Hasira za Wazanzibar kuchoshwa na Muungano

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
mkuu umeulizwa swali nimekujibu.. unaongeza mengie.. kwanza... nani baba na nani mtoto!! .. uanposema znz ni mwanetu ni kama tuna uwezo wa kuwafanya lolote. znz ni nchi .. tuwaache wajiamulie mambo yao wenyewe... Ndoa hailazimishwi.. ndani ya miaka 47 wao hawajaona faida yoyote!! mimi kama mtanganyika sitapungukiwa na lolote , nitafurahi wakiwa kama nchi jirani... sababu tutawatreat as foreigners .. umeme watalipa kama wageni.. biashara watakuwa wawekezaji..
Ukiona Wazanzibari hawajitoi kwenye Muungano ujue fika kwamba wanaupenda sana! Hayo malalamiko ni jambo la kawaida tu, ni sawa na wananchi wa Kigoma kulalamika juu ya kutounganishwa kwenye umeme wa gridi ya Taifa, au wananchi wa Kanda ya Ziwa kulalamikia kutofaidika kwao na madini! What's so special na malalamiko ya Wazanzibari wapatao 1mil tu?
 

Falconer

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
717
500
Buchana, huna mpya. Wewe hukufahamu kuwa Nyerere alitaka muungano wa nchi mbili. What so special na malalamiko ya wazanzibari wapatao 1ml tu?. Kweli ndugu yangu umekosa dira. Sisi sio special, sisi ni unique. WE WANT OUT, THATS IT. Nyinyi kama ni 30 ml, ni nyinyi na sisi ni sisi. Kwa nini hamutuachi tukaamua mambo yetu.
Munasema kuhusu security yenu wakati nyinyi ni wavamizi wa nchi majirani. Munahistoria ya uchokozi wa majirani. Sisi hatuja kuja kwenu kwa uchokozi. Nyinyi ndio wachokozi.Sisi hatutaki muungano wala hakuna jengine lolote hatuutaki muungano. It's time to free Zanzibar from Tanganyika colonialists.
 

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,202
2,000
Kajichome moto basi kama Boazizi ili uonesha mapenzi yako nahuo muungano, na pia utakuwa umeutetea vuzuri.
ILa kwa kifupi ni kuwa muungano hauna ridhaa ya wananchi wa pande zote mbili.
Pia hakuna faida yotote kwa Bara kuusu muungano
Kwa visiwani ni faida ipo kwa wafanyabiashara wachache na wanasiasa wenye njaa.
Sasa labda wewe utueleze huo umuhimu unaounona unatokana na hizo faida hapo ambazo utazitetea hata kama zitagharimu maisha yako
Tuache ushabiki muungano hauna fada ni mzigo wa kujitakia, kama ni undugu, sio ishu, kwani tumepakana na nchi nyingi za jirani ambapo tunaundugu nao.
Nionsheshe ni wapi ilipo ridhaa ya wananchi kuhusu kuwepo kwa nchi iitwayo Tanganyika ya Mjerumani iliyojumuisha Rwanda na Burundi, kisha onesha ridhaa ya wananchi kuhusu uwepo wa Tanganyika ya Mwingereza isiyojumuisha Rwanda na Burundi! tuoneshe ridhaa ya wananchi wa Zanzibar kuhusu Muungano wa Visiwa vya Unguja na Pemba!
 

Makaimati

JF-Expert Member
Apr 4, 2011
462
0
kimsingi Tanganyika tunanyonywa na hao wazanzibar, utaona viongozi wengi wakubwa kwenye itifaki ni kutoka zanzibar, wabunge wote wa pemba jumla ya kula zao ni sawa na mbunge mmoja wa tanganyika na tena wana haki sawa ya kupiga kura bungeni, mkopo sawa wa gari, mshahara sawa!! sasa huoni ni unyonyaji? makamu wa rais wawili, rais wa zanzibar, makamu wa rais tanganyika wote vyeo vya juu ni wazanzibar na wanalipwa pesa za muungano, sie tuna kikwete. bora tuwe na tanganyika yetu na wao wakabaki na zanzibar yao.
Kweli maneno yako Mkuu Duniangumu. Huo mnaouita "muungano" mliutaka nyinyi, mnaonaje mkatuwacha na mkawa huru?

