Hasheem thabeet atemwa na timu yake mpya

Hasheem thabeet atemwa na timu yake mpya

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,481
Reaction score
36,618
Hasheem Thabeet Aondolewa Pistons:
nyota wa kikapu ndani ya NBA mTanzania ametemwa na timu yake mpya Detroit Pistons kutoka jimboni Michigan aliyojiunga nayo siku kadhaa zilizopita.......
 
Hasheem Thabeet Aondolewa Pistons:
nyota wa kikapu ndani ya NBA mTanzania ametemwa na timu yake mpya Detroit Pistons kutoka jimboni Michigan aliyojiunga nayo siku kadhaa zilizopita.......
sababu za kutemwa?
 
kwa hicho kidogo alicho make huko,awahi kuja nacho bongo,aje awekeze ktk miradi mbalimbali kabla hajafuria ile yenyewe.

Kwa urefu ule na ile profile yake ya ki-nba kuonekana mitaa ya new york anabeba box ni aibu kubwa sana kwa taifa.
well said mkuu
 
Arudi bongo tu bado tunamuhitaji
 
kwa hicho kidogo alicho make huko,awahi kuja nacho bongo,aje awekeze ktk miradi mbalimbali kabla hajafuria ile yenyewe.

kwa urefu ule na ile profile yake ya ki-NBA kuonekana mitaa ya new york anabeba box ni aibu kubwa sana kwa taifa.
haya ni mambo serious lakini imenibidi nicheke.
Alipofikia hadi sasa ni pakubwa japo inapendeza akienda zaidi ya hapo maana hata akina Jordan enzi yao iliisha.
Ushauri uliompa ni mzuri kwa maana hao 'mastaa wastaafu' wa NBA wanaishi maisha mazuri baada ya kustaafu hata zaidi ya walipokuwa wakicheza. Hiyo ni sababu walijua kuwekeza nyakati wako vizuri.

kwa hicho kidogo alicho make huko,awahi kuja nacho bongo,aje awekeze ktk miradi mbalimbali kabla hajafuria ile yenyewe.

kwa urefu ule na ile profile yake ya ki-NBA kuonekana mitaa ya new york anabeba box ni aibu kubwa sana kwa taifa.

sidhani kama ana haja ya kukata tamaa kiasi hicho,nashauri aendelee kujifua zaidi arudishe kiwango,bado ni kijana mdogo mno kurudisha majeshi nyuma.andelee kupigana,askari hakati tamaa kirahisi hivyo.komaa mkuu,kila la kheri
 
Sasa akimbilie Euroleague Basketball akabangaize huko maana sioni dalili za kuinua kiwango na kupata timu nyingine soon na msimu bado wiki uanze
 
Hamna NBA ya daraja la pili huko? Au aende Spain ama england?
 
sijui kwanini huwa anashuka kiwango namna hiyo kila mara...au ameendekeza ile kitu
 
Ukiangalia career stats zake ni kwamba kwa kiwango cha NBA Hasheem huwa ni reserve, na mara nyingi ni 3rd option center. Kweli inafaa aende nje ya NBA kama Euroleague au China atakuwa na nafasi zaidi ya kung'ara.
 
Hasheem Thabeet hajawahi kupenda basketball. Hili ndilo tatizo. Sikumbuki kumuona akicheza basketball alipokuwa Tanzania kabla ya kwenda Marekani. Ni Wamarekani waliyembembeleza acheze basketball baada ya kuvutiwa na urefu wake lakini kwa kifupi ni mtu ambaye hana mapenzi na mchezo huo.
 
kwa hicho kidogo alicho make huko,awahi kuja nacho bongo,aje awekeze ktk miradi mbalimbali kabla hajafuria ile yenyewe.

kwa urefu ule na ile profile yake ya ki-NBA kuonekana mitaa ya new york anabeba box ni aibu kubwa sana kwa taifa.
Atarudi kivipi na ana mtoto na mmarekani?hizo hela ni zao jamaa hata akirudi atarudi mikono mitupu.awaulize Wesley Snipes na Mike Tyson wampe dondoo.
 
Back
Top Bottom