Hasara za NHIF kila Mwaka: Sababu nyingine ni baadhi ya watendaji kujimilikisha mfuko

HustlerD

Senior Member
May 15, 2021
131
425
Si kosa wala si vibaya kuwapa mamlaka ya kiuongozi vijana ili kuandaa viongozi wa kesho wenye weledi katika taifa hili

lakini vijana hawa wanaoaminiwa na taasisi wamekua chanzo cha kuitia hasara serikali na kurudisha nyuma mipango mizuri ya serikali yetu kwa tamaa ya maendeleo ya haraka, uzembe wao wa moja kwa moja au kwa kutojitambua

kwa tathmini hii ya PIC, nimesikitika na kuamua angalau kutolea mfano wa hali halisi katika ofisi za mfuko huu

Nitatolea mfano wa Meneja wa mkoa wa mfuko wa taifa wa bima ya afya(NHIF), mkoa wa Mwanza
Huyu kwa kumwangalia ni kijana wa makamo na nafikiri kwa taarifa zilizopo hana muda mrefu sana katika nafasi hiyo aliyoachiwa na mtangulizi wake aliyekuwepo ambaye kusema ukweli aliitendea haki nafasi hiyo.

Lakini huyu wa sasa amekua chanzo cha kurudisha nyuma maendeleo ya taasisi za afya katika ukanda ule kuanzia ngazi ya zahanati mpaka hospitali kubwa ya Kanda Bugando, nitaelezea kidogo.

1. Kwanza toka aingie huyu malipo ya claims za bima yamekua hayatoki kwa wakati tofauti na ilivyokua kama mwaka mmoja uliopita, kwa sheria za NHIF Mdai anatakiwa kulipwa deni lake ndani ya siku tisini(miezi mitatu) toka awasilishe madai yake, lakini hivi sasa kuna madai yana mpaka miezi nane, na si kituo kimoja wala viwili, hoja yake kubwa ni kusingizia mfumo na kusema mfuko hauna hela, hivyo wagonjwa wengi wamekua limited sana kwenye vipimo na matibabu wanayopata kupitia Bima ya NHIF, na hivyo kuleta usumbufu kwa wagonjwa,
alipe vituo pesa kwa wakati ili pia kuongeza ufanisi wa mfuko kwa kuongeza mzunguko wa fedha.

2. Mzee wa percent(10%), ukiachilia mbali kisingizio cha mfuko hauna hela, lakini kuna taarifa za chini kwa chini kua hao wadai wakitaka kulipwa haraka, basi inawabidi kumufuata ofisini(yeye au baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo) na kukubaliana nae angalau atapewa asilimia ngap ya malipo baada ya ku enforce malipo yako, na kwa ushahidi kuna baadhi ya watumishi wamesimamishwa kupisha uchunguzi

3. Kushindwa kuwasimamia doctors na idara nyingine za afya waliopo pale kwa ueledi, na kutengeneza watumishi wenye viburi na kujisikia, mfano kuna kesi ya dakitari mmoja alifukuzwa kituo X alipoenda kufanya ukaguzi baada ya kumtolea lugha chafu mmiliki wa kituo na meneja analifahamu hilo,

4. Kutokua na umakini katika kusimamia rasilimali fedha, kuna taarifa kua yeye na wenzake wamekua wakijikopesha pesa za mfuko kujinunulia magari ya kifahari na kutokuzirejesha kwa wakati na yeye kuishi maisha ya anasa ya kuzurula kwenye sehemu za starehe na vipensi (aibu sana kwa mkuu wa taasisi) wakati anachokisimamia kinapumulia mashine, wakati mwingine sisi serikali inatakiwa pia tutumie akili ya kawaida kulinganisha kipato cha mtumishi na aina ya maisha anayoishi, tutagundua kama anaisaidia serikali kusonga mbele au anaikwamisha.

TAKUKURU na taasisi nyingine za kiuchunguzi kazi kwenu, mengine mkifika pale ofisini mtajionea.

Hivyo kwa tathmini ya PIC, anzeni na uchunguzi kwa watu kama hawa wanalirudisha nyuma taifa letu kwa kuongoza na kufanya ofisi za umma kama nyumbani kwao.

Ni hayo tu
 
Back
Top Bottom