Khofu yangu ni kuchelewa na mkajikuta hamna Tanganyika wala Zanzibar

Zanzibar for Zanzibaris
 

Edward Teller

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
3,836
2,000
Mimi nipo tayari kuutetea muungano huu hata kama itanigharimu maisha. Nawakilisha....
si vibaya kama wewe na wenzio wachache hamtaki muungano-basi mtakufa na sisi wengine tutafuvunja muungano na kuendelea na maisha
kwa hio jiandae kwa hilo
 

MrFroasty

JF-Expert Member
Jun 23, 2009
751
250
@Lord,

Unaweza tutajia una ndugu wangapi kutoka Zanzibar ? Maana isije ikawa unaleta za kuleta.Mie nahisi kama udugu, basi watanganyika wana udugu zaidi na waganda, wakenya, warundi, wanyasa n.k.Hao wana udugu zaidi kimila, silka na utamaduni.Kuliko hata wazanzibari.

Hivyo ni kheri mukaelekeza nguvu kwenye EAC, ambapo wakongo wako tayari kabisa.Lakini Sitta anawakatalia, anasema wazanzibari ni ndugu wake zaidi kwa miaka 47!
 

Lord

Member
Feb 13, 2009
91
70
Acha ujinga, Muungano huu kama usiporekebishwa kufuata matakwa ya wananchi hautachukua miaka 10 mbele, lazima uvunjike! Kwani kati TZ Bara na Oman, wepi wenye undugu wa Damu na wazenji? Soma alama za nyakati-SUDAN ilikuwa moja sasa ziko ngapi? Czechslovakia ilikuwa moja, sasa iko wapi? USSR iko wapi? Mifano ni mingi kwani wote hao walikuwa hawana undugu wa damu?
Kumbe wazanzibar ndugu zao wa Oman???? Kweli nimeamini yale maneno yanayosemwa kuwa kuna watu wanatamani kuuvunja muungano ili wafufue undugu na waarabu. Si kosa lako huijui historia. Pengine wewe unayesema haya bibi yako ni Mnyamwezi.
 

Lord

Member
Feb 13, 2009
91
70
@Lord,

Unaweza tutajia una ndugu wangapi kutoka Zanzibar ? Maana isije ikawa unaleta za kuleta.Mie nahisi kama udugu, basi watanganyika wana udugu zaidi na waganda, wakenya, warundi, wanyasa n.k.Hao wana udugu zaidi kimila, silka na utamaduni.Kuliko hata wazanzibari.

Hivyo ni kheri mukaelekeza nguvu kwenye EAC, ambapo wakongo wako tayari kabisa.Lakini Sitta anawakatalia, anasema wazanzibari ni ndugu wake zaidi kwa miaka 47!
Ungeujua mwiingiliano uliopo kati ya wabara wanaoishi mwambao wa bahari ya hindi na wazanzibar usingekuwa na haja ya kuuliza hili swali
 

Lord

Member
Feb 13, 2009
91
70
Nionsheshe ni wapi ilipo ridhaa ya wananchi kuhusu kuwepo kwa nchi iitwayo Tanganyika ya Mjerumani iliyojumuisha Rwanda na Burundi, kisha onesha ridhaa ya wananchi kuhusu uwepo wa Tanganyika ya Mwingereza isiyojumuisha Rwanda na Burundi! tuoneshe ridhaa ya wananchi wa Zanzibar kuhusu Muungano wa Visiwa vya Unguja na Pemba!
Kuna ridhaa gani kati yako wewe na dada yako au kaka yako kuwa ndugu???
 

Lord

Member
Feb 13, 2009
91
70
Buchana, huna mpya. Wewe hukufahamu kuwa Nyerere alitaka muungano wa nchi mbili. What so special na malalamiko ya wazanzibari wapatao 1ml tu?. Kweli ndugu yangu umekosa dira. Sisi sio special, sisi ni unique. WE WANT OUT, THATS IT. Nyinyi kama ni 30 ml, ni nyinyi na sisi ni sisi. Kwa nini hamutuachi tukaamua mambo yetu.
Munasema kuhusu security yenu wakati nyinyi ni wavamizi wa nchi majirani. Munahistoria ya uchokozi wa majirani. Sisi hatuja kuja kwenu kwa uchokozi. Nyinyi ndio wachokozi.Sisi hatutaki muungano wala hakuna jengine lolote hatuutaki muungano. It's time to free Zanzibar from Tanganyika colonialists.
Unaweza taja ni vipi Tanganyika inawanyonya wazanzibar???
 

