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
“Tujiulize Makamo wa Rais wa Muungano ana uhusiano gani na Zanzibar wakati si mjumbe wa Baraza la Mawaziri, hana uhusiano wa kimamlaka ya utendaji na Zanzibar, wala hana uwezo wa kumpa amri hata sheha,” alihoji Mkurugenzi huyo.
Alisema kimsingi, kiungo kilichobaki katika Muungano hakina mamlaka yoyote kwa Zanzibar na kushauri kuna haja ya kufanya mabadiliko ikiwemo kuangalia upya orodha ya mambo ya muungano.
Alisema kwamba hivi sasa mambo ya muungano yakifanyiwa uchambuzi wa kina ni zaidi ya 31 kutoka 11 jambo ambalo alisema linahitaji kuangaliwa wakati wa kuandika Katiba mpya.
Aidha, alisema kumekuwepo na mgongano wa Katiba ya Muungano na Zanzibar katika utungaji wa sheria, akitoa mfano wa Ibara ya 64 ya Katiba ya Muungano ambayo inaruhusu sheria zinazopitishwa na Bunge kutumika Zanzibar wakati Ibara ya 132 (1) ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 inasema sheria zote zinazotungwa na bunge ambazo hazihusiani na mambo ya Muungano ni lazima ziridhiwe na Baraza la Wawakilsihi kabla ya kutumika Zanzibar.
Alisema kwamba pamoja na Bunge kuwa na wabunge 324 bado uwakilishi wa Zanzibar katika chombo hicho bado ni mdogo kwa kuwa bunge lililopita Zanzibar ilikuwa na wabunge 64 tu, na kutahadharisha kuwa idadi isiangaliwe kwa wingi wa watu au ukubwa wa kijiografia Zanzibar, iangaliwe kama ni mataifa mawili yaliyoungana.
Hata hivyo, alisema kwamba pamoja na kasoro hizo Katiba ya Muungano imeweka sharti kuwa huwezi kubadilisha orodha ya mambo ya muungano au kuongeza hadi ipatikane theluthi-mbili ya wabunge kutoka pande mbili za muungano, jambo ambalo alisema linahitaji kuzingatiwa katika mabadiliko yoyote ya Katiba ya Muungano.
Akichambuwa mada ya mkurugenzi wa mashitaka, mwanasheria wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Yahya Hamad Khamis, alisema amefuatilia sana nyaraka za muungano lakini nyingi zimesainiwa na Rais wa kwanza Mwalimu Julius Nyerere bila saini ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu sheikh Abeid Amani Karume, jambo ambalo linazua maswali mengi juu ya uhalali wa muungano.
“Nimetafuta sana sehemu aliyosaini Rais Karume, sioni saini yake, kama yupo mtu aliyeona atusaidie kwa hilo ili kuondosha utata,” alisema mwanasheria huyo huku akipigiwa makofi na washiriki wa kongamano hilo.
Hata hivyo, alisema muungano upo kinadharia lakini kwa mujibu wa sheria haupo kwa vile ni lazima iangaliwe umekuja vipi na nyaraka zenyewe kutokana na kiongozi mmoja kutoka upande mmoja wa muungano kutoonekana saini yake.
Yahya ambaye ni mwanasheria mkongwe Zanzibar, alisema kwamba upo mgongano wa kikatiba kwa sheria zinazotungwa na Bunge na baadaye kutumika Zanzibar kwa vile ibara ya 64 ya Katiba ya Muungano imeipa uwezo wa kutumika Zanzibar, huku akiunga mkono mtoa mada kuwa mgongano huo ni lazima uangaliwe upya katika kuandika katiba mpya.
Alisema kwamba masuala ya muungano yamekuwa yakiongezeka kinyemela jambo ambalo alisema linahitaji kuangaliwa kwa wakati hasa maeneo yenye kasoro ili yaweze kuangaliwa katika mjadala wa katiba unaotarajiwa kuanza nchini.
Akichangia mada hiyo, Mhandisi kutoka kampuni ya ZANTEL, Ali Khamis alishangaa kwa kusema kuwa matatizo ya muungano yamekuwepo muda mrefu lakini wanasheria Zanzibar wameshindwa kuyachambua na kuyatafutia ufumbuzi kwa mujibu wa sheria.
Naye Mwandishi wa habari Mkongwe Zanzibar, Salim Said Salim, alisema kwamba muungano wa Tanganyika na Zanzibar haukufanyika kwa uwazi, na ndio chanzo cha mkanganyiko katika muungano.
Alisema kuwa aliyekuwa Waziri mkuu wa Zanzibar wakati muungano unaundwa Marehemu Kassim Hanga na mwanasheria mkuu wa Zanzibar wakati huo Jaji Wolfang Dourado hawakushirikishwa ipasavyo katika kuunda muungano.
Hata hivyo, Salim alisema kwamba viongozi na wananchi wengi Tanzania Bara na Zanzibar hawafahamu mambo ya msingi yaliyokuwemo ndani ya Muungano na yasiokuwa ya muungano na kazi hiyo ya kuwaelimisha inahitaji kufanywa na serikali yenyewe ili wananchi waweze kuamua mfumo wa muungano wanaotaka.
Naye Miraji Khamis Kiongwe, alisema wakati umefika mtu anayechaguliwa kuwa kiongozi Zanzibar lazima ajulikane kama Mzanzibari halisi mwenye babu na bibi ili aweze kutetea vizuri maslahi ya Zanzibar.
 
