Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,277
- 105,478
Hili swala nalipa nafasi ndogo sana kwa sababu wakati yuko chuo alikuwa mchezaji mzuri sana sana mpaka kufikia kuwa drafted namba 2, na alifanya vizuri kwa urefu wake huu huu.
Hujaangalia ukweli kwamba alipokuwa chuo alikuwa anacheza katika mazingira tofauti. Huwezi kulinganisha college na NBA.
Hujaangalia kwamba inawezekana akawa na matatizo ya kiafya yanayoendana au yaliyosababisha urefu huo (kuna watu wana matezi yanayowafanya wawe warefu isivyo kawaida) ambayo yanaongezeka kadiri muda unavyoongezeka na kumpa complications zaidi with time.
Mambo ni mengi sana, tusiwe wepesi wa kusemea mambo ambayo hatuyajui vizuri.