Makaimati

JF-Expert Member
Apr 4, 2011
462
0
Sadakta Mkuu Duniangumu kwani kwa Wazanzibari walivyokuja juu, iko hatari kubwa mkaamka siku moja mkakuta hamna Tanzania wala Tanganyika.

Daini haraka Tanganyika yenu maana iliuliwa kinamna na Mkuu Nyerere kwa ajili ya kuimeza Zanzibar kiujanjaujanja.

Wazanzibari sasa wamebadilika na wamechoka kuwa koloni la Tanganyika.
 

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
0
Written by Ashakh (Kiongozi) // 24/04/2011 // Habari // 5 Comments-cheche zaruka ukumbini kutoka kwa wachangiaji
-Wengi wasema Muungano unanuka dhulma
-walioutetea wapigwa na mshangao.
Na Rasmi.
Jana katika ukumbi wa Froud Community Centre uliopo London, jumuiya ZAWA (Zanzibar Welfare association) iliendesha mjadala wa kuujadili muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao unatimiza miaka 47 tokea kuasisiwa kwake.
Lengo na madhumuni yalikuwa ni kuuzungumza muungano huo, faida na hasara zake kwa upande wa Zanzibar. Na kwa kila sekunde ilivyozidi kuenda mbele tokea kipigwe kipenga cha kuanza mjadala huo, wengi wa waliosimama hawakuwa na haja ya kuzungumza jema la muungano huo, wengine kwa hamasa kabisa walitamka wazi wazi kwamba muungano si tu umeoza na unanuka; bali Wazanzibari hawautaki hata uwe karibu yao.
Katika juhudi za mwisho na kuonyeshwa kukatishwa tamaa, watoa maoni waliokuwa wakitetea hoja ya kubaki na muungano huo, ambao kwa muda mwingi na hamu ya kutoa maoni uliongozwa na Bwana Gervas Budidi ambaye alijitambulisha kwamba ni Mtanzania, alisitiza kwamba haoni kama Nyerere alikuwa na nia yoyote mbaya katika uundwaji wa Muungano huo na kwamba ulikuwa ‘purely economic’ kama ilivyo miungano mingi tu. Na ni vyema zikarekebishwa kasoro tu zilizopo katika muungano huu na si vyema kuuvunja kwani una faida nyingi.
Hayo yalikuja baada ya mtoa mada wa mwanzo, Maalim Abdalla ambaye ni mlezi wa ZAWA kuelezea kwa kina kiini hasa cha muungano huu, hila chafu zilizotumika kuuleta na kwa nini hivi sasa Wazanzibari hawautaki.
Mmoja wa wachangiaji alitoa mfano wa faida hizo kwa Wazanzibari kwamba Wapemba wanaofanya shughuli zao Kariakoo, DaresSalam – ni ushahidi mmoja wapo wa faida hizo. Maoni ambayo yalisababisha minong’ono na majibu ya hasira kutoka kwa wengi waliohudhuria.
“…msituletee ujinga wenu hapa, kwani nyinyi mmekatazwa kutafuta riziki?” alimaka mmoja wa wachangiaji hoja.
Ukumbi ulianza kupata homa aliposimama mtoa mada wa tatu, Rashid ambaye ni mmoja wa viongozi wa Zawa na kuanza wazi wazi bila kutafuna maneno kuwaita makatili, wezi na wakandamizaji wa haki za Wazanzibari, viongozi wote wa Tanganyika ambao wanaung’ang’ania muungano batili huku wakijua kwamba wanavitumia vyombo vya muungano vikiwemo Raisi wa Muungano, Bunge na taasisi zote za Muungano kuifaidisha Tanganyika iliyojificha ambayo ipo. Vyombo ambavyo ni vyetu sote lakini Zanzibar hawazioni faida zake. Na akahoji kama Tanganyika haipo ni chombo gani kinachoshughulikia masuala yasiyo ya Muungano katika hiyo inayoitwa Tanzania kama si kujificha kwa Tanganyika na kuidhulumu kwa makusudi Zanzibar haki zake?
Mwendesha mjadala kwa mara kadhaa alilazimika kuinuka na kuanza kumpa vikaratasi vya kumuhimiza muda kwamba unamalizika na kupelekea kufupisha ujumbe wake ambao kwa hamasa kuu ulikua ni wa kuuponda muungano huo. Na kwa maoni yake binafsi wazi wazi akisema yeye hautaki hata kuusikia muungano huo, kwani hauna chembe ya nia njema kwa Wazanzibari.
Tahanani na mdadi ukapanda zaidi pale Ustadh Mbarak alipokuja na pendekezo lake la kuidai Zanzibar ambayo ni ya kabla ya hata ukoloni. “kwa nini tusidai Zanzibar ambayo ilikuwepo kabla ya ukoloni” alihoji na kupelekea maoni kutoka kwa mchangiaji ambaye kuna wakati alishindwa kujizuia na kuanza kusema kwa makelele licha ya kuwa amepewa na spika ya kusemea pia.
“tatizo tulilonalo kati yenu nyinyi na sisi Watanganyika kama mnavyotuita ni mkate tu… tuzungumzie hilo, na sio Zanzibar hiyo kabla ya ukoloni nani hivi sasa atatoa nchi yake” alihoji Bwana Kanguso mchangiajia ambaye baadhi ya wakati hakuweza kujizuia kuonyesha upenzi wake kwa Tanzania na kuanza kusema kwa kelele “…I support the point, I support the point..” kila lilipokuwa likizungumzwa la kusapoti muungano huo, na kusababisha wahudhuriaji kuanza kubishana naye na muongoza mjadala, Ahmed kuutuliza ukumbi kwa zogo lililoanza kutimka ukumbini hapo.
ZAWA katika hitimisho lake ililitoa matamko kadhaa ambayo yote kwa ujumla wake ni kurudishwa kwa suala hili la Muungano kwa wananchi , waulizwe upya kama bado wanauhitaji muungano na kama wanauhitaji ni muungano wa aina gani.
Mjadala huo ulirushwa live kupitia redio Mzalendo, na Wazanzibari wengi walionyesha shauku ya kutaka kutoa maoni yao.
Kwa mujibu wa ZAWA huu utakuwa ni mwanzo na si mwisho na ni muendelezo wa kudai haki za Zanzibar na ‘moto wa kudai haki za Wazanzibari’ hautozima katu hadi haki hizo zirudishwe. Na katika hilo ZAWA pia itasheherekea uhuru wa Zanzibar kila ifikapo tarehe ya uhuru huo kwani haioni sababu yoyote kwa nini isisheherekewe.
Huku tukisubiri sherehe za kutimia miaka 47 ya Muungano huo, ambao mara hii kitaifa zitafanyika Zanzibar; tutege sikio je nini kitajiri wakati hamasa na hisia za Wazanzibari na viongozi wao zimeanza kujitokeza wazi wazi kuupinga muungano huu. Sita nusura aghumiwe; je wengine hawatopatwa na maradhi ya moyo siku hiyo iwapo litatokea wasilolitarajia?
 