Semilong

JF-Expert Member
Mar 5, 2009
1,714
1,225
Alisema kwamba pamoja na Bunge kuwa na wabunge 324 bado uwakilishi wa Zanzibar katika chombo hicho bado ni mdogo kwa kuwa bunge lililopita Zanzibar ilikuwa na wabunge 64 tu, na kutahadharisha kuwa idadi isiangaliwe kwa wingi wa watu au ukubwa wa kijiografia Zanzibar, iangaliwe kama ni mataifa mawili yaliyoungana.
kwa hiyo mnataka kuwa na wabunge wangapi? sisi kinondoni kuna wabunge watatu na population ni sawa
kama hamridhiki hamna haja ya kuwa na muungano
Akichambuwa mada ya mkurugenzi wa mashitaka, mwanasheria wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Yahya Hamad Khamis, alisema amefuatilia sana nyaraka za muungano lakini nyingi zimesainiwa na Rais wa kwanza Mwalimu Julius Nyerere bila saini ya Rais wa kwanza wa Zanzibar, Marehemu sheikh Abeid Amani Karume, jambo ambalo linazua maswali mengi juu ya uhalali wa muungano.
"Nimetafuta sana sehemu aliyosaini Rais Karume, sioni saini yake, kama yupo mtu aliyeona atusaidie kwa hilo ili kuondosha utata," alisema mwanasheria huyo huku akipigiwa makofi na washiriki wa kongamano hilo.
.
kama hamna saini ya karume then muungano ni batili na hamna haja ya kuwa na muungano
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,581
0
Kwanini wasifunge virago waondoke, aanze Mzee Mwinyi na Watoto wake, then wafuate Wapemba wote wafunge maduka yao na Majini yao waondoke wafanye kwa vitendo na kwanini CCM haioni kuwa hawa ndio wana hatarisha amani na siyo CDM?? CCM has dead? if yes, When? if not, why this? if not sure, why not sign?
 
mashikolomageni

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
1,568
1,195
Hata hivyo, alisema muungano upo kinadharia lakini kwa mujibu wa sheria haupo kwa vile ni lazima iangaliwe umekuja vipi na nyaraka zenyewe kutokana na kiongozi mmoja kutoka upande mmoja wa muungano kutoonekana saini yake.
.
Hili jambo ndio UHAINI hayo yanayosemwa na CDM hayana uhusiano na uhaini, sasa hatua zichukuliwe au kama hazichukuliwi basi Zenj inayo haki ya kujitenga na sie Tanganyika yetu irudi mapema. Ila kama kweli upo kinadharia tu basi hatuna haja nao mngetangaza siku hiyo hiyo tu kuwa nyie ni Taifa na Majirani zeni ni Tanganyika.
 
Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,713
1,225
kwa hiyo mnataka kuwa na wabunge wangapi? sisi kinondoni kuna wabunge watatu na population ni sawa
kama hamridhiki hamna haja ya kuwa na muungano

kama hamna saini ya karume then muungano ni batili na hamna haja ya kuwa na muungano
Hivyo bwanamdogo uko na mada inayozungumzwa? Hebu nikkukumbushe kidogo! Ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar!
Hatuzungumzii madaraka mikoani ya Nyerere!
 
Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,713
1,225
Kwanini wasifunge virago waondoke, aanze Mzee Mwinyi na Watoto wake, then wafuate Wapemba wote wafunge maduka yao na Majini yao waondoke wafanye kwa vitendo na kwanini CCM haioni kuwa hawa ndio wana hatarisha amani na siyo CDM?? CCM has dead? if yes, When? if not, why this? if not sure, why not sign?
Watoto wa siku hizi mnapupa kujuwa mambo! Itabidi Kisarawe iwe Zanzibar ili hilo la Mwinyi kuondoka litekelezwe! Hivyo mnajidanganya kuwa hakuna walowezi wa kwenu Zanzibar? Mbona ni wengi na ndio vigogo vya CCM ndio maana Tanganyika hamko tayari kuwaacha kwenye mataa kwa kuvunja Muungano.
 
Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,581
0
Watoto wa siku hizi mnapupa kujuwa mambo! Itabidi Kisarawe iwe Zanzibar ili hilo la Mwinyi kuondoka litekelezwe! Hivyo mnajidanganya kuwa hakuna walowezi wa kwenu Zanzibar? Mbona ni wengi na ndio vigogo vya CCM ndio maana Tanganyika hamko tayari kuwaacha kwenye mataa kwa kuvunja Muungano.
We ndio Mtoto Mkuu chunga mdomo wako; Kama hamtaki kuondoka sasa mnalalamika nini kila siku, chagueni moja Mkae kimia au Mfunge virago muondoke tena hata leo ondokeni mnatupigia kelele kila siku mkisikia kuondoka mnatetemeka nini sasa.
 
GHIBUU

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
4,251
2,000
Kifo cha tanganyika ni cha kujitakia,,,,,maiti ipoo ifukueni basi huyo mtanganyika
 
Sio Mwanasiasa

Senior Member
Mar 4, 2011
115
195
mtu akitaka kuelewa mantik ya mabadiliko ya katiba ya zanzibar ni muhim kwake kwanza afaham nature ya huu muungano wetu..walichofanya wanzazibar ni kuunda katiba yao inayofuata matakwa ya muungano...so mabadiliko ya katiba ya zanzibar ni halali sana sana
 
HM Hafif

JF-Expert Member
Aug 16, 2009
1,359
0
Na Awadh A. Said
MAKALA ya Tundu Lissu iliyochapishwa na gazeti hili chini ya kichwa cha habari, Muungano wa Tanzania sasa umekuwa dhaifu zaidi imenishawishi kutoa maoni kwa kuona inaelekeza watu sivyo.
Lissu, ambaye ni mwanasheria mwenzangu, anasema mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 yamedhoofisha muungano wa Tanzania kwa "kumong'onyoa misingi karibu yote ya muungano huo, kubadili sura ya muungano wenyewe, mipaka yake na muundo wake." Ana khofu mabadiliko hayo "yanaweza kuwa chanzo kikuu cha kubomoka kwa Muungano na hata tishio kwa usalama wa mipaka ya Taifa."
Anaamini mabadiliko hayo yaliitangaza Zanzibar '‘kuwa nchi yenye mipaka kamili" na kwamba "Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa." Anaegemea kifungu cha kwanza cha Katiba ya Zanzibar kabla ya marekebisho, kinachosema, '‘Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."
Hapa kuna mambo mawili: Kwanza kuwa mabadiliko hayo ndio yaliyoitangaza Zanzibar nchi, na pili ndiyo yaliyobainisha mipaka ya Zanzibar ambayo mwanzo haikutajwa. Yote haya si kweli.
Zanzibar ilianza kuwa na katiba yake ya kwanza baada ya Mapinduzi ya 1964. Ilikuwa mwaka 1979. Baadaye ilifutwa na kuandikwa upya mwaka 1984 ilipoandikwa inayoendelea mpaka sasa. Ndiyo iliyofanyiwa marekebisho mara 10 yakiwemo haya yanayojadiliwa sasa. Je, Katiba hiyo haikutaja Zanzibar kama nchi hadi yalipokuja mabadiliko ya kumi? Ni kweli Katiba ya Zanzibar ya 1984 kabla ya marekebisho ya kumi ilieleza katika kifungu cha 1 kuwa "Zanzibar ni sehemu ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Lakini ukiwacha kifungu hicho, vifungu kadhaa au tuseme katiba yote inaitaja Zanzibar ni nchi.
(9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.
(9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …
(10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:
(10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.
(12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.
(21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI…
(23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi…
Inaonyesha Lissu alitazama tu kifungu hicho cha kwanza, akapuuza vingine. Katiba ya Zanzibar imebaki na idadi ileile ya vifungu 135 hata baada ya marekebisho ya kumi.
Msingi mkuu wa katika kanuni za kutafsiri sheria, ni kuwa ili uweze kupata tafsiri sahihi kwa waraka wowote (iwe ni Katiba, Sheria, Mkataba n.k.) unapaswa kusoma waraka wote ndipo upate maana, tafsiri au dhamira inayopatikana katika waraka huo kuhusiana na jambo husika. Ni dhahiri huwezi kuchopoa kifungu kimoja tu ukapata usahihi.
Hebu tuangalie hichohicho kifungu cha kwanza kisemacho '‘Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano." Ni sawa Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri Ya Muungano, lakini inasimama katika utambulisho upi? Ni sehemu kama Mkoa, Wilaya, Tarafa, Jimbo, Kata au kitongoji? Zanzibar ina katiba yake, ina Rais wake, ina Mahkama zake, ina mawaziri wake, ina Baraza lake la kutunga sheria (Baraza la Wawakilishi), ina watu wake (tena wana vitambulisho), ina bendera yake, ina wimbo wake wa Taifa, ina Mamlaka yake ya serikali za mitaa, ina magereza yake (Vyuo vya Mafunzo), ina vikosi vyake maalum vya ulinzi, ina mapato yake na bajeti yake n.k. Jee kuna Mkoa au Wilaya yenye yote hayo? Na yamekuwepo kabla ya mabadiliko yaliyofanywa.
Lissu anasema, "Rais anajua kuwa kabla ya mabadiliko hayo kufanyika, Zanzibar haikuwa nchi na wala mipaka yake haikutajwa." Kabla ya mabadiliko ya kumi, Katiba ya Zanzibar 1984, kifungu cha 2(i) kinasema:
2(i) "Eneo la Zanzibar ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka na bahari yake ambayo kabla ya Muungano ikiitwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar." Baada ya mabadiliko ya kumi, kifungu hicho kinaendelea kuwepo kikisema: Zanzibar ni nchi ambayo eneo la mipaka yake ni eneo lote la visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na visiwa vidogo vidogo vilivyoizunguka bahari yake ambayo kabla ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiitwa Jamhuri ya watu wa Zanzibar."