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
0
Written by mkulima // 24/04/2011 // Habari // No comments

Suala la Muungano uwepo au usiwepo ni dogo tu ikiwa Wawakilishi wetu watataka kuwa hivyo lakini kilichojitokeza ktk Baraza la Uwakilishi nikuwa kuna kambi 2 ndani ya Baraza ambazo 1 inataka Mungano uwepo ambao wajumbe wake wengi ni ccm na wengi wa wajumbe ni watu wenye asili ya Makundushi ambao akiwemo Spika na mawaziri wengi wa Muungano ambao vile vile ni wajumbe wa Baraza la Uwakilishi mfano Mh Nahodha na Mh Samia Suluh hawa wawili wamesikilikana hazarani kusema kuwa nafasi ya Uraisi wa Zanzibar 2020 itakuwa ni Nahodha au Samia.
Kwa hio Wzanzibar kama Baraza litaamua Muungano usiwepo basi Serekali ya Tanganyika haitokuwa na uwezo wowote wakuweza kuzuia hilo au kuwahukumu wajumbe wa Baraza kwa mamudhi hayo na Serekali ya Tanganyika itarudi.
Lakini suala hili limekuwa kumu kuamuliwa ktk Baraza kwa kuwa upande wa nyadhifa nyingi za Serekali zimeshikiliwa na watu wa makundushi akiwemo Spika wa Baraza na kuzuia harakati zozote ktk Baraza au nje ya Baraza kutolewa fursa ya kujadiliwa na Wzanzibar masuala ya Muungano, hii imekuja kuwa pindipo Muungano ukivunjika hafu ya watu wa upande huo itakuwa nitabu kushikilia nafasi nyingi za uongozi ktk Serekali ya Zanzibar.
Kwa hio suala la kuvunja Muungano tunalo sisi wenyewe kuwa tayari kufanya hivyo na ni simple tu hata dakika 10 hazifiki tunaweza kuvunja Muungano ama kutumia Baraza BLM au kurudishwa suala kwa Wzanzibar wenyewe kutowa mamudhi ambayo sio siri jawabu la Wzanzibar ni Muungano hawautaki hata kusikia harufu.