Hoja ya pili ya Lissu ni mabadiliko haya yanadhoofisha Muungano kwa vile yameondoa mamlaka ya kuigawa Zanzibar katika mikoa kutoka mikononi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na kuweka mamlaka hayo kwa Rais wa Zanzibar. Hili ni kweli limefanyika katika mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar. Tujiulize sababu. Inaeleweka wazi kuwa ni Rais wa Zanzibar ambae kipindi chote tokea Muungano wa Tanzania uasisiwe 1964, ndie anayeigawa Zanzibar katika mikoa na wilaya.
Hakuna kumbukumbu inayoonesha Rais wa Jamhuri ya Muungano amewahi kuigawa Zanzibar katika Mikoa au Wilaya. Sasa kwa takriban miaka 47 mamlaka hayo yalikuwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano kikatiba lakini kiutendaji na kiutekelezaji Rais wa Zanzibar ndiye aliyekuwa anatekeleza mamlaka hayo. Mabadiliko yametambua hilo na kurekebisha. Haiwezekani tukadumisha vifungu ndani ya katiba ambavyo vinaonekana ni pambo tu. Bali hili litoshe kuonesha mkanganyiko unaozikumba katiba zetu mbili.
Hoja ya tatu ya Lissu ni kuwa mabadiliko ya kumi yamepunguza mamlaka ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania. Anasema: "Mabadiliko yamekiuka katiba kwa kuinyang'anya Mahakama ya Rufaa mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahakama Kuu ya Zanzibar."
Hata mara moja tangu ianzishwe, haijawahi kutokea kwa Mahkama ya Rufaa kuwa na mamlaka ya kusikiliza rufaa zote zinazotoka katika Mahkama Kuu ya Zanzibar. Katiba ya Zanzibar iliipa mamlaka mahkama hiyo kwa baadhi ya kesi tu.
Kifungu cha 99 cha Katiba ya Zanzibar kinasema, Mahkama ya Rufaa ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania itakuwa na uwezo wa kusikiliza rufani toka Mahkama Kuu ya Zanzibar isipokuwa kesi zozote zinazohusika na:
Tafsiri ya katiba hii
Mambo ya kiislamu ambayo yameanza katika Mahkama za Kadhi.
Mambo mengine yoyote yaliyoainishwa katika katiba hii na sheria nyengine yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi.
Ndio kusema mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar hayakuongeza kitu kwani pamoja na ukweli kwamba mahakama hiyo haitokuwa na uwezo wa kusikiliza rufani kutoka Mahkama Kuu ya Zanzibar iliyotokana na mambo kuhusiana na vifungu vya haki za binadamu, inajulikana mamlaka ya Mahkama ya Rufaa ya Tanzania kwa Zanzibar ni kwa baadhi ya kesi tu.
Ieleweke kuwa kifungu cha 99(b) cha Katiba ya Zanzibar kimetaja kwa ufupi tu "mambo yaliyoanzia Mahakama ya Kadhi" lakini kwa mujibu wa Sheria Na. 3 ya mwaka 1985 iliyounda Mahakama ya Kadhi, mambo yote yanayohusu ndoa, talaka, mirathi na haki stahiki za mtoto yanasikilizwa katika mahakama za kadhi endapo wahusika wote ni waumini wa dini ya Kiislamu.
Hivyo pamoja na ukweli wa kuwa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar kwa kutumia kifungu cha 99(c) yameondoa uwezo wa Mahkama ya Rufaa kusikiliza masuala ya haki za binadamu, hakuna jipya. Lakini hata kama tukihoji busara iliyotumika katika kuliondoa suala la haki za Binadamu katika mamlaka ya Mahakama ya Rufaa bado si sahihi kujenga hoja kama kwamba hili la kuondoa baadhi ya mambo katika mamlaka ya Mahkama ya Rufaa ni jambo jipya lililokuja kwa mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar.
Lissu anasema mabadikilo ya Katiba ya Zanzibar yamekiuka katiba ya Jamhuri ya Muungano na kudhoofisha Muungano kwa vile sasa Zanzibar "imehalalisha uwepo wa vikosi vya Jeshi vya SMZ inavyoviita Idara Maalum." Idara Maalum imekuwepo hata kabla ya mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar ikijumuisha Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU), Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), Chuo cha Mafunzo (cha wahalifu) na kifungu hichi hakikubadilishwa hata nukta wala namba za vifungu.
Lakini tujiulize hivi Zanzibar chini ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar haina uwezo wa kuunda majeshi? Tena tutumie hiyohiyo katiba ya Jamhuri ya Muungano aliyozungumzia Lissu.
Ni kweli, kama alivyosema kuwa ibara ya 147(i) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema '‘ni marufuku kwa mtu yeyote au shirika lolote au kikundi chochote cha watu, isipokuwa Serikali kuunda au kuweka Tanzania Jeshi la aina yoyote."
Laitani mwandishi angeangalia kifungu cha 151 cha katiba hiyo akaona neno "Serikali" lilivyotafsiriwa angeondoa shaka yoyote juu ya uwezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweza kuunda na kuweka jeshi. Neno serikali linatafsiriwa kama:
"Serikali maana yake ni pamoja na serikali ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar au Halmashauri ya Wilaya au Mji, na pia mtu yeyote anaetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali au Halmashauri."
Tafsiri hii katika Katiba ya Muungano 1977 yenyewe inatoa fursa kwa serikali (ikiwemo SMZ) kama zilivyotafsiriwa na katiba hiyohiyo zilivyo na uwezo wa kuunda na kuweka jeshi.
Lissu amegusia vyeo vipya vya Zanzibar vya Makamo wa Kwanza wa Rais na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar vilivyoundwa na mabadiliko ya Katiba ya Zanzibar. Anasema nayo yamekiuka katiba ya Muungano na hivyo ni '‘batili na hayana nguvu yoyote ya kisheria." Ananukuu kifungu cha 64(3) cha Katiba ya Muungano 1977 kujenga hoja yake. Mbona amekinukuu nusu?
"Endapo sheria yoyote iliyotungwa na Baraza la Wawakilishi inahusu jambo lolote katika Tanzania Zanzibar ambalo liko chini ya mamlaka ya Bunge, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka…."
Lakini kwa mshangao utagundua kuwa kifungu hicho kinaendelea kumalizia kama ifuatavyo (lakini mwandishi ameona hiyo sehemu ya mwisho ya kifungu hicho asiinukuu, kwa nini, haieleweki)
"… na pia endapo sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inahusu jambo lolote ambalo liko chini ya mamlaka ya Baraza la Wawakilishi, sheria hiyo itakuwa batili na itatanguka."
Hivi muundo mzima wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na vyeo vya viongozi wa Serikali hiyo na watendaji wake ni jambo lililo chini ya mamlaka ya Bunge? Hamna popote katika katiba au sheria yoyote inayotoa mamlaka kwa Bunge juu ya kuunda vyeo au muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Vyeo hivi vya makamo wawili wa Rais wa Zanzibar vimetokana na kundwa kwa Serikali yenye Muundo wa Umoja wa Kitaifa lakini kama vyeo hivi ni batili basi kwanza huo muundo wenyewe uliopelekea kuwepo kwa vyeo ungekuwa ni batili!
Muundo wa SMZ na vyeo katika Serikali tangu Aprili 1964 ni mambo yaliyo kwenye mamlaka ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar na yanaongozwa na Katiba ya Zanzibar.
Lissu anaposema ilikuwa vema mabadiliko ya katiba ya Zanzibar yakafuata misingi ya sheria anaonyesha kuwa sheria zimevunjwa. Hilo si kweli. Kwanza, yapasa atambuwe kuwa ni fikra potofu kuamini katiba ya Muungano ndio katiba mama na ile ya Zanzibar ni mtoto. Katiba zote hizi ni sawa kisheria. Katiba ya Zanzibar ina nguvu juu ya mambo yote ya Zanzibar (yasiyokuwa ya Muungano) wakati ya Muungano ina nguvu kwa mambo ya muungano na yale ya Tanganyika.
Hata kama baadhi ya taasisi, vyombo na vyeo vya Zanzibar vinatambuliwa katika katiba ya Muungano, hiyo haimaanishi kuwa katiba ya Muungano ndio inayosimamia mambo hayo. Juu ya yote haya, bado ninaamini mabadiliko ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ni muhimu kwani iliyopo haitoshelezi wakati.
Tundu Lisu ameudanganya umma na kupotosha kabisa muungano kwa kutumia taaluma yake. Je huyu atafaa kuwa kiongozi?

Ahsante sana Sh Awadh kwa kutuweka sawa.

Allah akuzidishie kila lililo jema na kukujaza kila lenya kheri na kukuepusha na Sha
ri
 
Top Bottom