Baraza la Uwakilishi na Wajumbe wa Baraza

Yakiwashinda mambo wajumbe wa BLW rudisheni kwetu kwa kura ya maoni."][/caption]
 

Sigma

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
5,017
1,195
Wazanzibari hawataki Muungano.
Watanganyika hawautaki Muungano.
Nani kumbe anayeutaka?
Hebu tusubiri April 26, hotuba za marais wa JMT na ZnZ.
 

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,376
2,000
kimsingi Tanganyika tunanyonywa na hao wazanzibar, utaona viongozi wengi wakubwa kwenye itifaki ni kutoka zanzibar, wabunge wote wa pemba jumla ya kula zao ni sawa na mbunge mmoja wa tanganyika na tena wana haki sawa ya kupiga kura bungeni, mkopo sawa wa gari, mshahara sawa!! sasa huoni ni unyonyaji? makamu wa rais wawili, rais wa zanzibar, makamu wa rais tanganyika wote vyeo vya juu ni wazanzibar na wanalipwa pesa za muungano, sie tuna kikwete. bora tuwe na tanganyika yetu na wao wakabaki na zanzibar yao.
Mkuu,
Kuna gharama katika kuitawala nchi nyengine. Kwa hiyo Tanganyika lazima iingie gharama katika mission yake ya kuleta nchi moja,serikali moja.
Baada ya mission accomplished,hapo tutahisabu faida tu. hakutokuwa na hasara tena!
Lakini uhuru wa nchi unanunuliwa kwa shillingi ngapi? We buy it really cheap!! Kama ni kwa kuwalipa viongozi wa Zanzibar wachache tu.
 

hKichaka

Senior Member
Apr 23, 2011
199
0
Wana JF naomba mawazo yenu jamani huu mungano ni wa viongozi au ni kwetu sisi raia maana nimeshindwa kuelewa mara serikali moja ,au mbili au tatu au basi hata 20 lakini sisi wananchi unatusaidia nini?
 

mwanaone

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
637
1,000
Wazanzibari hawataki Muungano.
Watanganyika hawautaki Muungano.
Nani kumbe anayeutaka?
Hebu tusubiri April 26, hotuba za marais wa JMT na ZnZ.
jamani siku zote hatutaona umuhimu wa kitu mpaka pale tutakapokikosa. kujenga nyumba ni kazi na huchukua muda mrefu kuliko kubomoa. mimi maoni yangu muungano uendelee. ila cha msingi uwe muungano wenye maslahi ya pande zote mbili usiwe muungano wa kuunyonya au wa kuuonea upande mmoja. nchi zote ulimwenguni zinaangalia uwezekano wa kuungana ili kujenga uchumi nchi zao kwani sisi tufikirie kutengana. kinachopaswa ni kuungalia ni zipi kasoro za muungano na kuzisahihisha ili kila upande uwe na furaha na muungano. jamani haya ni ya maoni yangu kama mtanzania na siku najivunia kuwa mtanzania na nitahisi kupungukiwa kama siku itabidi nijiite mtanganyika kwangu mimi wazinzibari ni ndugu zangu na watanganyika ni ndugu zangu. na sioni fahari kujiita mtanganyika wala mzanzibari naona fahari kujiita mtanzania. muungu ibariki tanzania, mungu ibariki africa mungu tuuondoleo viongozi wote wenye kukandamiza haki zetuna kujali maslahi yetu. MUNGU TUDUMISHIE MUUNGANO WETU NA UTUPE HEKIMA ZITAZOTUSAIDIA KUUIMARISHA MUUNGANO WETU UWE NA MASLAHI KWA WOTE.
 

ATUGLORY

Senior Member
Mar 16, 2011
166
170
Ni kweli Ndugu wametuchosha sana wafunge virago waondoke na mwinyi na mtoto wake na wabunge wao na wapemba wao woteeee!

Mwende, mwende na mwende!!
 
Top Bottom